Translate

Sunday, January 12, 2014

matukio ya uhalifu mwaka 2013





TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI
“PRESS RELEASE” KUHUSIANA NA HALI YA UHALIFU KWA MWAKA, 2013.

§         JUMLA YA MAKOSA YOTE YA  JINAI YALIYORIPOTIWA KATIKA KIPINDI CHA MWAKA 2013 YALIKUWA NI 22,262 IKILINGANISHWA NA MAKOSA 29,722 YALIYORIPOTIWA KIPINDI KAMA HICHO MWAKA 2012.
§         KATI YA MAKOSA HAYO MAKOSA MAKUBWA YALIKUWA 2,213 WAKATI KIPINDI KAMA HICHO MWAKA 2012 MAKOSA MAKUBWA YALIKUWA 2,283.
§         MAKOSA YATOKANAYO NA JITIHADA ZA JESHI LA POLISI KWA KUSHIRIKIANA NA WANANCHI NA WADAU WENGINE KUPITIA MISAKO/DORIA KWA MWAKA 2013 YALIKUWA 430, WAKATI KIPINDI KAMA HICHO MWAKA 2012 YALIKUWA 416.
§         KWA UPANDE WA MAKOSA YA USALAMA BARABARANI, JUMLA YA MAKOSA  YOTE YA  AJALI PAMOJA NA UKIUKWAJI WA SHERIA ZA USALAMA BARABARANI YALIKUWA 46,565, WAKATI KIPINDI KAMA HICHO MAKOSA 54,304 YALIRIPOTIWA.
§         MATUKIO YA AJALI KWA MWAKA 2013 YALIKUWA 490, WAKATI KIPINDI KAMA HICHO MWAKA 2012 YALIKUWA 606.
§         AJALI ZILIZOSABABISHA VIFO MWAKA 2013 ZILIKUWA 276, WAKATI KIPINDI KAMA HICHO MWAKA 2012 ZILIRIPOTIWA AJALI 606.
§         WATU WALIOKUFA KUTOKANA NA AJALI MWAKA 2013 WALIKUWA 329, WAKATI KIPINDI KAMA HICHO MWAKA 2012 WALIKUFA WATU 323.
§         AJALI ZA MAJERUHI MWAKA 2013 ZILIKUWA 214, WAKATI KIPINDI KAMA HICHO MWAKA 2012 ZILIRIPOTIWA AJALI 352.
§         WATU WALIOJERUHIWA KATIKA AJALI MBALIMBALI MWAKA 2013 WALIKUWA 649, WAKATI KIPINDI KAMA HICHO MWAKA 2012 WALIKUWA WATU 875.
§         PESA  ZILIZOKUSANYWA KUTOKANA NA MAKOSA MBALIMBALI YA  UKIUKWAJI WA SHERIA ZA USALAMA BARABARANI [NOTIFICATION] MWAKA 2013 ZILIKUWA TSHS 1,219,020,000/= WAKATI KIPINDI KAMA HICHO MWAKA 2012 ZILIKUSANYWA PESA TSHS 1,440,150,000/=
§         BAADHI YA  SABABU ZA KUONGEZEKA KWA MATUKIO YA  AJALI NI KUONGEZEKA KWA VYOMBO VYA USAFIRI MKOANI MBEYA HASA MAGARI NA PIKIPIKI, BAADHI YA  MADEREVA KUTOKUZINGATIA SHERIA ZA USALAMA BARABARANI IKIWA NI PAMOJA NA MWENDO KASI HASA USIKU NA ULEVI  LICHA YA  JITIHADA ZA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA KUSHIRIKIANA NA BAADHI YA  WADAU KUTOA ELIMU HIYO MARA KWA MARA PAMOJA NA HALI YA  HEWA HUSUSANI UKUNGU NA UTELEZI KATIKA BAADHI YA  MAENEO YA  BARABARA YA  MBEYA/RUNGWE/KYELA.
§         BAADHI YA  MAFANIKIO AMBAYO JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA KUSHIRIKIANA NA WANANCHI YAMEPATIKANA NI PAMOJA NA :-

v     KWA UJUMLA HALI YA UHALIFU MKOA WA MBEYA KWA MAKOSA YOTE YA JINAI  MAKUBWA NA MADOGO UMEPUNGUA KWA ASILIMIA 25.

v     MATUKIO YA AJALI YAMEPUNGUA KWA ASILIMIA 19.

v     POMBE HARAMU YA MOSHI [GONGO] UJAZO WA LITA 583 NA MITAMBO MINNE ILIKAMATWA.

v     BHANGI YENYE UZITO WA KILO 1,096 NA GRAM 786 PAMOJA NA MASHAMBA MAWILI YENYE UKUBWA WA EKARI MOJA NA NUSU ILIKAMATWA.
v     MIRUNGI UZITO WA KILO 1 NA GRAM 500 ILIKAMATWA.
v     MADAWA YA KULEVYA KILO 1 NA GRAM 404.6 YALIKAMATWA.
v     SILAHA /BUNDUKI 35 ZILIKAMATWA KATI YA HIZO SMG 3,S/GUN 5,GOBOLE 21,SAR 1,BASTOLA ZILIZOTENGENEZWA  KIENYEJI 3 NA RIFFLE 2.
v     JUMLA YA RISASI 193 ZILIKAMATWA, KATI YA HIZO RISASI 38 ZA SMG/SAR, RISASI 130 ZA S/GUN NA RISASI 25 ZA BASTOLA.
v     SARE ZA JWTZ “KOMBATI” SURUALI 4, MASHATI 4, KOFIA 3 NA VIATU /MABUTI JOZI MBILI ZILIKAMATWA.
v     JUMLA YA SILAHA AINA YA GOBOLE 174 ZILISALIMISHWA MAENEO MBALIMBALI WILAYA YA CHUNYA KUFUATIA AGIZO LA KAMATI YA  ULINZI NA USALAMA WILAYA HIYO KUAGIZA WAMILIKI WOTE WA SILAHA HIZO KUFANYA HIVYO.
v     NYARA ZA SERIKALI ZENYE THAMANI YA TSHS 103,362,00/= NA USD 4,445 ZILIKAMATWA.
v     NOTI BANDIA 1,521 @TSHS 10,000/= SAWA NA TSHS 15,210,000,NOTI 19 @ TSHS 5,000/= SAWA NA TSHS 95,000/= NA DOLA  70 ZA KIMAREKANI @ DOLA 100 SAWA NA DOLA 7,000 ZILIKAMATWA.

PAMOJA NA MAFANIKIO HAYO LAKINI PIA KUNA BAADHI YA CHANGAMOTO ZINAZOLIKABILI JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA. CHANGAMOTO HIZO NI PAMOJA NA:-

-          KUONGEZEKA KWA MATUKIO YA MAUAJI KWA ASILIMIA 10 IKILINGANISHWA NA KIPINDI KAMA HICHO MWAKA 2012. ONGEZEKO HILO LINATOKANA NA KUKITHIRI KWA MAUAJI YA IMANI POTOFU ZA KISHIRIKINA NA KUJICHUKULIA SHERIA MKONONI [WIZI] PIA KUTOKANA NA HALI NGUMU YA KIUCHUMI. AIDHA KATIKA KIPINDI CHA MWAKA 2013 KULITOKEA MATUKIO MATATU YA WATU WANNE KUUAWA KWA KUZIKWA WAKIWA HAI KUTOKANA NA IMANI POTOFU ZA KISHIRIKINA [UCHAWI].

-          KUONGEZEKA KWA MATUKIO YA KUBAKA KWA ASILIMIA 64 IKILINGANISHWA NA KIPINDI KAMA HICHO MWAKA 2012. SABABU ZA KUONGEZEKA NI PAMOJA NA TAMAA ZA KIMWILI, ULEVI NA HALI NGUMU YA KIUCHUMI.

-          KUONGEZEKA KWA MATUKIO YA WIZI WA PIKIPIKI KWA ASILIMIA 56 IKILINGANISHWA NA KIPINDI KAMA HICHO MWAKA 2012. SABABU IKIWA NI PAMOJA NA TAMAA YA KUJIPATIA KIPATO KWA NJIA HARAMU.











WITO WA KAMANDA:

KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA PONGEZI KWA  WANANCHI WOTE WA MKOA WA MBEYA KWA USHIRIKIANO WAO WA DHATI KWA JESHI LA POLISI KATIKA MAPAMBANO DHIDI YA  UHALIFU NA WAHALIFU KUPITIA DHANA YA  ULINZI SHIRIKISHI NA POLISI JAMII KATIKA KIPINDI CHOTE CHA MWAKA 2013. AIDHA ANATOA RAI KWA JAMII KUENDLEA KUSHIRIKIANA NA JESHI LA POLISI KATIKA KIPINDI CHA MWAKA 2014.

PIA KAMANDA MSANGI ANATOA WITO KWA JAMII HASA WAHALIFU KUACHA TABIA YA KUWA NA   TAMAA YA UTAJIRI WA HARAKA KWA NJIA YA  MKATO/HARAMU BADALA YAKE WAJISHUGHULISHE KWA KUFANYA KAZI HALALI NA KUPATA KIPATO HALALI KWA KUZINGATIA MKOA WA MBEYA UNAZO FURSA NYINGI ZA KIUCHUMI IKIWA NI PAMOJA NA HALI YA  HEWA. ANATOA RAI PIA KWA VIONGOZI WA MADHEHEBU YA DINI, VIONGOZI WA SERIKALI, VYAMA VYA SIASA, MACHIFU, WAZEE WA MILA NA WATU MASHUHURI MKOANI MBEYA KUSHIRIKIANA NA JESHI LA POLISI KWA KUTOA ELIMU ZAIDI KWA JAMII ILI IEPUKANE NA IMANI POTOFU ZA KISHIRIKINA. AMEWATAKA PIA MADEREVA  KUENDESHA VYOMBO VYA MOTO KWA KUZINGATIA SHERIA NA ALAMA ZA USALAMA BARABARANI ILI KUEPUKA AJALI ZINAZOWEZA KUEPUKIKA KWANI ZINARUDISHA NYUMA MAENDELEO YA JAMII NA HATA NGUVU KAZI YA  TAIFA.

PIA ANATOA SHUKRANI KWA VYOMBO VYA HABARI VYA NDANI NA NJE YA MKOA WA MBEYA KWA USHIRIKIANO WENU NA KUWATAKA KUENDELEA NA HALI HII KWANI IMELETA MAFANIKIO MAKUBWA KATIKA KUFIKISHA HABARI KWA WAKAZI WA MBEYA NA TAIFA KWA UJUMLA. AIDHA NATOA WITO KWA WAANDISHI WA HABARI KUFUATA NA KUZINGATIA MAADILI YA UANDISHI WA HABARI [MEDIA ETHICS] ILI KUTOPOTOSHA UMMA NA KUEPUKA MADHARA KATIKA JAMII NA TAIFA.


MWISHO KAMANDA MSANGI ANAWATAKIA KHERI YA MWAKA MPYA WA 2014 WANANCHI WOTE WAKAZI WA MKOA WA MBEYA.


Signed by:
[AHMED .Z. MSANGI - SACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.











No comments:

Post a Comment