TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI
“PRESS RELEASE”TAREHE 09.01. 2014.
WILAYA YA ILEJE – MAUAJI.
WATU wawili wakazi wa Kitongoji cha Lupungu,Kijiji cha Ikinga,Kata ya
Ikinga,Tarafa ya Bundali,Wilaya ya Ileje,mkoani Mbeya wanashikiliwa na Jeshi la
polisi kwa tuhuma za mauaji.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Kamishna msaidizi Mwandamizi wa polisi,Ahmed
Msangi amesema watuhumiwa hao Laison Mshani(55), na Queen Minga(40) walitenda
kosa hilo Januari,7,2014 baada ya
kumkata kwa mapanga kichwani na sehemu mbalimbali za mwili wake
Francis Mshani(30) kisha kumchoma moto kuanzia kwenye magoti hadi
kichwani.
Amefafanua kuwa marehemu alitoka
kifungoni gerezani mwezi Novemba,2013 kwa kosa la kumjeruhi
mtalaka wake na kwamba chanzo cha mauaji
hayo bado hakijafahamika.
Hata hivyo Kamanda ameendelea kutoa wito
kwa jamii kuacha tabia ya
kujichukulia sheria mkononi kwani madhara yake ni makubwa na badala yake watumie njia za busara katika
kutatua migogoro ya kifamilia na kijamii kwa ujumla.
Wakati huo huo,Mtu mmoja
aliyefahamika kwa jina la Dastan Gama(38),Mfanyabiashara Mkazi wa
Songea,mkoani Ruvuma anashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa kosa la kukutwa na
vipodozi vilivyopigwa marufuku na
serikali.
Kamanda msangi amesema mtuhumiwa alikamatwa
Januari,8,2014 majira ya saa 10.30 mchana
huko maeneo ya Ifisi,Kata ya Utengule,Tarafa ya usongwe,Wilaya ya Mbeya
vijijini ambapo askari polisi wakiwa
katika doria walifanikiwa kumkata
Dastan akiwa na Sabuni
boksi mbili,Carolight ndogo dazani nne,Epictem 10,Extra Crela dazani
mbili,Diplozoni dazani 17,Movey dazani nne,soft touch dazani nne na Lemovet
boksi tatu.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment