Na Thompson Mpanji,Mbeya
MATUKIO ya ajali yameendelea kuundama Mkoa wa Mbeya
baada ya wananchi wa Kijiji cha Imezu kata ya Inyala wilaya
ya Mbeya Vijijini leo kulazimika kufunga bara bara ya Mbeya
Dar es Salaam kwa takribani saa sita baada ya kutokea ajali iliyoua
watoto wawili wa chekechea wanaokadiriwa kuwa na umri wa miaka
mitano mpaka sita.
Kamanda wa kikosi cha usalama barabarani Mkoa wa Mbeya
(RTO) Butusyo Mwambelo amewataja Watoto hao kuwa ni ,Timotheo Omary (5)
na Thadeo Braiston Malila (5) ambapo kati ya watoto hao mmoja
tayari mazishi yake yamefanyika na mwili wa mtoto mwingine utasafilishwa
kwenda kijiji cha uwanji Matamba Wilayani Makete.
Amesema kuwa tukio hilo limetokea majira ya saa
1.15 asubuhi baada ya watoto hao kugongwa na gari aina ya yenye namba
za usajili T 798 BVY tela T698 BVA lilokuwa kiendeshwa
na Dominick Mwakalundwa (34) mabibo dar e s salaam lililokuwa
likitokea Mbeya kwenda Mkoani Iringa liligonga watoto hao waliokuwa
pembeni ya bara bara wakitoka shule na kwamba aliokolewa na askari Polisi baada
ya wananchi kutaka kumshambulia..
Wakizungumza na Radio
five na matukio katika eneo la ajali
hiyo Wananchi hao, wamesema kuwa waliamua kuchukua uamuzi huo
baada ya kuchoshwa na ahadi za serikali kupitia wakala wa bara bara
za kuweka matuta katika eneo hilo la la shule ili kuepusha
ajali ambazo zimekuwa zikitokea mara kwa mara .
Bw.Michael Mashamba mkazi wa kijiji cha Imezu amesema kuwa
baada ta tukio hilo kutokea wananchi walijaa eneo la ajali na kuanza
kufunga bara bara kwa kutumia magogo na mawe ili kuzuia magari
yasipite eneo hilo kwa lengo la kushinikiza serikali kuweka matuta ili kuzuia
ajali kutokana na madai ya kufariki watu zaidi ya 30 kwa ajili katika maeneo
hayo.
Hata hivyo baada ya tukio hilo Mkuu wa Wilaya ya Mbeya
Dkt. Norman Sigalla aliwaomba wananchi kufungua bara bara
wakati serikali kwa kushirikiana na wakala wa bara bara (TAN ROADS) ikiwa
inaweka utaratibu wa kuweka matuta hayo haraka iwezekanavyo.
Aidha Sigalla ameliagiza jeshi la polisi Mkoani hapa
kuwachukulia hatua kali madereva watakoendesha magari kwa mwendo
kasi na kwamba watozwe faini na adhabu kali ambayo itawafanya wawe na
nidhamu na askari wasiwe marafiki wa madereva.
Mwisho
No comments:
Post a Comment