Translate

Wednesday, February 6, 2013

Askari polisi na jambazi wauawa katika mapigano Mkwajuni Chunya

Na Thompson Mpanji,Chunya

ASKARI Polisi wa kituo kidogo cha Polisi Mkwajuni wilayani Chunya, G.68.PC Jaffari Karume Mohamed (30), amefariki dunia  wakati akipatiwa matibabu  katika Hospitali Teule ya Mwambani,wilayani humo  baada ya kupigwa risasi katika majibizano ya risasi na majambazi.

Imeelezwa kuwa tukio limetokea jana  februari,6 majira ya  saa 6 usiku ,jirani na klabu ya pombe cha Mwaulambo,Mwambani Klabu,wilayani Chunya baada ya majambazi hayo kudaiwa kufanya uharifu katika maeneo tofauti na kufanikiwa kupora zaidi ya Sh.Mil.2.2 katika  kituo cha mafuta cha mfanyabiashara aliyetajwa kwa jina la Samora Muyombe walielekea Mkwajuni  wakiwa na  gari  aina ya Toyota Colora yenye nambari za usajili T.227 BST iliyokuwa ikiendeshwa na Shaban Msule(33),Mbena,Mkazi wa makambakoLand Cruiser.

Walisema majambazi hayo yalipita maeneo ya Makongolosi na Saza  wakijaribu kupora bila mafanikio  na hatimaye kufika Mkwajuni marehemu Jaffari akiwa doria na askari wenzake  waliokuwa wakifuatilia tukio hilo baada ya kupokea taarifa  walifanikiwa kuwakuta vna kupambana nao na ndipo alipojeruhiwa  kwa kupigwa risasi  ubavu wa kulia  na kukimbizwa Hospitali  ambapo alifariki dunia akiwa anapatiwa matibabu.
 
Walisema  baada ya polisi wa kituo cha Mkwajuni kupata taarifa hiyo waliweka mtego na kufanikiwa kuliona gari likipita jirani na kituo  na baada ya kuwafuatilia walilikuta gari hilo limepaki jirani na klabu hiyo huku Dereva wa gari hilo akishuka kwenda kununua maji ya kunywa na ndipo mkuu wa kituo aliyefahamika kwa jina moja la Dominiki akiwa amevalia kiraia alimfuatilia lakini kabla ya kumfikia dereva huyo Askari polisi jaffari alishuka akiwa na bunduki na majambazi kumshtukia na kummiminia risasi.

Walisema polisi nao walijibu mashambulizi na kufanikiwa kumuuwa jambazi  dereva Msule ambapo wengine  watatu walifanikiwa kutoroka kwa miguu na kuliacha gari ambalo lipo katika kituo cha polisi Mkwajuni.

Kaimu Kamanda wa polisi Mkoa wa Mbeya,Mrakibu Mwandamizi wa polisi  Barakael Masaki amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kudaiwa kuwa gari hilo limekamatwa lipo kituo cha polisi mkwajuni na mwili wa marehemu umehifadhiwa katika Hospitali Teule ya Wilaya ya Chunya ya Mwambani,Kata ya Mkwajuni ukisubiri taratibu nyingine za maziko ya kijeshi.

Kamanda Msaki alisema  wamefanikiwa  kukamata maganda  tisa  ya risasi aina ya SMG na SAR  pamoja na risasi sita  na kwamba msako mkali unaendelea  chini ya uongozi wa Mkuu wa upelelezi wa makosa ya jinai Mkoa wa Mbeya Robert Mayala (SSP),askari polisi na wananchi ili kuwabaini  na kuwakamata watuhumiwa waliohusika na tukio hilo.

Hata hivyo Kaimu Kamnada huyo ametoa wito kwa mtu ama watu  wenye taarifa  kuhusu  mahali walipo watu wanaodhaniwa kuhusika  na tukio hilo watoe taarifa  ili wakamatwe  na sheria iweze kuchukuwa mkondo wake vinginevyo wajisalimishe.

No comments:

Post a Comment