Translate

Tuesday, February 12, 2013

habari na historia kuhusiana na kujihudhuru papa B.16


    
Maskani > Kanisa >  2013-02-12 09:48:37
A+A-Chapisha ukurasa huuTuma kwa e-mail

http://sw.radiovaticana.va/global_images/x.gif
http://sw.radiovaticana.va/global_images/x.gif
Mchakato wa kumtafuta Papa Mpya kuanzia tarehe Mosi, Machi 2013
http://sw.radiovaticana.va/global_images/x.gif
http://sw.radiovaticana.va/global_images/x.gif
http://media01.radiovaticana.va/imm/1_0_664106.JPGPadre Federico Lombardi akielezea kuhusu tamko la Baba Mtakatifu Benedikto wa kumi na sita la kung'atuka kutoka madarakani mintarafu sheria za Kanisa anasema kwamba, ili Kiti cha Khalifa wa Mtakatifu Petro kiweze kuwa wazi, lazima idhihirishe wazi kwamba, kujiuzuru huku kuwe ni huru na wala si lazima kukubaliwe na wote.

Hivi ndivyo alivyofanya Baba Mtakatifu Benedikto wa kumi na sita, Jumatatu tarehe 11 Februari 2013 wakati wa Mkutano na Dekania ya Makardinali. Baba Mtakatifu atang'atuka rasmi madarakani hapo tarehe 28 Februari 2013, saa 2:00 Usiku. Tangu wakati huo Kiti cha Khalifa wa Mtakatifu Petro kitakuwa wazi kadiri ya Sheria za Kanisa.

Padre Lombardi anasema, Baba Mtakatifu Benedikto wa kumi na sita alipohojiwa na Bwana Peter Seewald, mwandishi wa kitabu alionesha kwamba, kuna uwezekano mkubwa kwa Khalifa wa Mtakatifu Petro kujiuzuru wadhifa wake katika hali ya amani, anapojisikia kwamba, hana tena nguvu ya kuweza kulihudumia Kanisa kwa tija na ufanisi mkubwa kutokana na matatizo ya afya, akili na kiroho. Kwa mazingira kama haya Papa anapaswa na kulazimika kujiuzuru wadhifa wake.

Baba Mtakatifu Benedikto wa kumi na sita, anatarajiwa kuhamia Ikulu ndogo ya Castel Gandolfo, nje kidogo ya mji wa Roma, ili kukamilisha baadhi ya majukumu yake katika uongozi. Wakati huo huo, ukarabati wa nyumba atakamoishi Baba Mtakatifu Benedikto wa kumi na sita, mjini Vatican utakuwa unakamilika. Mchakato wa kumchagua Khalifa wa Mtakatifu Petro, utaanza rasmi hapo tarehe Mosi Machi 2013. Padre Lombardi anasema kwamba, bado tarehe rasmi haijapangwa, lakini hakutakuwa na haja ya kusubiri siku nane kama zinavyotajwa wakati wa maombolezo ya kifo cha Papa.

Katika kipindi cha majuma mawili katika mwezi Machi, Kanisa litakuwa na Papa Mpya. Baba Mtakatifu Benedikto wa kumi na sita, kwa unyenyekevu mkubwa hatahusika kwenye Mkutano wa kumchagua Papa mwingine wala kujihusisha na shughuli za uongozi wa Kanisa kadiri ya sheria za Kanisa. Wakati huu Kanisa litakuwa chini ya Dekano wa Makardinali ambaye kwa sasa ni Kardinali angelo Sodano na Kardinali Tarcisio Bertone.

Padre Federico Lombardi anahitimisha kwamba kusema kwamba, binafsi amepokea tamko la Baba Mtakatifu Benedikto wa kumi na sita la kung'atuka kutoka madarakani kwa mshangao na hamasa kubwa kutokana na uhuru wake wa ndani pamoja na kujali wajibu na utume wa Khalifa wa Mtakatifu Petro kwa ajili ya mafao ya Kanisa. Baba Mtakatifu Benedikto wa kumi na sita, ameonesha ushuhuda mkubwa wa uhuru wa maisha ya kiroho, busara na hekima katika kuliongoza Kanisa kwenye Karne ya 21 yenye changamoto nyingi.


Kanisa limelipokea Tamko la Baba Mtakatifu Benedikto XVI kwa mshangao mkubwa!
http://sw.radiovaticana.va/global_images/x.gif
http://sw.radiovaticana.va/global_images/x.gif
http://media01.radiovaticana.va/imm/1_0_664087.JPGKardinalo Angelo Sodano, Dekano wa Makardinali, Jumatatu tarehe 11 Februari 2013 kwa niaba ya Makardinali wenzake amemwambia Baba Mtakatifu Benedikto wa kumi na sita kwamba, wamepokea habari za kung'atuka kwake madarakani kwa mshangao mkubwa! Ni tamko linaloonesha upendo mkuu kwa Kanisa la Mungu.

Makardinali wataendelea kumwonesha mshikamano na ushirikiano wa dhati hasa wakati huu baada ya kufanya maauzi mazito kwa ajili ya mafao na ustawi wa Kanisa baada ya kuliongoza Kanisa Katoliki kwa takribani miaka 8. Ilikuwa ni tarehe 19 Aprili 2005 alipokubali kubeba dhamana ya uongozi wa Kanisa Katoliki, akajiweka chini ya ulinzi na usimamizi wa Bikira Maria, akifuata nyayo za watangulizi wake 265 waliowahi kuliongoza Kanisa Katoliki tangu Mtakatifu Petro, yapata miaka elfu mbili iliyopita.

Kardinali Sodano anabainisha kwamba, kabla ya tarehe 28 Februari 2013, saa 2:00 Usiku, watapata nafasi ya kutoa heshima na shukrani zao za dhati, kama ambavyo watafanya viongozi wa Kanisa, Waamini na Watu wenye mapenzi mema kutoka sehemu mbali mbali za dunia. Katika kipindi hiki cha mpito, Kanisa bado litaendelea kumsikiliza Baba Mtakatifu Benedikto wa kumi na sita, katika mahubiri yake Jumatano ya Majivu, Mama Kanisa anapokianza kipindi cha Kwaresima; kwenye Katekesi zake Jumatano, Mkutano pamoja na Makleri wa Jimbo kuu la Roma pamoja na tafakari zake wakati wa Sala ya Malaika wa Bwana.

Kanisa kuwatangaza watakatifu wapya watatu hapo tarehe 12 Mei 2013
http://sw.radiovaticana.va/global_images/x.gif
http://sw.radiovaticana.va/global_images/x.gif
http://media01.radiovaticana.va/imm/1_0_664094.JPGBaba Mtakatifu Benedikto wa kumi na sita katika mkutano maalum na Dekania ya Makardinali hapo tarehe 11 Februari 2013 ameridhiwa Wenyeheri wafuatao kutangazwa kuwa watakatifu hapo tarehe 12 Mei 2013.

1. Mwenyeheri Antonio Primaldo na Wenzake: wafiadini.
2. Laura wa Mtakatifu Catherina wa Siena Montoya y Upegui, Bikira na Mwanzilishi wa Shirika la Masista Wamissionari wa Bikira Maria Mkingiwa Dhambi ya Asili na Shirika la Mtakatifu Catherina wa Siena.
3. Maria Guadalupe garcia Zavala, Mwanzilishi mwenza wa Shirika la Wahudumu wa Mtakatifu Margharita Maria wa Maskini.

Baba Mtakatifu Benedikto wa kumi na sita, aliungana na Makardinali 51 kwa kusali pamoja Sala ya Kanisa pamoja na kutoa mahubiri mafupi. Baada ya kupata maelezo ya kina kuhusu Wenyeheri hawa kutoka kwa Kardinali Angelo Amato, Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa linaloshughulikia kuwatangaza waamini kuwa wenyeheri na watakatifu, aliuliza maoni ya Makardinali nao wakakubali, ili waweze kutangazwa na kuandikwa kwenye Orodha ya Majina ya Watakatifu wa Kanisa Katoliki.

Viongozi wa Jumuiya ya Kimataifa wanampongeza na kumshukuru Baba Mtakatifu Benedikto XVI kwa unyenyekevu na ujasiri mkuu!
http://sw.radiovaticana.va/global_images/x.gif
http://sw.radiovaticana.va/global_images/x.gif
http://media01.radiovaticana.va/imm/1_0_664092.JPGTamko la Baba Mtakatifu Benedikto wa kumi na sita alilolitoa Jumatatu tarehe 11 Februari 2013 kuhusu kung'atuka kwake kutoka madarakani kutokana na sababu za umri na afya, zimewashtua watu wengi kiasi cha kubaki wameshika tama!

Habari kutoka sehemu mbali mbali za dunia zinaonesha kutambua mchango wa Baba Mtakatifu Benedikto wa kumi na sita pamoja na kuupokea uamuzi wake kwa heshima na taadhima, kwani kitendo cha ujasiri, moyo mkuu, unyenyekevu na uwajibikaji. Ni maneno ya Rais Giorgio Napolitano wa Italia, ambaye hivi karibuni walikuwa pamoja kusikiliza Tamasha la muziki lililokuwa limeandaliwa kwa ajili ya Maadhimisho ya Kumbu kumbu ya Mkataba wa Laterano.

Kardinali Angelo Bagnasco, Rais wa Baraza la Maaskofu Katoliki Italia anasema, kwa mara nyingine tena, Baba Mtakatifu Benedikto wa kumi na sita, ameonesha mfano na kielelezo cha kuigwa kwa ajili ya mafao ya Kanisa, kwa kuamua kung'atuka kutoka madarakani kwa utashi na uhuru kamili. Kanisa Katoliki nchini Italia linamshukuru kwa mchango wake wa hali na mali katika maisha na utume wa Kanisa nchini Italia.

Naye Chancellor Angela Merkel wa Ujerumani anasema amezipokea habari hizi kwa mshtuko mkubwa kiasi cha kuamsha ndani mwake heshima kubwa kwa Baba Mtakatifu Benedikto wa kumi na sita kutokana na mikutano yao mjini Roma na alipopata fursa ya kutembelea Ujerumani kunako mwaka 2011. Anakumbuka kwa namna ya pekee hotuba yake kwa Bunge la Shirikisho la Wananchi wa Ujerumani kuhusu dhamana ya wanasiasa katika Jamii: kusimama kidete kulinda na kutetea haki na ukweli. Ni changamoto ambayo imeacha chapa ya kudumu katika maisha yake.

Rais Francois Hollande wa Ufaransa anasema kwamba, huu ni uamuzi mgumu unaopaswa kuheshimiwa, kwa namna ya pekee kabisa anampongeza Baba Mtakatifu Benedikto wa kumi na sita kwa ujasiri na unyenyekevu wa aina hii.

Waziri mkuu wa Uingereza David Cameron amemwandikia Baba Mtakatifu Benedikto wa kumi na sita, ujumbe wa matashi mema na kwamba, watu wengi watakosa hekima na busara yake kama Kiongozi mkuu wa Kanisa. Amejitahidi sana kuhakikisha kwamba, uhusiano kati ya Uingereza na Vatican unaendelea kuimarika.

Askofu mkuu Justin Welby wa Kanisa kuu la Cantebury ambaye pia ni Kiongozi Mkuu wa Jumuiya ya Waanglikani Duniani, anasema, amepokea kwa mshangao mkubwa taarifa za kung'atuka kwa Baba Mtakatifu Benedikto wa kumi na sita kutoka madarakani. Kuwa Khalifa wa Mtakatifu Petro ni dhamana nyeti na yenye heshima ya hali ya juu, inayohitaji kuwa na mwono mpana na ujasiri.

Askofu mkuu Welby anamshukuru Mwenyezi Mungu kwa zawadi ya uwepo wa Papa Benedikto wa kumi na sita aliyejitoa bila ya kujibakiza kuliongoza Kanisa: kwa maneno na matendo yake; kwa sala na huduma za kichungaji, kama mfuasi amini wa Kristo.

Viongozi wengi wanamkumbuka Baba Mtakatifu Benedikto wa kumi na sita kwa kuendelea kuhamasisha majadiliano ya kidini na kiekumene; huku akisimama kidete kulinda na kutetea: haki, amani, upendo na mshikamano katika Jumuiya ya Kimataifa, kwa kuongozwa na kanuni auni. Ni matumaini ya viongozi mbali mbali wa kidini kwamba, Kanisa Katoliki litaendeleza majadiliano ya kidini na kiekumene kwa ajili ya mafao ya wengi, amani na ustawi wa Jumuiya ya Kimataifa. Wanaendelea kumtakia afya njema, utulivu na amani ya ndani.

Ni uamuzi wa busara unaofumbata hali ya unyenyekevu na ujasiri mkuu, unaoacha chapa ya kudumu kwa watu wengi. Ni Kiongozi aliyeshirikiana na wengine kuhimiza tunu msingi za maisha ya binadamu. Kwa hakika, uamuzi wake unapaswa kuheshimiwa na kuthaminiwa. Amefanya jambo la msingi kwa wakati muafaka.




Monday, February 11, 2013

Papa Benedikto XVI atangaza kujuuzuru kutoka katika madaraka ya kuliongoza Kanisa Katoliki



Papa Benedikto XVI atangaza kujuuzuru kutoka katika madaraka ya kuliongoza Kanisa Katoliki 

http://sw.radiovaticana.va/global_images/x.gif



Baba Mtakatifu Benedikto wa kumi na sita katika maadhimisho ya Mkutano wa Makardinali Jumatatu, tarehe 11 Februari 2013, ametangaza rasmi kwamba, kuanzia tarehe 28 Februari 2013 saa 2:00 Usiku atang'atuka kutoka madarakani na viongozi wenye dhamana ya kuitisha mkutano wa kumchagua Khalifa wa Mtakatifu Petro, watapaswa kufanya hivyo.

Baba Mtakatifu anasema, baada ya kuchunguza dhamiri yake mbele ya Mwenyezi Mungu pamoja na umri wake, anatambua kwamba, hana tena nguvu ya kutekeleza majukumu yake kama Khalifa wa Mtakatifu Petro. Huu ni utume ambao unapaswa kutekelezwa kwa maneno na matendo; sala na mateso.

Ulimwengu huu unakabiliwa na mabadiliko makubwa katika imani, jambo ambalo linahitaji kwa kiasi kikubwa maisha ya imani, ili kuweza kuliongoza Kanisa na kutangaza Injili ya Kristo. Baba Mtakatifu Benedikto wa kumi na sita anasema kwa unyenyekevu kwamba, katika miezi ya hivi karibuni, ametambua kwamba, hawezi tena kutekeleza majukumu yake kikamilifu.

Kwa utashi na uhuru kamili anatamka wazi kwamba, dhamana ya kuwa Khalifa wa Mtakatifu Petro, aliyokabidhiwa na Makardinali kunako tarehe 19 Aprili 2005 itafikia ukomo wake hapo tarehe 28 februari 2013 saa 2:00 Usiku. Baba Mtakatifu anawashukuru wote kwa upendo na kazi walizoshirikiana kwa pamoja katika kutekeleza majukumu yake kama Khalifa wa Mtakatifu Petro. Anaomba radhi kwa mapungufu yake ya kibinadamu.

Kwa sasa analikabidhi Kanisa kwa Yesu Kristo mchungaji mkuu. Anamwomba Bikira Maria kuwasaidia Makardinali katika mchakato wa kumchagua Khalifa wa Mtakatifu Petro. Anasema, ataendelea kulitumikia Kanisa katika maisha ya Sala.

Sunday, February 10, 2013

Papa B.16 kanisa katoliki tanzania na huduma ya afya

Kanisa Katoliki Tanzania limekuwa ni mdau mkubwa wa huduma katika sekta ya afya!



Baba Mtakatifu Benedikto wa kumi na sita katika Waraka wake wa kichungaji, Dhamana ya Afrika anabainisha kwamba, Kanisa tangu awali limekuwa likijihusisha na utoaji wa huduma ya afya kwa kuendeleza lile agizo la Kristo kwa wafuasi wake la kuponya magonjwa na udhaifu wa kila aina. RealAudioMP3

Hii ni changamoto kwa Taasisi za Kanisa zinazotoa huduma ya afya pamoja na wahudumu wa sekta ya afya kujitahidi kuona kwamba, kila mgonjwa ni kiungo kinachoteseka cha Fumbo la Mwili wa Kristo, yaani Kanisa. Wahudumu wa sekta ya afya wanachangamotishwa na Baba Mtakatifu kuwaonjesha wagonjwa ule upendo wenye huruma unaobubujika kutoka kwa Yesu mwenyewe, kwa ajili ya watu wenye shida. Anawataka kusimama imara katika imani na matumaini na kamwe wasife moyo wala kukata tamaa.

Taasisi za huduma ya afya hazina budi kuongozwa kufuatana na kanuni maadili za Kanisa, daima zikijitahidi kuenzi Injili ya uhai; daima ziwakumbushe wahudumu wa sekta ya afya na wagonjwa kwamba, Mungu peke yake ndiye Bwana wa uhai na mauti. Ndiyo changamoto ambayo Kanisa Katoliki Tanzania limeendeleza hadi wakati huu linapomshukuru Mungu kwa kumwimbia utenzi wa shukrani kwa miaka 150 ya Uinjilishaji wa kina, ambao umejionesha kwa namna ya pekee katika huduma, hususan kwenye sekta ya Afya na Elimu.

Katika mahojiano maalum na Radio Vatican, Askofu mkuu Josephat Lebulu wa Jimbo kuu la Arusha, Tanzania anabainisha kwamba, huduma kwa wagonjwa na wote wanaosukumizwa pembezoni mwa Jamii ni sehemu ya wito na utume wa Kanisa. Kanisa Katoliki nchini Tanzania, licha ya wakati fulani Serikali kutaifisha Hospitali, Zahanati na Vituo vya Afya vilivyokuwa vinamilikiwa na kuendeshwa na Kanisa Katoliki Tanzania, limeendelea kuwekeza katika sekta ya afya, kama lengo la kumhudumia mtu mzima: kiroho na kimwili.

Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania limeendelea kuratibu huduma hizi katika Majimbo na Parokia mbali mbali, ili kuhakikisha kwamba, zinakwenda kadiri ya sheria, kanuni na taratibu za Kanisa Katoliki, kwa kulenga kudumisha zawadi ya uhai, utu na heshima ya mwanadamu aliyeumbwa kwa sura na mfano wa Mungu. Kanisa pia limekuwa mstari wa mbele katika utoaji wa huduma ya maji safi na salama sehemu mbali mbali za Tanzania na kwamba, limeendelea kuwa ni mdau mkubwa wa maendeleo endelevu nchini Tanzania.

Askofu Mkuu Lebulu anasema kwamba, kwa hakika katika kipindi cha Miaka 150 ya Uinjilishaji nchini Tanzania, Kanisa Katoliki limepiga hatua kubwa katika utekelezaji wa wito na utume wake miongoni mwa Watanzania na kwa sasa wanayo haki ya kumwimbia Mungu utenzi wa sifa na shukrani na hasa wakati huu wa Maadhimisho ya Mwaka wa Imani.



Marehemu Askofu Msarikie kuzikwa hapo tarehe 14 Februari 2013 kwenye Kanisa kuu la Kristo Mfalme, Moshi

Marehemu Askofu Msarikie kuzikwa hapo tarehe 14 Februari 2013 kwenye Kanisa kuu la Kristo Mfalme, Moshi



Askofu mstaafu Amedeus Msarikie wa Jimbo Katoliki Moshi, aliyefariki dunia wakati akipata matibabu Jijini Nairobi, anatarajiwa kuzikwa kwenye Kanisa kuu la Kristo Mfalme, Jimbo Katoliki Moshi, hapo tarehe 14 Februari 2013.

Taarifa kutoka Jimbo Katoliki Moshi zinabainisha kwamba, Mwili wa Marehemu Askofu Msarikie unatarajiwa kuwasili kwenye Kiwanja cha Kimataifa cha Kilimanjaro KIA, Jumatano asubuhi tarehe 13 Februari 2013 na baadaye msafara kuelekea kwenye Kanisa kuu, ambako waamini na watu wenye mapenzi mema watapata fursa ya kutoa heshima zao za mwisho.

Askofu Amedeus Msarikie amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 82, baada ya kuliongoza Jimbo Katoliki Moshi kwa kipindi cha miaka 23. Marehemu Askofu Msarikie anakumbukwa na wengi kwa kupenda kuwekeza zaidi katika elimu. Wachunguzi wa mambo wanasema, pengine Jimbo Katoliki Moshi ni kati ya Majimbo ya Kanisa Katoliki Tanzania yaliyowekeza kwa kiasi kikubwa katika sekta ya elimu, kuanzia: elimu ya awali, msingi, sekondari na vyuo. Alikuwa ni muasisi wa Chuo Kikuu kishiriki cha elimu, Mwenge.

Anakumbukwa kwa namna ya pekee na Mapadre na wote waliopitia mikononi mwake alipokuwa Baba mlezi wa maisha ya kiroho, St. James Seminary. Kwa miaka mingi amekuwa ni Mwenyekiti wa Tume ya Walei Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania na matunda ya kazi zake kwa kushirikiana na Maaskofu wengine yanaonekana. RIP. Amina.

caritas kukutana kuwasaidia wakimbizi

   Maskani > Upendo na mshikamano >  2013-02-09 13:39:13
A+ A- Chapisha ukurasa huu Tuma kwa e-mail



Caritas MONA, kukutana ili kujadili mikakati ya kuwasaidia wakimbizi kutoka Mashariki ya Kati na Afrika ya Kaskazini



Shirikisho la Mashirika ya Misaada ya Kanisa Katoliki Mashariki ya Kati, na Kaskazini mwa Afrika, Caritas MONA, linalojumuisha mashirika 17, kuanzia tarehe 20 hadi 22 Februari, 2013 litakuwa na mkutano wake mkuu, utakaofanyika mjini Amman, nchini Yordani. Tatizo la wakimbizi Mashariki ya Kati ni kati ya ajenda kuu zitakazofanyiwa kazi na wajumbe 41 waliokwisha thibitisha kwamba, watashiriki.

Kardinali Robert Sarah, Rais wa Baraza la Kipapa linaloratibu misaada ya Kanisa Katoliki, Cor Unum anatarajiwa pia kushiriki katika mkutano huu. Hapo tarehe 19 Februari, Kardinali Sarah atatembelea Familia za wakimbizi kutoka Syria ili kushiriki pamoja nao shida na mahangaiko yao ya ndani. Wajumbe wa mkutano huu wanatarajiwa pia kukutana na Mfalme Abdallah wa Pili wa Yordan.

Wajumbe pia watapembua kwa kina na mapana mikakati ya shughuli za kichungaji na utekelezaji wake katika huduma kwa wakimbizi, wahamiaji na watu wasiokuwa na makazi maalum katika maeneo yao. Mateso na mahangaiko ya wakimbizi kutoka Syria ni changamoto kwa Kanisa na Jumuiya ya Kimataifa katika ujumla wake.



Wednesday, February 6, 2013

Caritas na huduma za upendo

Maskani > Upendo na mshikamano >  2013-02-06 07:42:39
A+ A- Chapisha ukurasa huu Tuma kwa e-mail



Mikakati ya Caritas Rwanda katika huduma za upendo na mshikamano kwa Mwaka 2013



Shirika la Misaada la Kanisa Katoliki nchini Rwanda, Caritas, limehitimisha mkutano wake wa mwaka kwa kutoa mapendekezo yanayopaswa kufanyiwa kazi na vitengo vyake vikuu vinne yaani: Utawala, Afya, Maendeleo na Huduma za Kijamii. Utekelezaji huu unalihusisha pia Baraza la Maaskofu Katoliki Rwanda kwa kuliomba lijihusishe zaidi na zaidi katika huduma kwa wafungwa magerezani.

Tume ya haki, amani, familia, vijana na elimu imeombwa pia kuwa karibu zaidi na Caritas, ili kwa pamoja waweze kutoa huduma bora na makini zaidi kwa Familia ya Mungu nchini Rwanda. Katika Maadhimisho ya Mwaka wa Imani, Caritas Rwanda inatarajia kuchapisha ujumbe maalum kwa ajili ya waamini, kama sehemu ya mchakato wa kuendeleza huduma kwa wafungwa magerezani; wakimbizi na wahamiaji ambao bado wako kwenye kambi za wakimbizi nchini humo.

Caritas katika Majimbo mbali mbali nchini Rwanda inahamasishwa kujenga vituo maalum vitakavyosaidia kutoa elimu ya ufundi na majiundo makini kwa watoto na vijana. Ili kuhamasisha uelewa makini wa huduma zinazotolewa na Caritas, kuna haja ya kuanzisha Siku ya Caritas Kiparokia. Taasisi inayoratibu huduma za afya zinazotolewa na Kanisa Katoliki nchini Rwanda, imewapongeza wajumbe wa Caritas Rwanda kwa mchango na huduma wanayotoa kwa wananchi wa Rwanda. Caritas Rwanda imealikwa pia kushiriki katika mkutano mkuu wa Taasisi hii utakaofanyika tarehe 14 Machi 2013.

Askari polisi na jambazi wauawa katika mapigano Mkwajuni Chunya

Na Thompson Mpanji,Chunya

ASKARI Polisi wa kituo kidogo cha Polisi Mkwajuni wilayani Chunya, G.68.PC Jaffari Karume Mohamed (30), amefariki dunia  wakati akipatiwa matibabu  katika Hospitali Teule ya Mwambani,wilayani humo  baada ya kupigwa risasi katika majibizano ya risasi na majambazi.

Imeelezwa kuwa tukio limetokea jana  februari,6 majira ya  saa 6 usiku ,jirani na klabu ya pombe cha Mwaulambo,Mwambani Klabu,wilayani Chunya baada ya majambazi hayo kudaiwa kufanya uharifu katika maeneo tofauti na kufanikiwa kupora zaidi ya Sh.Mil.2.2 katika  kituo cha mafuta cha mfanyabiashara aliyetajwa kwa jina la Samora Muyombe walielekea Mkwajuni  wakiwa na  gari  aina ya Toyota Colora yenye nambari za usajili T.227 BST iliyokuwa ikiendeshwa na Shaban Msule(33),Mbena,Mkazi wa makambakoLand Cruiser.

Walisema majambazi hayo yalipita maeneo ya Makongolosi na Saza  wakijaribu kupora bila mafanikio  na hatimaye kufika Mkwajuni marehemu Jaffari akiwa doria na askari wenzake  waliokuwa wakifuatilia tukio hilo baada ya kupokea taarifa  walifanikiwa kuwakuta vna kupambana nao na ndipo alipojeruhiwa  kwa kupigwa risasi  ubavu wa kulia  na kukimbizwa Hospitali  ambapo alifariki dunia akiwa anapatiwa matibabu.
 
Walisema  baada ya polisi wa kituo cha Mkwajuni kupata taarifa hiyo waliweka mtego na kufanikiwa kuliona gari likipita jirani na kituo  na baada ya kuwafuatilia walilikuta gari hilo limepaki jirani na klabu hiyo huku Dereva wa gari hilo akishuka kwenda kununua maji ya kunywa na ndipo mkuu wa kituo aliyefahamika kwa jina moja la Dominiki akiwa amevalia kiraia alimfuatilia lakini kabla ya kumfikia dereva huyo Askari polisi jaffari alishuka akiwa na bunduki na majambazi kumshtukia na kummiminia risasi.

Walisema polisi nao walijibu mashambulizi na kufanikiwa kumuuwa jambazi  dereva Msule ambapo wengine  watatu walifanikiwa kutoroka kwa miguu na kuliacha gari ambalo lipo katika kituo cha polisi Mkwajuni.

Kaimu Kamanda wa polisi Mkoa wa Mbeya,Mrakibu Mwandamizi wa polisi  Barakael Masaki amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kudaiwa kuwa gari hilo limekamatwa lipo kituo cha polisi mkwajuni na mwili wa marehemu umehifadhiwa katika Hospitali Teule ya Wilaya ya Chunya ya Mwambani,Kata ya Mkwajuni ukisubiri taratibu nyingine za maziko ya kijeshi.

Kamanda Msaki alisema  wamefanikiwa  kukamata maganda  tisa  ya risasi aina ya SMG na SAR  pamoja na risasi sita  na kwamba msako mkali unaendelea  chini ya uongozi wa Mkuu wa upelelezi wa makosa ya jinai Mkoa wa Mbeya Robert Mayala (SSP),askari polisi na wananchi ili kuwabaini  na kuwakamata watuhumiwa waliohusika na tukio hilo.

Hata hivyo Kaimu Kamnada huyo ametoa wito kwa mtu ama watu  wenye taarifa  kuhusu  mahali walipo watu wanaodhaniwa kuhusika  na tukio hilo watoe taarifa  ili wakamatwe  na sheria iweze kuchukuwa mkondo wake vinginevyo wajisalimishe.

Sunday, February 3, 2013

'Kanumba' aibukia Mbeya,adai baba alimkataa akiwa tumboni Shinyanga



Na  Thompson Mpanji,Mbeya

KIJANA anayedai kuwa ni mdogo wa msanii maarufu wa Bongo Movie  marehemu ‘The Great’Steven Kanumba  aliyejitambulisha kwa jina la Lameck Ngogo(20),Mkazi Sokomatola,jijini Mbeya ameibuka na kudai kuwa marehemu Kanumba ni Kaka yake  aliyezaliwa naye kwa Baba   lakini Mama tofauti.

‘Kanumba’ mdogo huyo ameibuka  asubuhi  ya  Januari,3,2013 katika mkutano wa waandishi wa habari na  viongozi na wanachama wa Chama cha NCCR waliofukuzwa kutoka Chama cha Demokrasia na maendeleo (CHADEMA),jijini Mbeya katika ukumbi wa Baa ya Double J,Sinde.

Ilikuwa kama ‘movie’ baada ya kijana huyo mwenye uso wa upole,tabasamu kama la marehemu Kanumba alipoingia na mwandishi wa habari wa kujitegemea,Samwel Mamba,Mkazi wa wilayani Mbozi  na kutulia kama msikilizaji ama naye Mwanahabari lakini macho ya wanahabari wengi yaligonga na kutuwa katika sura yake  huku wakiwa na maswali mengi ya kujiuliza wakisubiri mkutano huo umalizike mapema na kuanza kumhoji mwandishi Samwel kulikoni kijana huyo.

Mara baada ya kumalizika kwa kikao hicho Samwel huku akiwa ameshabaini kiu ya wanahabari alianza kwa kusema,”jamani nimewaletea mdogo wake kanumba…,nimemuibua kutoka katika guest ya Eden iliyopo maeneo ya uhindini jijini Mbeya ndiko anakofanyakazi.”

Aliendelea kwa kusema,” mimi sina la kuongea zaidi  ya kumsikiliza yeye asimulie historia yake maana mimi nililala katika nyumba hiyo ya kulala wageni leo(januari,3) na baada ya kumuona nilishtuka sana nilipomwita na kumuuliza alinielezea historia yake iliyonisababisha kumuombea ruhusa kwa wakubwa wake ili nije naye hapa leo nikijuwa tutakutana waandishi katika press conference hii.”

Kijana lameck hauwezi kumsingizia   kwa zile hulka za marehemu Star wa Bongo Movie Steve Kanumba ambapo alianza kusimulia historia  yake kuwa yeye ni mtoto  wa kwanza wa Mama yake Alatwingisya Ngogo na kwamba hilo jina analolitumia  la Ngogo ni la Babu yake mzaa mama yake.

Alisema Mama yake  ni mkazi wa Uwanji,Kata ya Mlondo,Wilaya ya Makete mkoani Njombe na kwamba aliwahi kuchukuliwa na Mama yake Mkubwa aliyemtaja kwa jina moja la Jane(Dada yake) na kuishi naye mkoani Shinyanga miaka 20 iliyopita ambapo  alibahatika kupata  uja uzito wa yeye(Lameck) na kutokana na Mama yake mkubwa kuchukia hali hiyo aliamua kumfukuza na kumrejesha nyumbani uwanji anapoishi hadi leo.

Lameck alisema kuwa Mama yake mkubwa huyo ambaye anaishi hadi leo mkoani Shinyanga hakumuuliza Mama yake kuwa mimba hiyo alipewa na nani zaidi ya kumrudisha nyumbani hadi alipojifungua na kuendelea na maisha hadi alipokuja kuolewa  na kuendelea kuishi  na Mume wake  hadi leo.

“Lakini nilipokuwa nikiendelea kukua na kupata ufahamu watu walikuwa wakiniambia kuwa huyo siyo Baba yangu mzazi licha ya mama kunieleza kuwa ndiyo baba yangu mzazi lakini baada ya kumdadisi sana  aliamua kunieleza kuwa ni kweli baba yangu alinikataa tangu nikiwa tumboni huko Shinyanga ambaye ni Baba yake msanii kanumba kabla hajafa,”alisema.

“Baadaye nililelewa na Bibi yangu anaitwa Nilang’ilwa na niliendelea na masomo na kuishia kidato cha pili katika shule ya Sekondari ya Mlondwe  na hivyo nikaja kwa Mjomba wangu Uyole kumsaidia kuuza viatu vya mitumba na baadaye nikatafuta kazi nikapata   katika nyumba ya kulala wageni ya Eden iliyopo Uhindini  ambako huyu Mwandishi alinikuta na kunihoji baada ya mimi kumuona amebeba mabegi ya camera na kuanza kumsimulia historia yangu hii,”alisema.

Aidha Lameck alisema aprili,mwaka 2011 alitafuta nauli na kwenda kumtafuta Baba yake  na alifikia kwa Mama yake mkubwa Jane  huku akifanyakazi katika Gereji  moja  inayoitwa kwa Remmy Shinyanga ambapo alifika katika nyumba ya baba yake na hakufanikiwa kumpata lakini alipata nambari yake ya simu  na kumpigia akijitambulisha lakini mzee huyo alimkataa katu katu kwa mara ya pili ambapo awali kwa mujibu ya maelezo ya mama yake kuwa aliikataa  mimba.

“Ninajuwa mzee anayo haki ya kukataa kwa sababu hajaniona ama hatujaenda kupima DNA kama kweli mimi ni mwanawe ama hapana,mwezi Disemba nilirudi Mbeya  ambavyo kama nilivyosimulia nilipo sasa  na   baada ya kumweleza mama alinisihi niache kumtafuta baba zaidi niangalie maisha yangu,nimekata tamaa na sasa nahangahika na maisha yangu,”alisema kwa majonzi Lameck.

Alipoulizwa  kuwa baada ya kusikia kifo cha kaka yake Kanumba  alikipokea vipi na kama aliwahi kwenda  katika msiba huo,alitikisa mabega kukataa kutokana na kukata tamaa ya kukataliwa na Baba yake,na hakuwa na nauli ya kwenda huko,lakini ameahidi kuwa ipo siku atakwenda moja kwa moja kwa baba yake akamkatae  ana kwa ana,hivyo anatafuta nauli.

Hata hivyo kijana huyo alisema yeye anakipaji cha kutunga  tamthiliya  na hadithi na kwamba aliwahi kwenda kujiunga katika kikundi kimoja cha kuigiza kilichopo pembeni kidogo mwa Jiji la Mbeya,katika mji mdogo wa Mbalizi kinachoongozwa na mtu aliyefahamika kwa jina la Mzushi lakini alikwama kutokana na kushindwa kulipa hela ya kiingilio Sh.250,000 lakini ndoto yake  amedai iko pale pale  ya kurithi  kipaji cha kaka yake  The Great Kanumba.

Mwisho.