Translate

Monday, November 26, 2012

JWTZ 10 mbaroni kwa kuuwa na kujeruhi Mbeya

Na Thompson Mpanji,Mbeya

ASKARI 10 wa Jeshi la wananchi (JWTZ) kikosi cha 44kj Mbalizi,wanashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa tuhuma za  mauaji  na kujeruhi watu wengine sita sanjari na kuharibu mali mbalimbali.

Kamanda wa polisi Mkoa wa Mbeya,Diwani Athumani amethibitisha kutokea kwa kifo hicho  Nov,18 majira ya saa 5 usiku  katika hospitali teule ya Ifisi wilaya ya mbeya vijijini mkoa wa mbeya na amemtaja marehemu kuwa ni Petro Sanga,( 25),mkulima,mkinga, mkazi wa chapakazi, mbalizi ambaye  alifariki dunia wakati akiendelea kupatiwa matibabu hospitalini hapo.

Athuman amesema  marehemu alichomwa kisu shingoni na mdomoni na kikundi cha watu  wanaosadikiwa kuwa askari wa jeshi la wananchi wa Tanzania, tarehe  hiyo majira ya saa 3 usiku akiwa katika grocery  iitwayo vavene mwe   iliyopo mbalizi mara baada ya  watu hao kuvamia bar iitwayo power night club ambamo awali alikuwepo pia marehemu.

Amesema watu wengine sita  walijeruhiwa kwa kupigwa sehemu mbalimbali za miili yao  na wanaodaiwa kuwa askari wa JWTZ na kupatiwa hati ya matibabu [pf3] kwa matibabu kati yao watatu walilazwa katika hospitali teule ya ifisi kwa matibabu zaidi na  majeruhi wengine watatu walipatiwa matibabu na kuruhusiwa.

Kamanda huyo amesema  kufuatia vurugu hizo baadhi ya mali za watu ziliharibiwa ambazo ni pamoja gari T.106 AWB aina ya toyota vista mali ya Paulo Maximilian ilivunjwa kioo cha mbele,gari T.884 AUU Toyota Cresta mali ya Alile Godfrey lilivunjwa side mirror upande wa kulia.  

Kamanda huyo amesema kuwa  wahalifu hao walianza kuwashambulia wananchi kwa kuwapiga wakitumia ngumi, mateke, mikanda, marungu, sime na mapanga na kwamba  marehemu  alijaribu kuokoa uhai wake kwa kukimbia toka eneo hilo hadi   katika grosary hiyo lakini watu hao walimkimbiza hadi eneo hilo na kumjeruhi vibaya kwa kumchoma kisu.

Amesema chanzo cha tukio hilo ni kulipiza kisasi kufuatia askari Godfrey Matete( 30),mjita, wa kikosi cha 44kj mbalizi kupigwa na walinzi wa kilabu cha pombe za kienyeji kiitwacho DDC kilichopo mbalizi  waliokuwa lindoni Nov,17,2012 majira ya saa 01:30.

Amefafanua kuwa  baada ya kushambuliwa  askari huyo alifungua kesi kituo cha polisi mbalizi usiku huo  kosa la kujeruhi na alipatiwa hati ya matibabu [pf3] kwa ajili ya kwenda kupata matibabu hospitalini ambapo walinzi wanne walikamatwa  kuhusiana na tukio hilo  kwa mahojiano.

Amewataja walinzi hao kuwa ni Frenk Mtasimwa (25),Mure Julias (26),Omari Charles (28) wote wakazi wa DDC mbalizi na  Legnard Mwampete (30),mkazi wa Izumbwe na kwamba  upelelezi wa kesi hiyo bado unaendelea.

Mwisho.

No comments:

Post a Comment