Translate

Friday, November 30, 2012

Jimbo Katoliki Mbeya linajiandaa kuadhimisha Sinodi ya Jimbo kwa kujikita katika Utume wa Familia

Na Thompson Mpanji,Mbeya


Askofu Evaristo Chengula wa Jimbo Katoliki Mbeya, Tanzania anatarajiwa kufungua Maadhimisho ya Sinodi ya Jimbo Katoliki Mbeya, Januari, 2013 kwa kupania kujikita zaidi katika Utume wa Familia. Waamini wataweza kupata nafasi ya kutembeleana nyumba hadi nyumba ili kuimarisha Utume wa Familia, ambayo kwa sasa inakabiliwa na changamoto mbali mbali kutoka ndani na nje ya familia yenyewe.

Askofu Chengula anabainisha kwamba, Sinodi ya Jimbo Katoliki Mbeya, itakuwa ni fursa ya kufanya tafakari ya kina kuhusu maisha na utume wake mintarafu mchakato wa Uinjilishaji Mpya, changamoto iliyotolewa na Mababa wa Sinodi ya Maaskofu juu ya Uinjilishaji Mpya, iliyohitimishwa hivi karibuni mjini Vatican. Katika maadhimisho hayo, Jimbo Katoliki Mbeya, litazindua pia Mkakati wa shughuli za kichungaji, ambao utakuwa dira na mwongozo wa Jimbo Katoliki Mbeya kwa miaka kadhaa ijayo.

Kanisa linapenda kuimarisha imani miongoni mwa waamini kwa kujikita zaidi katika masuala ya Maandiko Matakatifu, Katekesimu Mpya ya Kanisa Katoliki, Mafundisho Jamii ya Kanisa pamoja na kuendelea kutafakari kuhusu utajiri mkubwa unaofumbatwa katika Nyaraka za Mtaguso Mkuu wa Pili wa Vatican; changamoto kwa waamini kuchuchumilia utakatifu wa maisha, sanjari na kuendeleza jitihada za Mama Kanisa katika kuyatakatifuza malimwengu kwa njia ya ushuhuda wa maisha yao amini.

Maadhimisho ya Sinodi ya Jimbo Katoliki Mbeya, itakuwa ni fursa kwa Kanisa Jimboni Mbeya, kufanya tathmini ya kina kuhusu: majadiliano ya kidini na kiekumene, ikizingatiwa kwamba, Mbeya ni kati ya mikoa ambayo ina idadi kubwa ya madhehebu mbali mbali ya Kikristo, pengine, kuliko sehemu nyingine yoyote ya Tanzania. Ni muda wa kukazia majadiliano ya kidini na waamini wa dini ya Kiislam, ili kujenga na kuimarisha misingi ya: haki, amani, upendo na mshikamano wa kitaifa; daima wajikitahidi kutafuta mafao ya wengi.

Uchumi na maendeleo ya Kijamii ni mada itakayochambuliwa mintarafu Mafundisho Jamii ya Kanisa, ikizingatiwa kwamba, leo hii kuna idadi kubwa ya watu wanaoendelea kutumbukia katika baa la umaskini, ujinga na njaa na kwamba, hali inazidi kuwa mbaya hata kuliko ilivyokuwa miaka kadhaa iliyopita! Hapa kuna haja ya sera na mikakati ya maendeleo kutoa kipaumbele cha kwanza kwa utu na heshima ya binadamu, aliyeumbwa kwa sura na mfano wa Mungu.

Baada ya Maadhimisho ya Sinodi ya Jimbo Katoliki Mbeya, Askofu Evaristo Chengula anatarajiwa kutoa Waraka mara baada ya Sinodi, utakaokuwa ni dira na mwongozo wa Kanisa Katoliki Mbeya katika mikakati yake ya shughuli za kichungaji na kitume! Ni mwaliko kwa Familia ya Mungu Jimbo Katoliki Mbeya kushikamana na kutembea kwa pamoja, ili waweze kwa pamoja kutolea ushuhuda wa imani yao kwa Kristo na Kanisa lake.



Monday, November 26, 2012

mwanamke anayetuhumiwa kumtesa hadi kukatwa mkono mtoto Aneth kizimbani

Na Thompson Mpanji,Mbeya
 
MWANAMKE anayetuhumiwa kumtesa kumlisha kinyesi na kumchoma moto  mtoto wa kaka  yake  kumfungia ndani,  amepandishwa    kizimbani kwa mara ya pili    katika mahakama ya Wilaya ya Mbeya kujibu shtaka linalomkabili.
 
 
Mwendesha mashtaka wa Serikali, Achiles Mulisa ameileza  Mahakama kuwa Mtuhumiwa Wilvina Mkandala (24) Mkazi wa Majengo jijini humo  alitenda kosa la kusababisha majeraha akiwa na nia ovu ambayo imemsababishia ulemavu mtoto  Aneth Gasto (4).
 
 
Mulisa akisoma mashtaka hayo mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi wa mahakama hiyo Gilbert Ndeuruo amesema kosa hilo ni kinyume cha kanuni ya adhabu kifungu  cha 222(a) sura ya 16 kama ilivyorejewa mwaka 2002.
 
 Kutokana na hali hiyo mwendasha mashitaka huyo ameileza mahakama kuwa kesi inayo mkabili mwanamke huyo ilihitaji mashahidi sita   ambao ni Dactari aliye mfanyia upasuaji mtoto huyo   mwenyekiti wa Mtaa na barozi wake pamoja na Askari mpelelezi wa kesi hiyo na mtoto mwenye .
 
 
Amesema teyari mashahidi wanne kati ya sita wamekwisha toa ushahidi wao mahakani hapo .
 
 
Kutokana na kosa hilo mshtakiwa amekana shitaka hilo ambapo alirudishwa mahabusu hadi Novemba 27 Mwaka huu kesi hiyo itakapotajwa tena.
 
 
Amesema upande wa Jamhuri unamashahidi wanne ambao watatu kati yao teyari wamekwsha toa ushahidi wao katika mahakama hiyo .
 
 
Amewataja mashahidi hao kuwa ni Mwenyekiti wa Mtaa wa Majengo Shuku Mwakanyamale, Daktari anayemtibu mhanga katika Hospitali ya Rufaa ya Mbeya Dr. Paul Kasubi  na Habiba Mwakanyamale.
 
 
Wengine ni Askari Polisi aliyepeleza kesi hiyo WP Pudensia na Mtoto mwenyewe  ambao wako tayari kufika mahakamani na kutoa ushahidi wao mbele ya mahakama.
 
 
Awali mshatakiwa huyo aliieleza mahakama kuwa na uhusiano na mtoto  huyo ambapo pia alikiri kuwa na taarifa za kile kinachoendelea juu ya matibabu ya mtoto huyo na kuhusu kukatwa kwa mkono wake wa kushoto na kufungwa bandeji ngumu(POP) kwenye mkono uliobaki.
 
 
 

TAMISEMI yawataka tanesco na mamlaka nyingine zisikwamishe ujenzi wa miradi ya Worl Bank

Na Thompson Mpanji,Mbeya

OFISI ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa  na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) imewaagiza  Mameneja wa mikoa wa tanesco,mamlaka za maji na simu kuhakikisha wanatoa ushirikiano katika kuhakikisha  miradi iliyofadhiriwa na Benki ya dunia haihujumiwi.

Aidha imesema uchgelewaji wa  miradi hiyo ambayo imetolewa fedha  na benki ya dunia zaidi ya Sh.Bil.28 katika Halamshauri saba na CDA imekuwa ikichelewa kukamilika hasa katika baadhi ya mikoa ya Dodoma,Arusha kutokana na  baadhi ya wakuu wa taasisi mbali mbali zinazohusika na miundo mbinu  kuchelewa kuondoa miundo mbinu yao kwa madai ya gharama kubwa za kuhamisha.

Rai hiyo ilitolewa  na Kaimu katibu mkuu  ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa  na Serikali za Mitaa (TAMISEMI),Jumanne Sagin wakati akifungua  mkutano wa wakurugenzi wa Halmashauri saba Nchini na  Mamlaka  ya ustawishaji Dodoma (CDA)  ambako ipo miradi hiyo (Nov,19)jana Jijini Mbeya  katika ukumbi wa Mkapa.

Sagin alisema kuwa   katika kipindi cha  miezi 15 tangu kuanza  utekelezaji wa awamu ya miradi hiyo kumekuwepo na mafanikio   makubwa katika  miradi hiyo ambayo ni pamoja na miundo mbinu ya barabara,masoko,vituo vya mabasi,madampo,utunzaji na uhifadhi wa mazingira na kwamba baadhi ya miradi ilikwamba  kutokana na ukiritimba wa baadhi ya wakuu wa taasisi.

Bw.Sagin Alisema kuwa kutokana na hali hiyo amepanga kuonana na makatibu wakuu wa wizara zinazosimamia taasisi hizo ikiwa ni pamoja na wizara ya  Nishati na Madini na Maji  kwa ajili ya kuhakikisha mameneja  wa Tanesco wa Mikoa wanakuwa na uelewa  kuhusiana na umuhimu wa kukamilika kwa  miradi hiyo.

Alisema kuwa wakuu wa  Taasisi hizo wanapaswa kujua kuwa  kukamilika kwa miradi hiyo ni ukombozi wa watanzania  na ukuaji wa  uchumi  kutokana na ukweli kuwa   kuwapo kwa  miundo mbinu hiyo kunalenga  kuondoa umaskini  miongoni mwa watanzania na kutekeleza adhama ya maisha bora kwa kila mtanzania .

Alisema kuwa  warsha hiyo ya siku mbili inalenga  kuwakumbusha wakuu wa Halmashauri na wadau wengi walioalikwa  kuona  umuhimu wa kuhakikisha wanasimamia na kutoa ushirikiano kuhakikisha  miradi hiyo inakamilika  kwa wakati uliopangwa  na kuachana na tabia ya sasa ya kila mtu  kutaka kulipwa kwa ajili ya kuhamisha miundo mbinu yake  zikiwemo nguzo.

Kaimu katibu mkuu  huyo alisema kuwa  miradi hiyo inalenga kubadili maisha ya watanzania kwa ajili ya kuhakikisha wanatumia  miundo  mbinu hiyo katika kuachana na umaskini mkubwa walio nao na kuwa na hali bora kutokana na miundo mbinu hiyo  kwa kusimamiwa na kutunzwa vema.

Aidha aliwataka wakurugenzi  wa Halmashauri hizo kutunza na kuendeleza  miradi hiyo  ili iweze kuwa  endelevu na bora na hivyo kuwasaidia watanzania  wengi kwa muda mrefu tofauti na  ilivyo sasa  ambapo  miradi mingi imekuwa  ikihujumiwa .

Mwisho

Tanzania itakombolewa na wanahabri

Na Thompson Mpanji,Mbeya.

IMEELEZWA kuwa Tanzania itakombolewa  endapo wanahabari wataisoma historia tangu uhuru,kuchambua na kufuatiliaji  utekelezaji wa sera sanjari na kutoa taarifa sahihi na kamili  kupitia vyombo vya habari.

Hayo yamesemwa na mwezeshaji wa mafunzo ya uchambuzi wa sera na mchanganuo wa bajeti,Robert Renatus wakati akitoa mada katika mafunzo yanayoendelea kwa wanahabari katika ukumbi wa Ukaguzi jijini Mbeya.

Alisema  wanahabari ndiyo watu pekee watakaoweza kuikomboa nchi kutokana na hali ngumu ya maisha kwa watanzania  kupitia kuzichambua sera mbalimbali na kuziandikia habari za kina ikiwemo na makala juu ya utekelezaji wake.

Mwezeshaji huyo  alitolea mfano Nchi za Ulaya na  magharibi  wamefanikiwa katika uchumi  wa mtu mmoja mmoja na taifa kwa ujumla na hatimaye kufikia maendeleo makubwa kutokana na kutumia mfumo wa SWOT Analysis kwa kuangalia uwezo,udhaifu,fursa na vitisho.

Alisema vyombo vya habari vinapaswa kutumia nafasi yake kukosoa utekelezaji mbovu wa sera  ili sekta husika ziweze kubadilika,kujisahihisha,kuwa makini na kufanya usimamizi mzuri  na hatimaye kufikia lengo lililokusudiwa la kumsaidia mtanzania.

Hata hivyo wakipitia muhtasari wa mada ya sera washiriki wa mafunzo hayo walisema wamepata ufahamu mkubwa na kubaini kuwa sera  zinatungwa ngazi za juu bila kushirikishwa wananchi na hivyo kushindwa kutekelezeka,.

Aidha katika mafunzo hayo imebainika kuwa baadhi ya wanahabari wamekuwa wakilipua katika kufanya kazi zao kwani  hawazami kwa undani katika uandishi kutokana na kutojuwa sera ikiwemo umuhimu wa vyombo vya habari katika kufuatilia na kutathmini utekelezaji wa sera.

Mwisho.

JWTZ 10 mbaroni kwa kuuwa na kujeruhi Mbeya

Na Thompson Mpanji,Mbeya

ASKARI 10 wa Jeshi la wananchi (JWTZ) kikosi cha 44kj Mbalizi,wanashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa tuhuma za  mauaji  na kujeruhi watu wengine sita sanjari na kuharibu mali mbalimbali.

Kamanda wa polisi Mkoa wa Mbeya,Diwani Athumani amethibitisha kutokea kwa kifo hicho  Nov,18 majira ya saa 5 usiku  katika hospitali teule ya Ifisi wilaya ya mbeya vijijini mkoa wa mbeya na amemtaja marehemu kuwa ni Petro Sanga,( 25),mkulima,mkinga, mkazi wa chapakazi, mbalizi ambaye  alifariki dunia wakati akiendelea kupatiwa matibabu hospitalini hapo.

Athuman amesema  marehemu alichomwa kisu shingoni na mdomoni na kikundi cha watu  wanaosadikiwa kuwa askari wa jeshi la wananchi wa Tanzania, tarehe  hiyo majira ya saa 3 usiku akiwa katika grocery  iitwayo vavene mwe   iliyopo mbalizi mara baada ya  watu hao kuvamia bar iitwayo power night club ambamo awali alikuwepo pia marehemu.

Amesema watu wengine sita  walijeruhiwa kwa kupigwa sehemu mbalimbali za miili yao  na wanaodaiwa kuwa askari wa JWTZ na kupatiwa hati ya matibabu [pf3] kwa matibabu kati yao watatu walilazwa katika hospitali teule ya ifisi kwa matibabu zaidi na  majeruhi wengine watatu walipatiwa matibabu na kuruhusiwa.

Kamanda huyo amesema  kufuatia vurugu hizo baadhi ya mali za watu ziliharibiwa ambazo ni pamoja gari T.106 AWB aina ya toyota vista mali ya Paulo Maximilian ilivunjwa kioo cha mbele,gari T.884 AUU Toyota Cresta mali ya Alile Godfrey lilivunjwa side mirror upande wa kulia.  

Kamanda huyo amesema kuwa  wahalifu hao walianza kuwashambulia wananchi kwa kuwapiga wakitumia ngumi, mateke, mikanda, marungu, sime na mapanga na kwamba  marehemu  alijaribu kuokoa uhai wake kwa kukimbia toka eneo hilo hadi   katika grosary hiyo lakini watu hao walimkimbiza hadi eneo hilo na kumjeruhi vibaya kwa kumchoma kisu.

Amesema chanzo cha tukio hilo ni kulipiza kisasi kufuatia askari Godfrey Matete( 30),mjita, wa kikosi cha 44kj mbalizi kupigwa na walinzi wa kilabu cha pombe za kienyeji kiitwacho DDC kilichopo mbalizi  waliokuwa lindoni Nov,17,2012 majira ya saa 01:30.

Amefafanua kuwa  baada ya kushambuliwa  askari huyo alifungua kesi kituo cha polisi mbalizi usiku huo  kosa la kujeruhi na alipatiwa hati ya matibabu [pf3] kwa ajili ya kwenda kupata matibabu hospitalini ambapo walinzi wanne walikamatwa  kuhusiana na tukio hilo  kwa mahojiano.

Amewataja walinzi hao kuwa ni Frenk Mtasimwa (25),Mure Julias (26),Omari Charles (28) wote wakazi wa DDC mbalizi na  Legnard Mwampete (30),mkazi wa Izumbwe na kwamba  upelelezi wa kesi hiyo bado unaendelea.

Mwisho.

kuhusu sakata la Mbegu feki Mbozi,wakulima wapewa somo na mtafiti


Na Thompson Mpanji,Mbeya
 
WAKULIMA nchini wameshauriwa kujenga utamaduni wa kudai lisiti wakati wa kununua mbegu za mazao ya aina mbalimbali katika maduka ya pembejeo yanayotambulika ili kuepuka kuuziwa mbegu feki ambazo zimetapakaa na kuwaletea hasara kubwa wakulima walio wengi sanjari na kuhatarisha maisha ya walaji.
 
Aidha imeleezwa kuwa mbegu za mahindi ya njano ambazo zinadaiwa kutoa unga wa njano baada ya kusagwa zinazodaiwa kusambazwa kwa wakulima walio wengi wilayani Mbozi zinatumika kwa ajili ya malisho ya mifugo na siyo kwa binadamu.
 
Akizungumza na gazeti hili Mtafiti wa zao la mahindi kutoka taasisi ya utafiti kanda ya nyanda za juu kusini (ARI Uyole), Anderson Elibariki Temu alisema mbegu za mahindi zenye rangi ya njano ni mojawapo ya aina inayopendelewa sana nchini Marekani na imekuwa ikitumika kwa ajili ya vyakula vya kuku na ng’ombe wa maziwa.
 
Mtafiti huyo alisema ingwa hajabahatika kuyaona mahindi hayo yanayozungumziwa lakini kutokana na maelezo aliyoyapata ana uenda yalizalishwa kwa ajili ya mifugo na siyo kwa ajili ya chakula cha binadamu.
 
"Lakini nawashauri wakulima kwa kuona tatizo hilo na mbegu hazijifichi inatakiwa wakulima wawe makini wawe waangalifu wakati wa kununua mbegu kwa sababu hii imekuwa ni kero kubwa kwa wakulima wa kanda ya nyanda za juu kusini na Tanzanja kwa ujumla Mkulima anapojitahidi kuwa na mtaji hadi kununua mbegu, anaipanda,gharama za mbolea ,maandalizi ya shamba na gharama nyingine alafu mwisho anaikuta mbegu aliyoipanda kwa mfano siyo Uyole Hybrid 615 ni hasara kubwa,"alisema.
 
Temu alisema ili mkulima aweze kukwepa udanganyifu huo anapaswa anapoenda kununua mbegu ahakikishe mbegu ipo kwenye mifuko ya kampuni halisia inayozalisha hiyo mbegu mfano kampuni inayozalisha mbegu za uyole ya Highland seed growers ambapo nje ya mfuko kuna anuani na jina la kampuni,na kwamba akwepe kununua mbegu zinazouzwa baada ya kufunguliwa katika mfuko .
 
Alisema Mkulima naweza kununua mbegu iliyokuwepo katika mifuko kwa sababu wanaweza kuiba mifuko ama kutumia ujanja wowote,kwa hiyo njia ya mwisho ya kuwabana wauzaji wa mbegu feki ni kudai lisiti na kuitunza hadi wakati wa msimu wa amvuno.
 
"ili tatizo likijitokeza la mbegu kutokuwa halisi nenda kwa ofisa shamba ukikutana na tatizo atakuelekeza ngazi na utaratibu wa kufuata ili mhusika weze kufuatiliwa na ikibidi sheria ichukuwe mkondo wake kwa sababu sheria zipo kuanzia kuzalisha mbegu kuhakikisha zina ubora na mamlaka husika zinazofuatilia zipo,hakikisha una lisiti hadi mwisho wa msimu,"alisisistiza Mtafiti huo.
 
Mwisho.

Wednesday, November 14, 2012

Askofu Chengulaamwalika waziri mulugo kuchangisha zaidi ya Sh.mil.100 ujenzi wa kijiji cha watoto yatima cha Kambarage Mbeya

Na Thompson Mpanji,Mbeya
 
MLEZI Mkuu wa Chama cha vijana,wanawake wa kikristo Tanzania(YWCA),Tawi la Mbeya,Askofu Evaristo Chengula wa kanisa Katoliki Jimbo la Mbeya ametoa wito kwa watanzania wote wenye mapenzi mema bila kujali itikadi za kisiasa,dini,kabila wala rangi kuchangia Kijiji cha watoto yatima wanaoishi katika mazingira hatarishi na wenye mtindio wa ubongo cha Kambarage  ili kuweza kukamilisha ujenzi huo.
 
Askofu Chengula ambaye ndiye msimamizi mkuu wa YWCA amemualika Naibu  Waziri wa elimu na mafunzo ya ufundi,Philipo Mulugo (MP)  kuendesha harambee ya ujenzi wa Kijiji cha watoto yatima cha Kambarage novemba, 24 mwaka huu.
 
Naibu waziri Mulugo anatarajia kuwa mgeni rasmi katika changizo hilo litakaloambatana na  maandhimisho ya miaka 20 ya YWCA,Tawi la Mbeya hafla inayotarajia kufanyika katika ukumbi wa Mkapa,jijini Mbeya.
 
Askofu Chengula ataungana na walezi na wasimamizi wenzake wa chama hicho ambao ni Askofu wa kanisa la Anglikana,nyanda za juu kusini, John Mwela,Askofu wa kanisa la Moravian jimbo la kusini magharaibi,Alinikisa Cheyo,Askofu wa Jimbo la Moravian jimbo la kusini, Lusekelo Mwakafwila na Askofu wa KKKT Dayosisi ya Konde,Dkt.Islael Mwakyolile.
 
Akizungumza kwa niaba ya Askofu Chengula,Katibu wa YWCA Tawi la Mbeya,Bi.Tabitha Bughali alisema   watarajia mgeni rasmi,Naibu Waziri Mulugo atafanikisha kuchangisha Sh.Mil.100 ili kuendeleza ujenzi huo kwa awamu ulioanza tangu mwaka 2009 ambapo zaidi ya sh.Bil.2 zinahitajika kukamilisha ujenzi huo.
 
Katibu huyo alisema awali Mwenyekiti wa IPP Media, Reginald Mengi  alichangia  zaidi ya Sh.Mil.25 kusaidia ujenzi huo na baadhi ya wadau wengine waliochangia ni pamoja na mmiliki wa shule za Clementine foundation Marry Camm ambaye anatarajiwa kuwasili katika shughuli hizo,Prof.Mwansoko,Mbunge wa viti maalum Mh.Hilda Ngoye,Prof.Mark Mwandosya na wadau wengi.
 
Amewataja wageni watakaohudhuria katika changizo hilo ni Mkuu wa Mkoa wa Mbeya,Abbas Kandoro,Wakuu wa Wilaya zote za Mkoa wa Mbeya,wabunge,wakurugenzi wa halmashauri,wakurugenzi wa mahoteli ambapo baadhi ya wadau tayari wameshaanza kutoa michango yao kama Wakili Mbise,,Makasini Hotel,Mwenyekiti wa umoja wa wamiliki wa hoteli Mahenge,Penge Hoteli,Wakili Mshokolwa na wakili Msigwa.
 
Bi.Bughali alisema shughuli hiyo itaendeshwa na kamati ya maandalizi inayoongozwa na Jaji Upendo Msuya ambaye ndiye Mwenyekiti wa kamati ya hiyo na kwamba wafanyabiashara,taasisi za serikali na binafsi na watu mbalimbali wenye mapenzi mema wanatarajia kushiriki katika harambee hiyo na ametoa wito kwa watanzania wote kujitokeza kuiunga mkono YWCA katika harakati za kuwasaidia watoto yatima.
 
Mwisho.

Tuesday, November 13, 2012

Wajasiliamali Mbeya wasema bidhaa za nje zinawatesa

Na Thompson Mpanji,Mbeya




BAADHI ya wajasiliamali wametoa wito kwa serikali kuwawezesha mitaji,mazingira ya kufanyia kazi sanjari na kuwaweka katika vikundi ili waweze kumudu na kuingia katika ushindani wa soko la ndani na nje kuliko ilivyo sasa ambapo bidhaa za nje zinawatesa katika soko la ndani kutokana na kuzalishwa kwa muda mfupi kwa wingi na kuuza bei ya chini.



Wakizungumza wakati wa maonesho ya wajasiliamali kutoka mikoa mbalimbali ya Tanzania na baadhi ya nchi za afrika mashariki,walisema kuwa kutokana na changamoto hiyo serikali haina budi kutumbukiza mkono wake kuwasaidia kwa hali na mali ili waweze kuendelea kujiajiri,kuwauzia watanzania wa chini,kati na juu bidhaa imara kwa bei nafuu sanjari na kupata tija na hatimaye kujiinua kiuchumi.



Mkurugenzi wa Witega Works and Fubrication iliyopo jijini Mbeya,William Gamba alisema kampuni yake inajishughulisha na utengenezaji wa zana za kilimo mathalani majembe ya kukokota kwa ng'ombe (plau) na majiko banifu lakini wamekuwa wakikumbana na ushindani mkubwa kutoka kwa wafanyabiashara kutoka nje kutokana na kuwa na mitaji midogo na vitendea kazi vya kukodi.



Alisema endapo serikali itamwezesha anao uwezo wa kutengeneza majembe ya kukokota kwa ng'ombe zaidi ya 200 kwa mwaka ambayo atawauzia wakulima kwa bei nafuu na hivyo kufikia adhama ya kauli mbiu ya taifa ya kilimo kwanza kwa vitendo na hivyo kuwakomboa wakulima hasa wa vijijini na wote wakafanikiwa kujiinua kiuchumia na kuongeza uzalishaji wa zana za kilimo na mazao.



Gamba alisema kutokana na utaalamu alioupata kutoka katika kiwanda cha utengenezaji wa zana za kilimo(ZZK) cha jijini Mbeya kilichokufa katika miaka ya 70 anao uwezo wa kutengeneza majembe ya mkono,koleo na fyekeo lakini mtaji mdogo ndiyo kikwazo.



Hata hivyo ameiomba serikali kuwaangalia kwa macho mawili waandaaji wa maonyesho mbalimbali ya wajasiliamali kwani ni kazi ngumu kuwakusanya pamoja hadi kufanikisha zoezi hilo linalohitaji wadhamani wa kutosha na fedha za kuendeshea shughuli hiyo.



Naye Mhasibu wa kampuni hiyo ambaye pia ni Mke wa Mkurugenzi huyo,Odilia Gamba ametoa wito kwa wanawake kuwasaidia waume zao katika shughuli mbalimbali za ujasiliamali ili kuinua kipato cha familia na kuendeleza miradi mbalimbali waliyoianzisha.



Maonyesho hayo ni ya tatu kuaandaliwa na Kampuni ya Mbeya Trade Fair and Enterteinment yalifunguliwa na Mkuu wa mkoa wa Mbeya,Abbas kandoro na kuwakilishwa na Mkuu wa wilaya ya Mbeya,Dkt.Norman Sigalla ambapo wageni wengine waliohudhuria maonyesho hayo ni Mkuu wa wilaya ya Ileje na kufungwa na Kamanda wa polisi Mkoa wa Mbeya,Diwani Athuman.



Katika maonyesho hayo wakazi mbalimbali kutoka ndani na nje ya Mkoa wa Mbeya walijitokeza kwa wingi kujionea na kununua bidhaa mbalimbali vikiwemo vyakula na vinywaji vya asili,nguo za asili,tiba asili,zana za kilimo na majiko banifu yanayosaidia kwa kiasi kikubwa utunzaji na uhifadhi wa mazingira.



Mwisho.

Wednesday, November 7, 2012

Polisi Mbeya wafanikiwa kuzima jaribio la kuteka malori ya mafuta yanayosafirisha kwenda nchi jirani kupitia Mbeya,wahusika wapanga mawe barabara ya Mbeya/Tunduma maeneo ya mama john wakiwa na vidumu vitupu vya mafuta,wadai haiwezekani kukosa mafuta ilhali mafuta yanapita machoni pao,wang'ang'ania makufuli ya matenki ya mafuta

Na Thompson Mpanji,Mbeya
 
JESHI la polisi limefanikiwa kuzima jaribio la baadhi ya madereva wa boda boda na daladala kuzuia magari yanayobeba mafuta kusafirisha kwenda nchi za jirani za Zambia baada ya kuamua kuweka kizuizi cha mawe katika barabara ya Mbeya/ Tunduma,katika maeneo ya mama John kwa madai ya kukerwa na adha ya mafuta huku wakiyaona  yakipita kuelekea nchi jirani.
 
Sakata hilo limedumu kwa takribani masaa mawili tangu saa 1 asubuhi hadi saa 3 asubuhi baada ya madereva wa daladala na waendesha boda boda kudaiwa kupandwa na jazba ya kukosa mafuta katika kituo cha Orxy Mama John na hivyo kuamua kupanga mawe barabarani jambo ambalo inadaiwa endapo Polisi wasingejitokeza haraka hali ingekuwa tete kutokana na baadhi yao kuonekana waking'ang'ania makufuli ya malori ya mafuta waliyofanikiwa kuyazuia na kuwateremsha madereva kwa nguvu.
 
"Ninakwambia kulikuwa na hatari kubwa kama wasingetokea wale FFU kwa sababu wengine walitaka kuyapiga kiberiti malori hayo ya mafuta baada ya kuwalazimisha madereva wa magari hayo kufungua nao wakagoma na huku madereva wa malori ya mafuta nao walikuwa wamechukia kwa hiyo tungekuwa tunazungumza kitu kingine,na madereva wengine wa malori walivyopata taarifa kuwa hali siyo shwari waligeuza na kurudi Uyole kuegesha Uyole walivyopata lakini walipotokea maaskari walitawanyika,"alisema mmoja wa wafanyakazi wa kituo hicho cha mafuta ambaye hakutaka kutaja jina lake.
 
Alisema kuwa chanzo cha hasira ya watu hao hawakuamini kama mafuta waliyokuwa wakiyatoa ya petroli kama yamekwisha na kubakiwa na mafuta ya dizeli na hivyo kuanza kupiga kelele na kuhamishia hasira zao barabarani hadi Jeshi la polisi likiongozwa na Mkuu wa Polisi wa Wilaya ya Mbeya Sylivester Ibrahim kuwaaminisha kwa kumuomba mmiliki wa kituo hicho kupima na kuhakikisha kweli hakuna mafuta waliamua kuondoka.
 
Gazeti hili limeshuhudia majira ya saa 4 asubuhi baada ya hali ya utulivu kurejea malori ya mafuta yalionekana yakipita kasi katika maeneo ya mama John tofauti na siku nyingine ambapo taarifa kutoka kituo cha Mafuta cha Uyole yanapoegeshwa magari yanayoelekea Tukuyu kuwa mafuta yapo ila bei ya mafuta ya petroli kwa lita inadaiwa kufikia Sh.3,000.
 
Mmoja wa waendesha boda boda ambaye hakutaka kutaja jina lake alisema wamekerwa sana na kitendo cha kuhangahika na kukosa mafuta kwa takribani siku nne sasa huku magari ya mafuta yakiwa yanapitishwa machoni pao kwenda zambia na kwingineko jambo ambalo alidai bado linawasumbua katika vichwa vyao kuwa serikali inafurahi kero hii wanayoipata walala hoi wa chini huku familia zao zikiendelea kuteseka na njaa kwa kukosa kufanyakazi.
 
Suala hili la ukosefu wa mafuta bado linaonekana ni kitendawili kwa watanzania na kwamba endapo serikali haitalishughulikia na kulimaliza haraka iwezekanavyo kuna hatari ya malori yanayosafirisha mafuta kwenda nchi ya zambia kupitia Mbeya yakafanyiwa hujuma kutokana na kuwepo na tetesi kuwa hawajaridhika kukosa mafuta ilhali wanayaona yanapita mbele ya machjo yao.
 
Hata hivyo Mwandishi wa habari hizi ameshuhudia Mkuu wa Polisi wa Wilaya ya Mbeya,Sylivester,Mkuu wa upelelezi wa Wilaya,Ntatiro,ofisa habari wa Polisi na baadhi ya makachero wakiwa wamesimamia hali ya usalama katika zoezi la utoaji wa mafuta ya Petroli na mafuta ya taa katika kituo cha Total Mafiati huku kukiwa na foleni kubwa ya magari,waendesha boda boda,watu walioshika vidumu vya lita tatu na tano.
 
 
Mwisho.
 

Sunday, November 4, 2012

Vyombo vya habari vyanyooshewa kidole,ni kutokana na kutangaza vyuo feki,VETA yasema matangazo yasirushwe hadi wahakikishe wamethibitisha cheti kama kweli chuuo kina usajiri,ikibi wakaangalie na majengo,asema Grace College imesajiriwa rasmi na inajulikana kitaifa

Na Thompson Mpanji,Mbeya




VYOMBO vya habari nchini vimetakiwa kuhoji uhalali wa vyuo sanjari na kupata uthibitisho wa vyeti vya usajili kutoka Chuo cha ufundi stadi (VETA),kwa wahusika wanaohitaji kufanya matangazo ya biashara katika Radio,magazeti na Luninga ili kuwasaidia wazazi na wananfunzi wasiweze kupotea na kuingia hasara ya ada na gharama nyinginezo katika vyuo visivyosajiriwa.



Mkurugenzi wa VETA kanda ya nyanda za juu kusini,Justin Rutta ametoa wito huo wakati wa mahafali ya tisa ya wahitimu wa kozi za uhazili,utalii na masuala ya Hoteli na programu ya Kompyuta katika chuo cha kanisa la Neema cha Grace College kilichopo Forest Maghorofani,jijini Mbeya.



Rutta alisema vyombo vya habari kama jicho la jamii vinapaswa kuwasaidia wazazi na wanafunzi wanaohitaji kupata elimu bora inayotambulika kitaifa hasa katika wakati huu ambapo wajanja wengi wameibuka na kuanzisha vyuo visivyo na hadhi,visivyosajiliwa lakini kutokana na ujanja ujanja vimekuwa vikitumia gharama kubwa kujitangaza katika vyombo vya habari vikubwa vinavyotambulika kwa lengo la kuwalubuni wananchi.



"Media ndiyo mhimili unaotoa taswira kwa jamii kuhusu kipi kizuri na kipi kibaya kwa hiyo pamoja na kuhitaji matangazo nawaombeni msirushe matangazo ya vyuo hadi wawaonyeshe cheti cha usajili,kwa sababu vinginevyo media ndiyo itaonekana inashirikiana na mataperi kuipotosha jamii na waulizeni wanapotoka na ikibidi nendeni mkaangalie na majengo yao,"alisema.



Alifafanua kuwa hivi karibuni Veta ilivifunga vyuo vyote ambavyo havikuwa na vigezo vya kutoa elimu na kwamba katika mchakato wa sasa wa kupita kuvikagua na kuvipatia usajiri upya Chuo cha Grace College ni miongoni mwa vyuo vilivyosajiriwa na kutambulika kitaifafa baada ya Veta kukipitisha.



"Wazazi na vijana kuweni macho na vyuo vinavyoanzishwa kitaperi katika maghofu ya nyumba na voichochoro vya kutisha,na matokeo yake mzazi anagharamia ada na gharama nyingine lakini mtoto akihitimu cheti chake chenye mapambo mazuri hakitambuliki kitaifa,chuo hakijasajiriwa na hivyo inakuwa ni hasara kwa mzazi na mtoto anapoteza mwelekeo wake wa baadaye,"alisema Rutta.



Hata hivyo Mkurugenzi huyo aliwataka wahitimu hao kwenda kuwa kielelezo cha chuo cha Grace kuwa ni kisima cha elimu bora,wanafunzi wanaofuata maadili mema,uchapakazi,upendo,ubunifu sanjari na ushirikiano katika maeneo ya kazi watakayofanikiwa kuajiriwa huku akiwataka watakaokosa nafasi wasikate tamaa na badala yake waende kujiajiri na kuondokana na utegemezi.



Awali Mkuu wa chuo cha Grace College,Sinana Otaigo Daniel alisema licha ya chuo hicho kumilikiwa na kanisa la Neema lakini kinapokea wanafunzi wa imani zote,bila ubaguzi na kwamba wanatoa pia elimu ya stadi za maisha,malezi bora, sanjari na kozi ya lugha ya kiingereza na kifaransa, na maosmo ya sekondari kwa miaka miwili na ada zao ni nafuu huku wanafunzi wa kike wakikaa katika Hosteli iliyomo ndani ya uzio wa chuo.



Mkuu huyo alisema kutokana na uhataji wa mahali salama kwa malazi na patulivu kwa kusomea hasa kwa wananfunzi wa kike,mikakati imewekwa ya kuongeza majengo mengine kwa hosteli inayotarajia kulaza wanafunzi zaidi ya 70 huku jitihada nyingine za kujenga mabweni ya wanafunzi wa kiume zikiendelea kwa kushirikiana na wazazi,kanisa na wafadhiri mbalimbali.



Ametoa wito kwa wazazi,wadau wa elimu,wafadhiri na watanzania wote wenye mapenzi mema kujitokeza kukichangia chuo hicho ili kiweze kujenga mabweni ya kutosha na hivyo wanafunzi kuweza kusoma kwa usalama bila bughudha za kidunia na hatimaye kupata viongozi bora wa baadaye na wataalamu wa taifa.



Mwisho.

Friday, November 2, 2012

Abood lauwa Kondakta na kujeruhi 25,ni baada ya kufika Mbeya,ni la Dar Tunduma,mochwari wachanganya maiti

Na Thompson Mpanji,Mbeya

MTU mmoja amefariki dunia na wengine 25 kujeruhiwa baada ya Basi la abiria la kampuni ya Abood lililokuwa likitokea Dar es salaam kuelekea Tunduma, kugongana na lori la mizigo lililokuwa likielelekea Dar es salaama katika maeneo ya Sae kwa Mbilinyi jijini Mbeya.
 
Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo linalodaiwa kutokea jana majira kati yasaa moja na mbili usiku walimtaja  kwa jina moja mtu  aliyefariki dunia papo hapo  kuwa ni mmoja wa makondakta wa basi aliyefahamika kwa jina la  white na wengine kujeruhiwa vibaya baada ya lori  lenye konteiner lenye  nambari za usajili T.616 ATQ kutaka kuikwepa basi dogo la abiria maarufu daladala iliyogeuza ghafla  maarufu kusinga katika eneo la Mbilinyi,Sae na kujikuta likivaana na  Basi lenye nambari za usajili T545 AZE lililokuwa likielekea Tunduma.
 
Mashuhuda hao walisema  baada ya dereva wa lori kulikwepa daladala na   alikutana na  basi la Abood  na hivyo  kufanya jitihada za kulikwepa na kujikuta basi hilo likiingia katika  upande wa konteiner la lori.
 
Kamanda wa polisi Diwani Athuman amethibitisha kutokea kwa ajili hiyo na kwamba uchunguzi unaendelea kujuwa chanzo cha ajali.
 
Muuguzi mkuu wa Hospitali ya Rufaa Mbeya,Thomas  akizungumza kwa njia ya simu alisema walipokea wagonjwa 25 ambapo hadi kufikia leo asubuhi wamebakia na wagonjwa wanne na kwamba  taarifa ya jana jioni inaonesha walipokea maiti mbili lakini inakinzana na  taarifa ya chumba cha kuhifadhia maiti ambayo inaonesha wamepokea maiti moja iliyotokana na ajali ambapo marehemu alitambulika kwa jina la Charles almaarufu white,kabila mpale mkazi wa Kilimanjaro na tayari imechukuliwa na ndugu zake na kusafirishwa.
 
Mwisho.

wananchi Mbeya wafunga barabara kwa masaa sita ,ni kutokana na kugongwa watu zaidi ya 30 wakiwemo watoto wawili wa chekechea


Na Thompson Mpanji,Mbeya

MATUKIO ya ajali yameendelea kuundama Mkoa wa Mbeya  baada ya wananchi  wa Kijiji cha Imezu  kata ya Inyala  wilaya ya Mbeya Vijijini  leo kulazimika kufunga bara bara ya  Mbeya  Dar es Salaam kwa takribani saa sita baada ya kutokea ajali iliyoua watoto  wawili wa chekechea  wanaokadiriwa kuwa na umri wa miaka mitano mpaka sita.

Kamanda wa kikosi cha usalama barabarani  Mkoa wa Mbeya (RTO) Butusyo Mwambelo amewataja Watoto hao kuwa ni ,Timotheo  Omary (5) na Thadeo Braiston  Malila (5)  ambapo kati ya watoto hao mmoja tayari mazishi yake yamefanyika  na mwili wa mtoto mwingine utasafilishwa  kwenda kijiji cha uwanji Matamba Wilayani Makete.

Amesema kuwa tukio hilo  limetokea  majira ya saa 1.15 asubuhi baada ya watoto hao kugongwa na gari aina ya  yenye namba  za usajili T 798 BVY  tela  T698  BVA lilokuwa kiendeshwa na  Dominick  Mwakalundwa (34) mabibo dar e s salaam lililokuwa likitokea Mbeya  kwenda Mkoani Iringa liligonga watoto  hao waliokuwa pembeni ya bara bara wakitoka shule na kwamba aliokolewa na askari Polisi baada ya wananchi kutaka kumshambulia..

Wakizungumza na  Radio five na matukio  katika eneo la ajali hiyo Wananchi hao,  wamesema kuwa waliamua kuchukua  uamuzi huo  baada ya kuchoshwa na ahadi za serikali kupitia wakala wa bara bara  za kuweka matuta  katika eneo hilo la la shule  ili kuepusha ajali ambazo zimekuwa zikitokea mara kwa mara .

Bw.Michael Mashamba mkazi wa kijiji cha Imezu amesema kuwa baada ta tukio hilo kutokea wananchi walijaa eneo la ajali  na kuanza kufunga  bara bara kwa kutumia magogo na mawe  ili kuzuia magari yasipite eneo hilo kwa lengo la kushinikiza serikali kuweka matuta ili kuzuia ajali kutokana na madai ya kufariki watu zaidi ya 30 kwa ajili katika maeneo hayo.

 Hata hivyo baada ya tukio hilo Mkuu wa Wilaya ya Mbeya Dkt. Norman  Sigalla  aliwaomba wananchi  kufungua bara bara wakati serikali  kwa kushirikiana na wakala wa bara bara (TAN ROADS) ikiwa inaweka utaratibu  wa kuweka matuta hayo haraka iwezekanavyo.

Aidha Sigalla ameliagiza jeshi la polisi  Mkoani hapa kuwachukulia hatua  kali madereva watakoendesha  magari kwa mwendo kasi  na kwamba watozwe faini na adhabu kali ambayo itawafanya wawe na nidhamu  na askari wasiwe marafiki wa madereva.
Mwisho