Na Thompson Mpanji,Mbeya
WAKULIMA nchini wameshauriwa kujenga utamaduni wa kudai lisiti
wakati wa kununua mbegu za mazao ya aina mbalimbali katika maduka ya
pembejeo yanayotambulika ili kuepuka kuuziwa mbegu feki ambazo
zimetapakaa na kuwaletea hasara kubwa wakulima walio wengi sanjari na
kuhatarisha maisha ya walaji.
Aidha imeleezwa kuwa mbegu za mahindi ya njano ambazo zinadaiwa
kutoa unga wa njano baada ya kusagwa zinazodaiwa kusambazwa kwa wakulima
walio wengi wilayani Mbozi zinatumika kwa ajili ya malisho ya mifugo na
siyo kwa binadamu.
Akizungumza na gazeti hili Mtafiti wa zao la mahindi kutoka taasisi
ya utafiti kanda ya nyanda za juu kusini (ARI Uyole), Anderson
Elibariki Temu alisema mbegu za mahindi zenye rangi ya njano ni mojawapo
ya aina inayopendelewa sana nchini Marekani na imekuwa ikitumika kwa
ajili ya vyakula vya kuku na ng’ombe wa maziwa.
Mtafiti huyo alisema ingwa hajabahatika kuyaona mahindi hayo
yanayozungumziwa lakini kutokana na maelezo aliyoyapata ana uenda
yalizalishwa kwa ajili ya mifugo na siyo kwa ajili ya chakula cha
binadamu.
"Lakini nawashauri wakulima kwa kuona tatizo hilo na mbegu
hazijifichi inatakiwa wakulima wawe makini wawe waangalifu wakati wa
kununua mbegu kwa sababu hii imekuwa ni kero kubwa kwa wakulima wa kanda
ya nyanda za juu kusini na Tanzanja kwa ujumla Mkulima anapojitahidi
kuwa na mtaji hadi kununua mbegu, anaipanda,gharama za mbolea
,maandalizi ya shamba na gharama nyingine alafu mwisho anaikuta mbegu
aliyoipanda kwa mfano siyo Uyole Hybrid 615 ni hasara kubwa,"alisema.
Temu alisema ili mkulima aweze kukwepa udanganyifu huo anapaswa
anapoenda kununua mbegu ahakikishe mbegu ipo kwenye mifuko ya kampuni
halisia inayozalisha hiyo mbegu mfano kampuni inayozalisha mbegu za
uyole ya Highland seed growers ambapo nje ya mfuko kuna anuani na jina
la kampuni,na kwamba akwepe kununua mbegu zinazouzwa baada ya
kufunguliwa katika mfuko .
Alisema Mkulima naweza kununua mbegu iliyokuwepo katika mifuko kwa
sababu wanaweza kuiba mifuko ama kutumia ujanja wowote,kwa hiyo njia ya
mwisho ya kuwabana wauzaji wa mbegu feki ni kudai lisiti na kuitunza
hadi wakati wa msimu wa amvuno.
"ili tatizo likijitokeza la mbegu kutokuwa halisi nenda kwa ofisa
shamba ukikutana na tatizo atakuelekeza ngazi na utaratibu wa kufuata
ili mhusika weze kufuatiliwa na ikibidi sheria ichukuwe mkondo wake kwa
sababu sheria zipo kuanzia kuzalisha mbegu kuhakikisha zina ubora na
mamlaka husika zinazofuatilia zipo,hakikisha una lisiti hadi mwisho wa
msimu,"alisisistiza Mtafiti huo.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment