Translate

Sunday, August 25, 2013

WILAYA YA MOMBA – WATU SABA WAKAMATWA KWA KOSA LA KUHARIBU MALI NA KUJERUHI. WENGINE WASHIKILIWA KUINGIA NCHINI BILA KIBALI.




TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI
“PRESS RELEASE” TAREHE 24. 08. 2013.

WILAYA YA MOMBA – WATU SABA WAKAMATWA KWA KOSA LA KUHARIBU MALI NA
                                           KUJERUHI.

MNAMO TAREHE 21.08.2013 MAJIRA YA  SAA 12:00HRS HUKO KATIKA KITONGOJI CHA MCHANGANI KIJIJI CHA SENGA KATA YA  KAMSAMBA WILAYA YA  MOMBA MKOA WA MBEYA.  KUNDI LA WANANCHI WALIOAMUA KUJICHUKULIA SHERIA MKONONI KUTOKA KATIKA KIJIJI CHA ILAMBO KATA YA  KAPETA WILAYA YA  SUMBAWANGA VIJIJINI MKOA WA RUKWA WALIVAMIA MAKAMBI YA  WAVUVI YALIYOPO KATIKA KIJIJI HICHO NA KUWAPIGA KWA KUTUMIA FIMBO KISHA KUCHOMA MOTO MABANDA KADHAA YA  WAVUVI YALIYOJENGWA KWA KUTUMIA NYASI.

CHANZO CHA TUKIO HILO NI KUGOMBEA  ENEO LA VIJIJI TAJWA. UFUATILIAJI WA MGOGORO HUU UNAENDELEA.  JUMLA YA  WATU SITA WALIJERUHIWA KATIKA TUKIO HILO AMBAO NI 1. MSABAHA S/O JUMA, MIAKA 40, MZARAMO,MKULIMA/MVUVI  2. MAXIMO S/O MWAKANYEMBA, MIAKA 24,KYUSA,MKULIMA/MVUVI  3. MICHAEL S/O SANGA, MIAKA 30,MKINGA,MKULIMA/MVUVI 4. CHONDE S/O KALISTO, MIAKA 56, MNYAMWANGA, MKULIMA/MVUVI 5. ZAWADI S/O JOHN SICHULA, MIAKA 39, MNYAMWANGA, MKULIMA/MVUVI NA 6. GIBSON S/O EDWARD KACHINGWE, MIAKA 26, MSAGALA, MKULIMA/MVUVI WAHANGA WOTE NI WAKAZI WA KIJIJI CHA SENGA NA WALIPATIWA MATIBABU NA KURUHUSIWA HALI ZAO ZINAENDELEA VIZURI.

 KUFUATIA TUKIO HILO JUMLA YA  WATUHUMIWA SABA WAMEKAMATWA. TARATIBU ZINAFANYWA ILI WAFIKISHWE MAHAKAMANI AMBAO NI 1. SAMWEL S/O DAUD, MIAKA 42, MNYIHA,  MKULIMA 2. GERVAS S/O LUKAS, MIAKA 52, MSUKUMA, MKULIMA 3.NYERERE S/O MWITA,  MIAKA 52,MSUKUMA,MKULIMA 4.RICHARD S/O WILSON, MIAKA 43, MFIPA, MKULIMA 5. GEBRUS S/O RAMADHAN, MIAKA 28, MNYASA, MKULIMA 6. LULINDE S/O DASE, MIAKA 43, MSUKUMA, MKULIMA NA 7. FUNGUZA S/O MASANJA, MIAKA 43, MSUKUMA, MKULIMA WATUHUMIWA WOTE NI WAKAZI WA KIJIJI CHA SENGA KAMSAMBA. KWA SASA HALI NI SALAMA KATIKA ENEO HILO.

KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI  ANATOA WITO KWA JAMII  KUTOJICHULIA SHERIA MKONONI NA KUITATUA MIGOGORO YAO KWA NJIA YA  MAZUNGUMZO. AIDHA ANATOA RAI  KWA   YEYOTE MWENYE TAARIFA JUU YA  MAHALI WALIPO WATUHUMIWA  WENGINE WALIOHUSIKA NA TUKIO HILI AZITOE KATIKA MAMLAKA HUSIKA ILI WAKAMATWE NA SHERIA ICHUKUE MKONDO WAKE, VINGINEVYO WAJISALIMISHE MARA MOJA.

WILAYA YA  KYELA – KUPATIKANA NA POMBE HARAMU YA  MOSHI [GONGO].

MNAMO TAREHE 23.08.2013 MAJIRA YA  SAA 10:35HRS HUKO KYELA- KATI WILAYA YA  KYELA MKOA WA MBEYA. ASKARI POLISI WAKIWA DORIA WALIMKAMATA KAMWELA S/O MWASAMWENE,MIAKA 37,KYUSA,MKULIMA,MKAZI WA MBUGANI AKIWA NA POMBE HARAMU YA  MOSHI UJAZO WA LITA NANE [08] AKIWA AMEBEBA KWENYE BAISKELI YAKE. MTUHUMIWA NI MTUMIAJI NA MUUZAJI WA POMBE HIYO. TARATIBU ZINAFANYWA ILI AFIKISHWE MAHAKAMANI. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI  ANATOA WITO KWA JAMII KUACHA KUTUMIA POMBE HARAMU YA  MOSHI  KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NA NI HATARI KWA AFYA YA  MTUMIAJI.

WILAYA YA  MBEYA MJINI – KUINGIA NCHINI BILA KIBALI.

MNAMO TAREHE 23.08.2013  MAJIRA YA  SAA 17:30HRS HUKO UYOLE JIJI NA  MKOA WA MBEYA.  ASKARI POLISI WAKIWA DORIA WALIMKAMATA DEMARK S/O RAFOE,MIAKA 28,RAIA NA MKAZI WA NCHINI ETHIOPIA AKIWA AMEINGIA NCHINI BILA KIBALI. MBINU NI KUSAFIRI KWA NJIA YA  KIFICHO.  TARATIBU ZINAFANYWA ILI AKABIDHIWE IDARA YA  UHAMIAJII. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI  ANATOA WITO KWA JAMII KUENDELEA KUTOA TAARIFA KATIKA MAMLAKA HUSIKA KUHUSU WATU WANAOWATILIA SHAKA IKIWA NI PAMOJA NA RAIA WA KIGENI ILI HATUA ZA KISHERIA DHIDI YAO ZICHUKULIWE.
                                                        Signed by:
                                                        [ DIWANI ATHUMANI   - ACP ]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.

MAUAJI KYELA NA MOMBA,MBEYA



TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI
 “PRESS RELEASE” TAREHE 23. 08. 2013.
WILAYA YA  KYELA – MAUAJI.
MNAMO TAREHE 22.08.2013 MAJIRA YA  SAA 00:30 HRS HUKO KATIKA HOSPITALI YA  WILAYA YA  KYELA MKOA WA MBEYA. ARON S/O MSOLE, MIAKA 70, MNDALI, MKULIMA, MKAZI WA KIJIJI CHA IBANDA ALIFARIKI DUNIA WAKATI AKIENDELEA KUPATIWA MATIBABU HOSPITALINI HAPO. CHANZO NI BAADA YA  KUPIGWA JIWE UBAVUNI NA ANANIA S/O SIMTOE, MIAKA 50, MNYAMWANGA, MKULIMA, MKAZI WA IBANDA KUFUATIA NG’OMBE WAKE KUINGIA KATIKA SHAMBA LA MAREHEMU NA KUHARIBU MAZAO. MWILI WA MAREHEMU UMEFANYIWA UCHUNGUZI NA DAKTARI WA SERIKALI NA KUKABIDHIWA NDUGU KWA MAZISHI. MTUHUMIWA AMEKAMATWA. TARATIBU ZINAFANYWA ILI AFIKISHWE MAHAKAMANI. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI ANATOA WITO KWA JAMII KUTATUA MATATIZO/MIGOGORO YAO KWA NJIA YA  KUKAA MEZA YA  MAZUNGUMZO ILI KUEPUKA MATATIZO YANAYOWEZA KUEPUKIKA.

WILAYA YA  MOMBA – AJALI YA  GARI KUMGONGA MTEMBEA KWA MIGUU                     NA KUSABABISHA KIFO.

MNAMO TAREHE 22.08.2013 MAJIRA YA  SAA 05:30 HRS HUKO KATIKA KIJIJI CHA MPEMBA BARABARA YA  MBEYA/TUNDUMA WILAYA YA  MOMBA MKOA WA MBEYA. GARI NA DEREVA ASIYEFAHAMIKA JINA WALA MAKAZI YAKE LILIMGONGA MTEMBEA KWA MIGUU ASIYEFAHAMIKA JINA WALA MAKAZI YAKE,  JINSI YA  KIUME MWENYE UMRI KATI YA  MIAKA 30-35 NA KUSABABISHA KIFO CHAKE PAPO HAPO. MWILI WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA KITUO CHA AFYA TUNDUMA. DEREVA ALIKIMBIA NA GARI MARA BAADA YA  TUKIO. . KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI ANATOA WITO KWA MADEREVAKUWA MAKINI WANAPOTUMIA VYOMBO VYA MOTO KWA KUZINGATIA SHERIA ZA USALAMA BARABARANI ILI KUEPUKA AJALI ZINAZOWEZA KUEPUKIKA. AIDHA ANATOA RAI KWA YEYOTE MWENYE TAARIFA JUU YA  MAHALI ALIPO MTUHUMIWA AZITOE KATIKA MAMLAKA HUSIKA ILI AKAMATWE NA SHERIA ICHUKUE MKONDO WAKE, VINGINEVYO AJISALIMISHE MARA MOJA.
                                                                    Signed by:
(DIWANI ATUMANI – ACP)
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.

AJALI ZAUWA MBEYA




TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI
“PRESS RELEASE” TAREHE   22. 08. 2013.



WILAYA YA MBOZI – AJALI YA GARI KUACHA NJIA KUPINDUKA NA KUSABABISHA KIFO.

MNAMO TAREHE 21.08.2013 MAJIRA YA SAA 15:00 HRS HUKO KATIKA KIJIJI CHA LWATI BARABARA YA KAMSAMBA /MLOWO WILAYA YA MBOZI MKOA WA MBEYA. GARI T.855 ACJ AINA YA  M/FUSO LIKIENDESHWA NA DEREVA CLEMENT S/O EXAVERY, LILIACHA NJIA NA KUPINDUKA KISHA KUSABABISHA KIFO CHA LAUDEN S/O MWAMPANGALA, MIAKA17, MKULIMA, MNYIHA, MKAZI WA NAMBIZO NA MAJERUHI KWA WATU TISA WOTE WAMELAZWA KATIKA HOSPITALI YA  MBOZI MISHENI. CHANZO MWENDO KASI. MWILI WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA KATIKA ZAHANATI YA KIJIJI CHA NAMBIZO. DEREVA AMEKAMATWA. TARATIBU ZINAFANYWA ILI AFIKISHWE MAHAKAMANI. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI ANATOA WITO KWA MADEREVA KUWA MAKINI WANAPOTUMIA VYOMBO VYA MOTO KWA KUZINGATIA SHERIA ZA USALAMA BARABARANI ILI KUEPUSHA AJALI ZINAZOWEZA KUEPUKIKA.


WILAYA YA MBARALI - AJALI YA GARI KUMGONGA MTEMBEA KWA MIGUU NA KUSABABISHA KIFO.


RUJ/TR/AR/41/2013 – AJALI YA  GARI KUMGONGA MTEMBEA KWA MIGUU NA KUSABABISHA KIFO.
MNAMO TAREHE 21.08.2013 MAJIRA YA SAA 13:45 HRS HUKO KATIKA KIJIJI CHA MLANGALI WILAYA YA MBARALI MKOA WA MBEYA. GARI T.901 ASQ/T.415 AXA AINA YA  SCANIA LIKIENDESHWA NA DEREVA SHADRACK S/O HAMIS, MIAKA 34, MMAKUA, MKAZI WA IRINGA LIKITOKEA MBEYA KUELEKEA MAFINGA LILIMGONGA MTEMBEA KWA MIGUU MONICA D/O MHAHWA, MIAKA 56, MBENA, MKAZI WA MAKETE NA KUSABABISHA KIFO CHAKE MUDA MFUPI BAADA YA  KUFIKISHWA KATIKA HOSPITALI YA  MISHENI CHIMALA. CHANZO CHA AJALI KINACHUNGUZWA. DEREVA AMEKAMATWA. MWILI WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA KATIKA HOSPITALI HIYO. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI ANATOA WITO KWA MADEREVA KUWA MAKINI WANAPOTUMIA VYOMBO VYA MOTO KWA KUZINGATIA SHERIA ZA USALAMA BARABARANI ILI KUEPUSHA AJALI ZINAZOWEZA KUEPUKIKA.



[ DIWANI ATHUMANI – ACP ]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.


VIJANA WALIOMALIZA KIDATO CHA NNE MWAKA 2012 NA CHA SITA MWAKA 2013 NA KUCHAGULIWA KUFANYA USAILI WA KUJIUNGA NA JESHI LA POLISI INAPATIKANA KWENYE TOVUTI YA POLISI www.policeforce.go.tz.



TANGAZO                            TANGAZO                            TANGAZO                   TANGAZO
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA DIWANI ATHUMANI – ACP ANAWATANGAZIA WANANCHI WOTE YA KUWA ORODHA YA MAJINA YA VIJANA WALIOMALIZA KIDATO CHA NNE MWAKA 2012 NA CHA SITA MWAKA 2013 NA KUCHAGULIWA KUFANYA USAILI WA KUJIUNGA NA JESHI LA POLISI INAPATIKANA KWENYE TOVUTI YA POLISI www.policeforce.go.tz.
MUHIMU.                                                                                                          
       i.            MWOMBAJI ANARUHUSIWA KUFANYA USAILI KWENYE KITUO CHOCHOTE CHA USAILI KILICHO KARIBU NAE KULINGANA NA TAREHE ZINAVYOONYESHA KWENYE TANGAZO LA USAILI.
     ii.            KWA MKOA WA MBEYA NA IRINGA KITUO CHAO NI MBEYA NA USAILI UTAFANYIKA KUANZIA TAREHE 16/09/2013 HADI 19/9/2013 SAA 2:00 ASUBUHI HADI SAA 10:00 JIONI KATIKA OFISI YA KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
  iii.            MWOMBAJI ALIYEITWA KWENYE USAILI AJE NA VYETI VYOTE VYA MASOMO(ACADEMIC CERTIFICATES),RESULTS SLIP(S) NA LEAVING CERTIFICATE(S), NAKALA HALISI YA CHETI CHA KUZALIWA(ORIGINAL BIRTH CERTIFICATE). HATI YA KIAPO CHA KUZALIWA HAITAKUBALIWA.
  iv.            MWOMBAJI AWE NA NANMBA YA SIMU AMBAYO ITAMJULISHA ENDAPO ATAKUBALIWA.
     v.            KILA MWOMBAJI ALIYEITWA KWENYE USAILI ATAJIGHARAMIA USAFIRI, CHAKULA, NA MALAZI KWA MUDA WOTE WA ZOEZI LA USAILI.


v    NI MUHIMU SANA KILA MWOMBAJI KUZINGATIA MUDA WA KUANZA USAILI.

Tamasha la TGNP lilete matumaini kwa wanawake


Na Thompson Mpanji,Mbeya

MTANDAO   wa jinsia Tanzania(TGNP) kwa kushirikiana na wanaharakati na wadau mbalimbali wanatarajia kushiriki Tamasha  mapema septemba,3,2013 ambapo litatoa nafasi  na fursa  kwa wanaharakati  zaidi ya 5,000 kushiriki kutoka ndani na nje  ya Tanzania.

Tukio hili la siku nne,linajumuisha uchambuzi,utafiti,uanaharakati,kujenga uwezo,sanaa vyote vikiwa  na matokeo dhahiri ili kutoa ama kuonesha ushuhuda wa yale yanayojiri miongoni mwetu.

Malengo ya tamasha la jinsia 2013 ni kusherehekea  miaka ishirini  ya harakati za ukombozi wa wanawake kimapinduzi inayochangia upatikanaji wa haki za wanawake,usawa wa kijinsia na haki za kijamii.

Kuongeza  uelewa  wa  muktadha uliopo kimataifa,wa mfumo dume na uliberali mamboleo,madhara yake kwa wanawake walioko pembezoni na jamii zao,mapambano yao dhidi  ya mifumo chanya na mingine kandamizi,na mikakati mbadala kwa ajili ya ukuaji na maendelo endelevu yenye usawa na haki.

Aidha kuendeleza uelewa wa nadharia na vitendo  kwenye ukombozi wa wanawake kimapinduzi,ikiwa ni pamoja  na kutunza  kumbukumbu  za mapambano halisi dhidi ya mfumo dume na uliberali mamboleo,na jinsi ya kuimarisha  ukombozi wa wanawake kimapinduzi katika ngazi zote.

Tunasema hongera TGNP,wadau na wanaharakati wengine kuazimisha Tamasha hilo ambalo ninaamini litawapatia mwelekeo wenu katika harakati hizi za kumkomboa binadamu na hasa mwanamke.

Ninaweza kusema kuwa Tamasha hilo litasaidia kufanya ufuatiliaji na tathmini  kuhusu mlikotoka,mlipo na mnapoelekea katika harakati hizi ngumu ambazo kwa wakati mwingine zinahatarisha maisha na hivyo kuhitaji moyo wa kujitolea na kujituma zaidi kutoka ndani ya sakafu ya moyo,ndani ya mishipa na damu kwa ujumla.

Tunaamni kuwa tamasha hilo pia litawaweka pamoja na kupanga mikakati na mipango kazi  itakayotekelezeka katika ngazi zote kwa ajili ya ujenzi wa harakati za ukombozi wa wanawake kimapinduzi nchini Tanzania,Afrika na dunia kwa ujumla.

Tamasha hili litasaidia kuimarisha  utambuzi,mitandao,ujenzi wa nguvu za pamoja na miungano ya ukombozi wa wanawake kimapinduzi kama misingi  ya kuelekea tapo la ukombozi wa wanawake kimapinduzi wa Afrika.

Tunaambiwa kuwa katika Tamasha hilo kutakuwa na  Mada mbalimbali kama vile jinsia Demokrasia na maendeleo,miaka 20 ya harakati za ukombozi wa wanawake kimapinduzi,haki na usawa wa kijinsia,tuko wapi na tunakwenda wapi,Mapambano  ya haki  ya ardhi na uchumi,rudisha rasilimali kwa wananchi,mapambano ya ukombozi wa  wanawake kimapinduzi kwa ajili ya Demokrasia kwenye vyombo vya kiserikali na visivyo vya kiserikali.

Mada nyingine ni pamoja na mabadiliko ya katiba au mapinduzi,Mapambano  ya ukombozi wa wanawake kimapinduzi na ujenzi wa tapo miaka ishirini ijayo sanjari na ujenzi wa umoja wa Afrika kwa mtazamo wa ukombozi  wa wanawake kimapinduzi.


Kabla ya kuendelea tuangalie hili Shirika la TGNP linatoka wapi na linafanya nini katika jamii,ni miongoni mwa mashirika  yasiyo ya kiserikali yanayofanya jitihada mbalimbali katika kuhakikisha tatizo hili linakomeshwa kabisa  na kutoweka katika jamii ya kitanzania na dunia kwa ujumla.

Ni shirika  la kiraia na kiuharakati,linalotetea mabadiliko ya kijamii kwa mtazamo wa kifeministi ambayo yanalenga  kwenye usawa wa jinsia,ukombozi wa wanawake,haki za kijamii,kufikia na kumiliki rasilimali kwa wanawake,vijana  na makundi mengine  yaliyoko pembezoni.

Dhana ya TGNP ni kujenga tapo la mabadiliko  katika jamii,ambalo litachangia kuwepo kwa jamii yenye mabadiliko ambayo inatambua  na kuthamini masuala ya jinsia,demokrasia,haki za binadamu na haki za kijamii.

Kwa mujibu wa Ofisa uhusiano wa TGNP Kenny Ngomuo anasema septemba,3,2013 ni Tamasha  la jinsia  ambalo huandaliwa  na mtandao wa jinsia Tanzania(TGNP) wakishirikiana  na mtandao wa mashirika  watetezi wa haki za binadamu na usawa wa jinsia (FemAct),pamoja na washirika  wao wengine  kama mitandao ya jinsia  ngazi ya kati ( IGNs),zilizopo  katika ngazi za wilaya,makundi mbalimbali ya kijamii ambayo ni sehemu ya semina  za jinsia na maendeleo (GDSS) za TGNP, na vikundi vingine  ambavyo  vimetambuliwa  katika utafiti kuhusu harakati za ukombozi wa wanawake kimapinduzi (TFMB).

Ngomuo ansaema Tamasha la jinsia  ni nafasi ya wazi kwa ajili ya watu binafsi,mashirika na mitandao,walio katika mapambano yanayofanana,kubadilishana uzoefu,taarifa,kujengeana uwezo,kusherehekea mafanikio  na kutathmini changamoto zilizo mbele yao,kujenga  na kuimarisha mitandao,na kupanga kwa pamoja  mikakati kwa ajili ya kuleta mabadiliki  ya kijamii kwa mtazamo wa kifeministi,kujengeana uwezo ili kuchangia katika mijadala ya wazi kuhusu maendeleo ya jamii na binafsi.

Ofisa huyo anasema Lengo  kuu la tamasha  ni kuwaleta pamoja wanawake/wanaharakati wa kifeministi na wengineo,ambao wanawamini kwenye usawa wa jinsia na  ukombozi wa wanawake ,kutoka Nyanja zote za maisha ,kutoka vijiji na wilaya za Tanzania,na sehemu  mbalimbali duniani,kwa lengo la uanaharakati na ushirikishanaji wa taarifa  kwa masuala mahsusi.

Anasema taswira ya TGNP inafanya jitihada za kuwezesha ukuaji wa vuguvugu la ukombozi wa mwanamke kimapinduzi lenye misingi yake katika jamii hivyo kupelekea kufanyakazi moja kwa moja na wanaharakati katika makundi ya kijamii,wanamtandao na makundi ya muungano  katika ngazi mbalimbali.

Ngomuo anasema mkazo mkubwa unawekwa  katika kukuza uwezo wa hayo makundi na mitandao ili yaweze kufanya uchambuzi wa kijinsia  na ujenzi wa nguvu ya pamoja katika kutekeleza mipango yenye kuleta mabadiliko ndani  ya jamii zao na kujenga  mahusiano na wengine  katika ngazi ya jamii ya taifa,kikanda na kimataifa.

Anafafanua zaidi kuwa dhima ya TGNP ni kuwa chachu katika ujenzi  wa harakati za vuguvugu la ukombozi wa mwanamke kimapinduzi unaolenga kubomoa mfumo dume na mifumo mingine kandamizi ikiwepo ukoloni mamboleo,ubeberu na ubepari ngazi zote,kutetea,kushawishi na kushinikiza  uwepo wa usawa wa jinsia,ukombozi wa mwanamke kimapinduzi,haki ya kijamii.


Aidha Ngomuo anabainisha Dira yao ni kuwepo kwa jamii ya Tanzania inayoheshimu  usawa wa jinsia  na haki ya kijamii,kusimamia haki za jamii.

Hata hivyo anahitimisha kwa kuelezea mafanikio  kwa miaka 20 tangu TGNP ianzishwe ni kuwa imefanikiwa kushawishi sera za umma kuingiza masuala ya harakati za vuguvugu la ukombozi wa mwanamke kimapinduzi,ikiwepo kuingiza masuala ya usawa wa kijinsia na haki za kijamii kwenye mifumo na taasisi ikiwemo na kukuza hamasa na uelewa wa wanachama,washiriki na serikali,kila lakheri TGNP na wadau wengine katika Tamasha hilo ambalo litaongeza kasi,ari na nguvu ya kufanyakazi zaidi!!.

tmpanji@yahoo.com
www.mpanjimwanamai.blogspot.com
0765 813180