TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA
MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI
“PRESS RELEASE” KUHUSIANA NA HALI YA
UHALIFU KWA MWAKA, 2013.
§
JUMLA YA MAKOSA
YOTE YA JINAI YALIYORIPOTIWA KATIKA KIPINDI CHA MWAKA 2013 YALIKUWA NI 22,262
IKILINGANISHWA NA MAKOSA 29,722 YALIYORIPOTIWA
KIPINDI KAMA HICHO MWAKA 2012.
§
KATI YA MAKOSA
HAYO MAKOSA MAKUBWA YALIKUWA 2,213
WAKATI KIPINDI KAMA HICHO MWAKA 2012
MAKOSA MAKUBWA YALIKUWA 2,283.
§
MAKOSA
YATOKANAYO NA JITIHADA ZA JESHI LA POLISI KWA KUSHIRIKIANA NA WANANCHI NA WADAU
WENGINE KUPITIA MISAKO/DORIA KWA MWAKA 2013
YALIKUWA 430, WAKATI KIPINDI KAMA
HICHO MWAKA 2012 YALIKUWA 416.
§
KWA UPANDE WA
MAKOSA YA USALAMA BARABARANI, JUMLA
YA MAKOSA YOTE YA AJALI PAMOJA NA UKIUKWAJI WA SHERIA ZA
USALAMA BARABARANI YALIKUWA 46,565,
WAKATI KIPINDI KAMA HICHO MAKOSA 54,304 YALIRIPOTIWA.
§
MATUKIO YA AJALI
KWA MWAKA 2013 YALIKUWA 490, WAKATI KIPINDI KAMA HICHO MWAKA 2012 YALIKUWA 606.
§
AJALI
ZILIZOSABABISHA VIFO MWAKA 2013
ZILIKUWA 276, WAKATI KIPINDI KAMA
HICHO MWAKA 2012 ZILIRIPOTIWA AJALI 606.
§
WATU WALIOKUFA KUTOKANA NA AJALI MWAKA 2013 WALIKUWA 329, WAKATI KIPINDI KAMA HICHO MWAKA 2012 WALIKUFA WATU 323.
§
AJALI ZA MAJERUHI MWAKA 2013 ZILIKUWA 214,
WAKATI KIPINDI KAMA HICHO MWAKA 2012
ZILIRIPOTIWA AJALI 352.
§
WATU WALIOJERUHIWA KATIKA AJALI MBALIMBALI
MWAKA 2013 WALIKUWA 649, WAKATI KIPINDI KAMA HICHO MWAKA 2012 WALIKUWA WATU 875.
§
PESA ZILIZOKUSANYWA KUTOKANA NA MAKOSA MBALIMBALI
YA UKIUKWAJI WA SHERIA ZA USALAMA
BARABARANI [NOTIFICATION] MWAKA 2013
ZILIKUWA TSHS 1,219,020,000/= WAKATI
KIPINDI KAMA HICHO MWAKA 2012
ZILIKUSANYWA PESA TSHS 1,440,150,000/=
§
BAADHI YA SABABU ZA KUONGEZEKA KWA MATUKIO YA AJALI NI KUONGEZEKA
KWA VYOMBO VYA USAFIRI MKOANI MBEYA
HASA MAGARI NA PIKIPIKI, BAADHI YA MADEREVA
KUTOKUZINGATIA SHERIA ZA USALAMA BARABARANI IKIWA NI PAMOJA NA MWENDO KASI HASA
USIKU NA ULEVI LICHA YA JITIHADA ZA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA
KUSHIRIKIANA NA BAADHI YA WADAU KUTOA
ELIMU HIYO MARA KWA MARA PAMOJA NA HALI YA
HEWA HUSUSANI UKUNGU NA UTELEZI KATIKA BAADHI YA MAENEO YA
BARABARA YA MBEYA/RUNGWE/KYELA.
§
BAADHI YA MAFANIKIO AMBAYO JESHI LA POLISI MKOA WA
MBEYA KWA KUSHIRIKIANA NA WANANCHI YAMEPATIKANA NI PAMOJA NA :-
v
KWA UJUMLA HALI
YA UHALIFU MKOA WA MBEYA KWA MAKOSA YOTE YA JINAI MAKUBWA NA MADOGO UMEPUNGUA KWA ASILIMIA 25.
v
MATUKIO YA AJALI
YAMEPUNGUA KWA ASILIMIA 19.
v
POMBE HARAMU YA MOSHI [GONGO] UJAZO WA LITA 583 NA MITAMBO MINNE ILIKAMATWA.
v
BHANGI YENYE
UZITO WA KILO 1,096 NA GRAM 786 PAMOJA NA MASHAMBA MAWILI
YENYE UKUBWA WA EKARI MOJA NA NUSU
ILIKAMATWA.
v
MIRUNGI UZITO WA
KILO 1 NA GRAM 500 ILIKAMATWA.
v
MADAWA YA KULEVYA
KILO 1 NA GRAM 404.6 YALIKAMATWA.
v
SILAHA /BUNDUKI 35 ZILIKAMATWA KATI YA HIZO SMG 3,S/GUN 5,GOBOLE 21,SAR 1,BASTOLA
ZILIZOTENGENEZWA KIENYEJI 3 NA RIFFLE 2.
v
JUMLA YA RISASI 193 ZILIKAMATWA, KATI YA HIZO RISASI
38 ZA SMG/SAR, RISASI 130 ZA S/GUN NA RISASI 25 ZA BASTOLA.
v
SARE ZA JWTZ “KOMBATI” SURUALI 4, MASHATI 4, KOFIA
3 NA VIATU /MABUTI JOZI MBILI ZILIKAMATWA.
v
JUMLA YA SILAHA AINA YA GOBOLE 174 ZILISALIMISHWA MAENEO MBALIMBALI
WILAYA YA CHUNYA KUFUATIA AGIZO LA KAMATI YA
ULINZI NA USALAMA WILAYA HIYO KUAGIZA WAMILIKI WOTE WA SILAHA HIZO
KUFANYA HIVYO.
v
NYARA ZA SERIKALI ZENYE THAMANI YA TSHS
103,362,00/= NA USD 4,445
ZILIKAMATWA.
v
NOTI BANDIA 1,521 @TSHS 10,000/= SAWA NA TSHS 15,210,000,NOTI 19 @ TSHS 5,000/= SAWA NA TSHS
95,000/= NA DOLA 70 ZA KIMAREKANI @ DOLA 100 SAWA NA DOLA
7,000 ZILIKAMATWA.
PAMOJA NA MAFANIKIO HAYO LAKINI PIA
KUNA BAADHI YA CHANGAMOTO ZINAZOLIKABILI JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA.
CHANGAMOTO HIZO NI PAMOJA NA:-
-
KUONGEZEKA KWA
MATUKIO YA MAUAJI KWA ASILIMIA 10 IKILINGANISHWA NA KIPINDI KAMA HICHO MWAKA
2012. ONGEZEKO HILO
LINATOKANA NA KUKITHIRI KWA MAUAJI YA IMANI POTOFU ZA KISHIRIKINA NA
KUJICHUKULIA SHERIA MKONONI [WIZI] PIA KUTOKANA NA HALI NGUMU YA KIUCHUMI.
AIDHA KATIKA KIPINDI CHA MWAKA 2013 KULITOKEA MATUKIO MATATU YA WATU WANNE
KUUAWA KWA KUZIKWA WAKIWA HAI KUTOKANA NA IMANI POTOFU ZA KISHIRIKINA [UCHAWI].
-
KUONGEZEKA KWA
MATUKIO YA KUBAKA KWA ASILIMIA 64 IKILINGANISHWA NA KIPINDI KAMA
HICHO MWAKA 2012. SABABU ZA KUONGEZEKA NI PAMOJA NA TAMAA ZA KIMWILI, ULEVI NA
HALI NGUMU YA KIUCHUMI.
-
KUONGEZEKA KWA
MATUKIO YA WIZI WA PIKIPIKI KWA ASILIMIA 56 IKILINGANISHWA NA KIPINDI KAMA HICHO MWAKA 2012. SABABU IKIWA NI PAMOJA NA TAMAA YA
KUJIPATIA KIPATO KWA NJIA HARAMU.
WITO WA KAMANDA:
KAMANDA
WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI
ANATOA PONGEZI KWA WANANCHI WOTE WA MKOA
WA MBEYA KWA USHIRIKIANO WAO WA DHATI KWA JESHI LA POLISI KATIKA MAPAMBANO
DHIDI YA UHALIFU NA WAHALIFU KUPITIA
DHANA YA ULINZI SHIRIKISHI NA POLISI
JAMII KATIKA KIPINDI CHOTE CHA MWAKA
2013. AIDHA ANATOA RAI KWA JAMII KUENDLEA KUSHIRIKIANA NA JESHI LA POLISI
KATIKA KIPINDI CHA MWAKA 2014.
PIA
KAMANDA MSANGI ANATOA WITO KWA JAMII HASA WAHALIFU KUACHA TABIA YA KUWA NA TAMAA YA UTAJIRI WA HARAKA KWA NJIA YA MKATO/HARAMU BADALA YAKE WAJISHUGHULISHE KWA
KUFANYA KAZI HALALI NA KUPATA KIPATO HALALI KWA KUZINGATIA MKOA WA MBEYA UNAZO
FURSA NYINGI ZA KIUCHUMI IKIWA NI PAMOJA NA HALI YA HEWA. ANATOA RAI PIA KWA VIONGOZI WA MADHEHEBU YA DINI, VIONGOZI WA SERIKALI, VYAMA
VYA SIASA, MACHIFU, WAZEE WA MILA NA WATU MASHUHURI MKOANI
MBEYA KUSHIRIKIANA NA JESHI LA POLISI KWA KUTOA
ELIMU ZAIDI KWA JAMII ILI IEPUKANE NA IMANI POTOFU ZA KISHIRIKINA. AMEWATAKA
PIA MADEREVA KUENDESHA VYOMBO VYA MOTO KWA KUZINGATIA SHERIA NA ALAMA ZA USALAMA BARABARANI
ILI KUEPUKA AJALI ZINAZOWEZA KUEPUKIKA KWANI ZINARUDISHA NYUMA MAENDELEO YA JAMII
NA HATA NGUVU KAZI YA TAIFA.
PIA ANATOA SHUKRANI KWA VYOMBO VYA
HABARI VYA NDANI NA NJE YA MKOA WA MBEYA KWA USHIRIKIANO WENU NA KUWATAKA KUENDELEA NA HALI HII KWANI IMELETA
MAFANIKIO MAKUBWA KATIKA KUFIKISHA HABARI KWA WAKAZI WA MBEYA NA TAIFA KWA
UJUMLA. AIDHA NATOA WITO KWA WAANDISHI WA HABARI KUFUATA NA KUZINGATIA MAADILI
YA UANDISHI WA HABARI [MEDIA ETHICS] ILI
KUTOPOTOSHA UMMA NA KUEPUKA MADHARA KATIKA JAMII NA TAIFA.
MWISHO KAMANDA MSANGI ANAWATAKIA KHERI YA MWAKA MPYA WA
2014 WANANCHI WOTE WAKAZI WA MKOA WA MBEYA.
Signed by:
[AHMED .Z.
MSANGI - SACP]
KAMANDA
WA POLISI MKOA WA MBEYA.