Na Thompson Mpanji,Mbeya.
IMEELEZWA kuwa Tanzania
itakombolewa endapo wanahabari wataisoma
historia tangu uhuru,kuchambua na kufuatiliaji utekelezaji wa sera sanjari
na kutoa taarifa sahihi na kamili
kupitia vyombo vya habari.
Hayo yamesemwa na mwezeshaji
wa mafunzo ya uchambuzi wa sera na mchanganuo wa bajeti,Robert Renatus wakati
akitoa mada katika mafunzo yanayoendelea kwa wanahabari katika ukumbi wa
Ukaguzi jijini Mbeya.
Alisema wanahabari ndiyo watu pekee watakaoweza
kuikomboa nchi kutokana na hali ngumu ya maisha kwa watanzania kupitia kuzichambua sera mbalimbali na
kuziandikia habari za kina ikiwemo na makala juu ya utekelezaji wake.
Mwezeshaji huyo alitolea mfano Nchi za Ulaya na
magharibi wamefanikiwa katika uchumi wa
mtu mmoja mmoja na taifa kwa ujumla na hatimaye kufikia maendeleo
makubwa kutokana na kutumia mfumo wa SWOT Analysis kwa kuangalia
uwezo,udhaifu,fursa na vitisho.
Alisema vyombo vya habari
vinapaswa kutumia nafasi yake kukosoa utekelezaji mbovu wa sera ili sekta husika ziweze kubadilika,kujisahihisha,kuwa
makini na kufanya usimamizi mzuri na
hatimaye kufikia lengo lililokusudiwa la kumsaidia mtanzania.
Hata hivyo wakipitia
muhtasari wa mada ya sera washiriki wa mafunzo hayo walisema wamepata ufahamu
mkubwa na kubaini kuwa sera zinatungwa ngazi za juu bila kushirikishwa wananchi na hivyo kushindwa kutekelezeka,.
Aidha katika mafunzo hayo
imebainika kuwa baadhi ya wanahabari wamekuwa wakilipua katika kufanya kazi zao
kwani hawazami kwa undani katika
uandishi kutokana na kutojuwa sera ikiwemo umuhimu wa vyombo vya habari katika
kufuatilia na kutathmini utekelezaji wa sera.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment