Na Thompson Mpanji,Mbeya
OFISI ya Waziri Mkuu
Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
(TAMISEMI) imewaagiza Mameneja wa mikoa wa tanesco,mamlaka za maji na
simu kuhakikisha wanatoa ushirikiano katika kuhakikisha miradi
iliyofadhiriwa na Benki ya dunia haihujumiwi.
Aidha
imesema uchgelewaji wa miradi hiyo ambayo imetolewa fedha na benki ya
dunia zaidi ya Sh.Bil.28 katika Halamshauri saba na CDA imekuwa
ikichelewa kukamilika hasa katika baadhi ya mikoa ya Dodoma,Arusha
kutokana na baadhi ya wakuu wa taasisi mbali mbali
zinazohusika na miundo mbinu kuchelewa kuondoa miundo mbinu yao kwa madai ya gharama kubwa za kuhamisha.
Rai hiyo ilitolewa na
Kaimu katibu mkuu ofisi ya Waziri Mkuu
Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
(TAMISEMI),Jumanne Sagin wakati akifungua
mkutano wa wakurugenzi wa Halmashauri saba Nchini na Mamlaka
ya ustawishaji Dodoma (CDA) ambako ipo miradi hiyo (Nov,19)jana Jijini Mbeya katika ukumbi wa Mkapa.
Sagin alisema kuwa katika
kipindi cha miezi 15 tangu kuanza utekelezaji wa awamu ya miradi hiyo
kumekuwepo na mafanikio makubwa katika miradi hiyo ambayo ni pamoja na miundo mbinu
ya barabara,masoko,vituo vya mabasi,madampo,utunzaji na uhifadhi wa mazingira na kwamba baadhi
ya miradi ilikwamba kutokana na ukiritimba wa baadhi ya wakuu wa
taasisi.
Bw.Sagin Alisema kuwa kutokana na hali hiyo amepanga kuonana
na makatibu wakuu wa wizara zinazosimamia taasisi hizo ikiwa ni pamoja na
wizara ya Nishati na Madini na Maji kwa ajili ya kuhakikisha mameneja wa Tanesco wa Mikoa wanakuwa na uelewa kuhusiana na umuhimu wa kukamilika kwa miradi hiyo.
Alisema kuwa wakuu wa
Taasisi hizo wanapaswa kujua kuwa
kukamilika kwa miradi hiyo ni ukombozi wa watanzania na ukuaji wa
uchumi kutokana na ukweli
kuwa kuwapo kwa miundo mbinu hiyo kunalenga kuondoa umaskini miongoni mwa watanzania na kutekeleza adhama ya maisha bora kwa kila mtanzania .
Alisema kuwa warsha
hiyo ya siku mbili inalenga kuwakumbusha
wakuu wa Halmashauri na wadau wengi walioalikwa
kuona umuhimu wa kuhakikisha wanasimamia na kutoa ushirikiano kuhakikisha
miradi hiyo inakamilika kwa wakati uliopangwa na kuachana na tabia ya sasa ya kila mtu kutaka kulipwa kwa ajili ya kuhamisha miundo
mbinu yake zikiwemo nguzo.
Kaimu katibu mkuu
huyo alisema kuwa miradi hiyo
inalenga kubadili maisha ya watanzania kwa ajili ya kuhakikisha wanatumia miundo
mbinu hiyo katika kuachana na umaskini mkubwa walio nao na kuwa na hali
bora kutokana na miundo mbinu hiyo kwa kusimamiwa na kutunzwa vema.
Aidha aliwataka wakurugenzi
wa Halmashauri hizo kutunza na kuendeleza miradi hiyo ili iweze kuwa
endelevu na bora na hivyo kuwasaidia watanzania wengi kwa muda mrefu tofauti na ilivyo sasa ambapo
miradi mingi imekuwa ikihujumiwa
.
Mwisho
No comments:
Post a Comment