Translate

Sunday, September 15, 2013

WAWILI WAUAWA MBEYA KWA KUHUSISHWA NA WIVU WA MAPENZI



TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI
“PRESS RELEASE” TAREHE 15. 09. 2013.





WILAYA YA MBEYA MJINI – MAUAJI

MNAMO TAREHE 15/09/2013 MAJIRA YA SAA 01:00HRS HUKO ITUHA JIJINI MBEYA WATU WAWILI MMOJA ALIYETAMBULIKA KWA JINA MOJA LA SOPHIA ANAYEKADIRIWA KUWA NA UMRI KATI MIAKA 35 – 40, MSAFWA, MKULIMA NA MKAZI WA ITUHA, PAMOJA NA MTU MMOJA MWANAUME AMBAYE HAJATAMBULIWA, ANAYEKADIRIWA KUWA NA UMRI KATI YA MIAKA 40 – 45 WALIFARIKI DUNIA WAKATI WAKIWA NJIANI KUPELEKWA HOSPITALI BAADA YA KUSHAMBULIWA KWA KUPIGWA MAWE NA MARUNGU SEHEMU MBALIMBALI ZA MIILI YAO NA MTU/WATU WASIOFAHAMIKA. MBINU ILIYOTUMIKA NI KUWAVAMIA WAKIWA NJIANI WAKIREJEA NYUMBANI USIKU. CHANZO CHA MAUAJI HAYO KINAHUSISHWA NA WIVU WA KIMAPENZI,HADI SASA MTU MMOJA  AITWAE  ZEBEDAYO S/O JOHN, MIAKA 32, MSAFWA, MKULIMA NA MKAZI WA ITUHA AMEKAMATWA KWA KUTILIWA MASHAKA KUHUSIKA NA TUKIO HILO NA UPELELEZI UNAENDELEA. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI ANATOA WITO KWA JAMII KUACHA TABIA YA  KUJICHUKULIA SHERIA MKONONI BADALA YAKE WATUMIE NJIA YA  MAZUNGUMZO KUMALIZA MIGOGORO YAO. PIA ANATOA RAI KWA WANANCHI/YEYOTE MWENYE TAARIFA JUU YA WALIKO WAHUSIKA WA TUKIO HILO WAZITOE ILI WAKAMATWE NA SHERIA ICHUKUE MKONDO WAKE.          



WILAYA YA CHUNYA – KUPATIKANA NA POMBE YA MOSHI {GONGO}



MNAMO TAREHE 14.09.2013 MAJIRA YA SAA 14:20HRS HUKO KITONGOJI CHA KISUNGU KIJIJI CHA UPENDO KATA YA   MAMBA WILAYA YA CHUNYA MKOANI MBEYA ASKARI POLISI WAKIWA KATIKA MSAKO WALIMKAMATA FELISTA D/O ROMAN, MIAKA 36, MNYAMWANGA, MKULIMA NA MKAZI WA KIIJIJI CHA KISUNGU AKIWA NA POMBE YA MOSHI [GONGO] LITA 12 KATIKA DUMU LA LITA 20, MBINU ILIYOTUMIKA NI KUIFICHA NDANI YA NYUMBA YAKE. MTUHUMIWA NI MUUZAJI NA MTUMIAJI WA POMBE HIYO.    MTUHUMIWA AMEKAMATWA NA TARATIBU ZINAFANYWA ILI AFIKISHWE MAHAKAMANI.  KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI  ANATOA WITO KWA JAMII  KUACHA MARA MOJA TABIA YA  KUTUMIA POMBE HARAMU YA  MOSHI KWANI NI HATARI KWA AFYA YA  MTUMIAJI NA NI KINYUME CHA SHERIA .



 [DIWANI ATHUMANI   - ACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.

MHE. DIWANI KATA YA KIWIRA AKAMATWA KWA DIWANI WA CHADEMA RUNGWE MBARONI KWA TUHUMA ZA KUFANYA MAPENZI NA MWANAFUNZI.



TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI
“PRESS RELEASE” TAREHE 14. 09. 2013.


WILAYA YA  RUNGWE  – MHE.  DIWANI KATA YA  KIWIRA AKAMATWA KWA
                                           TUHUMA ZA KUFANYA MAPENZI NA MWANAFUNZI.



§         MNAMO TAREHE 12.09.2013 MAJIRA YA  SAA 19:30HRS  HUKO KATIKA KITONGOJI CHA KIBUMBE  KATA YA   KIWIRA – TUKUYU  WILAYA YA   RUNGWE MKOA WA MBEYA,  RAPHAEL S/O FRANK, MIAKA 42, KYUSA, MKULIMA NA MKE WAKE SUZANA W/O FRANK, MIAKA 38, KYUSA,  MKULIMA WOTE WAKAZI WA KIBUMBE KIWIRA – TUKUYU  WAKIWA NYUMBANI KWAO WALIGUNDUA KUTOWEKA KATIKA MAZINGIRA YA  KUTATANISHA KWA MTOTO WAO AGNES D/O RAPHAEL, MIAKA 18, KYUSA, MWANAFUNZI KIDATO CHA NNE SHULE YA  SEKONDARI KIWIRA HIVYO JITIHADA ZA KUMTAFUTA ZILIANZA MARA MOJA  USIKU KUCHA BILA MAFANIKIO.

§          MNAMO TAREHE 13.09.2013 MAJIRA YA  SAA 06:00HRS WAZAZI HAO BAADA YA  KUONA MTOTO WAO HAKULALA NDANI KAMA ILIVYO KAWAIDA WALIAMUA KWENDA KATIKA KITUO CHA POLISI KIWIRA NA KUTOA TAARIFA YA  KUPOTELEWA  NA MTOTO.  HATA HIVYO MAJIRA YA  SAA 09:00HRS MTOTO WAO AGNES D/O RAPHAEL ALIRUDI NYUMBANI NA WAZAZI WAKE WALIPOMHOJI JUU YA  MAHALI ALIPOKUWA ALIWAJIBU KUWA   ALIKUWA NA MHE  DIWANI WA KATA YA  KIWIRA [CHADEMA]  LAURENT S/O MWAKALIBULE, MIAKA 28, KYUSA, MKAZI WA KIWIRA – KATI NA KWAMBA WALILALA KATIKA NYUMBA YA  MDOGO WAKE NA DIWANI HUYO AMBAYE JINA LAKE BADO KUFAHAMIKA NA KUWA KABLA YA  KUKUTANA WALIWASILIANA KWA NJIA YA  SIMU YA  KIGANJANI.

§         MTUHUMIWA AMEKAMATWA, UPELELEZI WA SHAURI HILI UNAENDELEA .


§         KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI  ANATOA WITO KWA JAMII  HASA WANAFUNZI KUJIEPUSHA NA MADHARA YA  KUFANYA MAPENZI [NGONO] KWANI NI HATARI KWA  AFYA ZAO NA PIA KWA MAISHA YAO YA  BAADAE BADALA YAKE WAZINGATIE ZAIDI  MASOMO KWA FAIDA YAO , VIZAZI VYAO NA TAIFA KWA UJUMLA..




 [DIWANI ATHUMANI   - ACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.

Maiti ya kichanga yatupwa Rungwe




TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI
PRESS RELEASE” TAREHE 11. 09. 2013.


        WILAYA YA  RUNGWE  - KUTUPA MTOTO MCHANGA.
MNAMO TAREHE 10.09.2013 MAJIRA YA  SAA 14:00HRS HUKO KATIKA MTAA WA BAGAMOYO – TUKUYU MJINI WILAYA YA  RUNGWE   MKOA WA  MBEYA. ILIOKOTWA MAITI YA  MTOTO MCHANGA MWENYE UMRI WA SIKU MOJA JINSI YA  KIKE IKIWA IMETELEKEZWA NA MAMA MZAZI  WA MTOTO HUYO AMBAYE BADO HAJAFAHAMIKA. MWILI WA MAREHEMU AMBAO UMEHIFADHIWA KATIKA HOSPITALI YA  SERIKALI YA  MAKANDANA – TUKUYU ULIKUTWA NYUMA YA  KISIMA CHA MAFUTA CHA CALTEX UKIWA UMEVINGIRISHWA KWA KUTUMIA KIPANDE CHA KITENGE KISHA KUWEKWA NDANI YA  MFUKO WA RAMBO NA JUU YAKE KUWEKWA JIWE. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA  KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI  ANATOA WITO  KWA YEYOTE MWENYE TAARIFA JUU YA  MAHALI ALIPO MTUHUMIWA ALIYEFANYA KITENDO HIKI CHA KIKATILI NA CHA KINYAMA AZITOE KATIKA MAMLAKA HUSIKA ILI AKAMATWE NA SHERIA ICHUKUE MKONDO WAKE,VINGINEVYO AJISALIMISHE MWENYEWE MARA MOJA.


.
                                                                 Imesainiwa na
 [ DIWANI ATHUMANI  - ACP ]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.


Monday, September 9, 2013

auawa Mbeya kwa kuiba Bambucha

TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI
PRESS RELEASE” TAREHE 09. 09. 2013.
 
 
WILAYA YA  MBEYA MJINI  - MAUAJI.
 
MNAMO TAREHE 08.09.2013 MAJIRA YA  SAA 14:15HRS HUKO KATIKA HOSPITALI YA  RUFAA MBEYA JIJI NA MKOA WA MBEYA. MUSA S/O MBUKWA, MIAKA 30, MFIPA, MKULIMA, MKAZI WA NSALAGA – UYOLE ALIFARIKI DUNIA WAKATI AKIENDELEA KUPATIWA MATIBABU HOSPITALINI HAPO BAADA YA  KUJERUHIWA KWA KUPIGWA NA KUNDI LA WANANCHI WALIOAMUA KUJICHUKULIA SHERIA MKONONI TAREHE 08.09.2013 SAA 10:00HRS  KWA TUHUMA ZA WIZI WA BAISKELI AINA YA  BAMBUCHA YENYE THAMANI YA  TSHS 125,000/= MALI YA CHRISTOPHER S/O MWAITEGE, MIAKA 39, MSAFWA, MKULIMA, MKAZI WA GOMBE. MBINU NI KUMSHAMBULIA MAREHEMU  KWA KUTUMIA SILAHA ZA JADI MAWE NA FIMBO SEHEMU MBALIMBALI ZA MWILI WAKE WAKATI AKIWA NJIANI ANAPELEKWA KITUO CHA POLISI. MWILI WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA HOSPITALINI HAPO. JITIHADA ZA KUWABAINI NA KUWAKAMATA WALIOHUSIKA NA TUKIO HILI ZINAENDELEA. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA  KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI  ANAENDELEA KUTOA WITO  KWA JAMII KUACHA TABIA YA  KUJICHUKULIA SHERIA MKONONI KWANI NI KINYUME CHA SHERIA BADALA YAKE WAWAFIKISHE KATIKA MAMLAKA HUSIKA WATUHUMIWA WANOWAKAMATA KWA TUHUMA MBALIMBALI ILI HATUA ZA KISHERIA DHIDI YAO ZICHUKULIWE.
 
 
WILAYA YA  MBARALI – KUPATIKANA NA BHANGI.
 
MNAMO TAREHE 08.09.2013 MAJIRA YA  SAA 12:45HRS HUKO ENEO LA MKONGWE – UBARUKU WILAYA YA  MBARALI MKOA WA MBEYA. ASKARI POLISI WAKIWA DORIA WALIWAKAMATA 1. MODESTUS S/O MKOLA, MIAKA 24, MBENA,MKULIMA 2. ALEX S/O MALONGO, MIAKA 19, MBENA, MKULIMA, 3. BENI S/O MWAIPWAPWA, MIAKA 29, MKINGA 4.TIMO S/O MAJI YA  PWANI, MIAKA 29, MKINGA WOTE WAKAZI WA UBARUKU WAKIWA NA BHANGI UZITO WA GRAM 29. WATUHUMIWA NI WAVUTAJI WA BHANGI. TARATIBU ZINAFANYWA ILI WAFIKISHWE MAHAKAMANI. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA  KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI  ANAENDELEA KUTOA WITO  KWA JAMII KUACHA MATUMIZI YA DAWA ZA KULEVYA KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NA NI HATARI KWA AFYA YA MTUMIAJI.
 
 
Imesainiwa na:
[ DIWANI ATHUMANI  - ACP ]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
 

Sunday, September 8, 2013

MATUKIO KATIKA PICHA TAMASHA LA TGNP

TAMASHA LA MIAKA 20 YA TGNP



TGNP WANAWAKE WAITAKA KATIKA KUWEKA BAYANA MASUALA YA WANAWAKE



Na Thompson Mpanji,Dar

WANAWAKE nchini wameendelea kupataza sauti zao  kwa tume ya Katiba kuwekwa wazi na kutamka bayana masuala yanayohusu wanawake katika rasimu ya katiba  mpya ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ikiwemo  katika eneo la Tunu za Taifa  kwa kuongeza neno   Usawa wa jinsia.

Hayo yamesemwa  na mwezeshaji katika jukwaa la Katiba Ruth Meena   katika viwanja vya makao makuu ya Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP),Mabibo,jijini hapa wakati wa maadhimisho ya Tamasha la miaka  20 ya shirika hilo tangu kuanzishwa.

Meena amesema  katika Katiba mpya inayotarajiwa kuundwa ni muhimu kutoa kipaumbele na kuingizwa kmasuala ya wanawake   ambayo hayataleta mkanganyiko kwa namna yeyote ili mambo ya msingi yaendelea kuchukuliwa uzito. 

Mwezeshaji huyo amesema usawa wa jinsia lazima utiririke  katika katiba yote   kwani  ndiyo msingi mkuu huku akidai haki za wanawake  lazima zibainishwe kwa uwazi,haki za mtoto hasa wa kike ziwekwe bayana kwani  wanafahamu  muktadha wa jamii  katika  kumbagua mtoto wa kike.

Meena alisema mila na desturi  zinazokinzana   na wanawake  zibatilishe na katiba mpya iseme kwa uwazi,miiko watakayopewa viongozi watakawaongoza  ioneshe  kupinga ukatili  sanjari na vyama vya siasa  kupewa mipaka  katika kampeni kuhusu matumizi ya pesa ili nchi isije kuongozwa na  fedha chafu.

Awali kabla ya kuanza kwa mjadala wa  jukwaa la katiba ,vijana kutoka jukwaa la wanaharakati wanawake (WFF) kutoka  TGNP walitumbuiza kwa ngonjera  huku baadhi ya  washiriki wakishangilia  ubeti mmoja uliowavuita  wengi.

Akianzisha ubeti huo mmoja wa wanaharakati hao,Aisha Kijawala aliuliza  machangudoa wateja wake nani ambapo wenzake walijibu kuwa ni Mawaziri,Wabunge,Mapolisi  na wengine wengi ubeti uliowainua washiriki wote katika tamasha hilo la TGNP huku wakiwatuza fedha.

Mwisho.


Chadema walonga maisha ya wanachunya



LICHA ya kuwa na utajiri mkubwa wa madini ya Dhahabu katika Wilaya ya Chunya Mkoani Mbeya, bado wananchi na wakazi wa wilaya hiyo wanaendelea kuteseka kwa ukosefu wa maji safi na salama.

Tatizo la maji limeshindwa kupatiwa ufumbuzi  katika Wilaya hiyo kwa muda mrefu sasa ambapo wadau mbali mbali wameshauri Serikali kufanya kama ilivyofanya Mkoani Shinyanga kuchukua maji Ziwa Victoria kilomita zaidi ya 700.

Wamesema Wilaya ya Chunya ina Ziwa Rukwa ambalo lingeweza kusaidia kujenga mradi wa maji na kuwaondolea adha wananchi wa Chunya ziwa ambalo liko umbali usiozidi kilomita 50 hivyo kupunguza gharama kama zilizotokea Mkoani Shinyanga.

Ushauri huo ulitolewa jana na Katibu Mwenezi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Lukasi Mwampiki, alipokuwa akihutubia wananchi wa Kijiji cha Saza Wilayani Chunya katika ziara ya kuimarishja chama inayoendelea Wilayani humo.

Alisema katika kijiji cha Saza ambacho kwa miaka hamsini tangu uhuru hawajawahi  kupata huduma za maji safi na salama licha ya kuwepo kwa mgodi mkubwa wa madini ya dhahabu inayochimbwa na wawekezaji wa nje.

Alisema kukosekana kwa Maji katika Wilaya hiyo ni aibu kubwa na inaonesha dhahiri Mwekezaji kutowajali wananchi ambapo pia hawanufaiki na uchimbaji huo ambao umeshindwa kuwatatulia tatizo sugu la maji linalowakabili wananchi hao kwa muda mrefu.

Mwampiki alisema Serikali inaweza ikatumia njia rahisi kama ilivyofanyika Mkoani Shinyanga ambako tatizo la maji limetatutiliwa kwa kuchukuliwa maji katika Ziwa Viktoria lililo umbali wa zaidi ya Kilomita 700 ili hali ziwa Rukwa likiwa jirani kabisa na Wakazi wa Chunya ambao wanaweza kusahau kabisa shida ya maji.

Alisema maji ya Ziwa Rukwa yakichukuliwa  yataondoa gharama na adha wanayoipata Wananchi kwa kusafiri umbali mrefu kutafuta maji huku wakishindwa kufanya shughuli zingine za maendeleo hususani wanafunzi ambao hushindwa kuhudhuria masomo ambapo bado maji yanayopatikana kutofaa kwa matumizi ya binadamu.

Aliongeza kuwa wananchi walitakiwa kushirikishwa kabla ya mwekezaji hajaanza uchimbaji wa madini ili apewe vipaumbele vitakavyo wanufaisha moja kwa moja likiwemo tatizo sugu la maji ambalo alitakiwa alitatue kabla ya kazi yoyote.

Aidha katika hatua nyingine Mwampiki aliwashauri wananchi wa Kijiji cha Saza kuwahoji Madiwani wao kuhusu hati chafu zinazotolewa na Mkaguzi wa Hesabu za Serikali(CAG) kwa Halmashauri na wao kuziangali tu na kukosesha sifa Halmashauri kwa matumizi mabaya ya fedha za wananchi.

Mwisho.

wawili wafariki kwa ajali Mbeya mjini na Rungwe,Dereva wa Hiace asakwa baada ya kusababisha kifo na kukimbia



TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI
 “PRESS RELEASE” TAREHE   07. 09. 2013.


WILAYA YA RUNGWE – AJALI YA GARI KUMGONGA MPANDA PIKIPIKI NA      
                                                KUSABABISHA KIFO.

MNAMO TAREHE 06.09.2013 MAJIRA YA SAA 17:00HRS HUKO ISYONJE BARABARA YA MBEYA/TUKUYU WILAYA YA RUNGWE MKOA WA MBEYA. GARI NO T.906 AJK T/HIACE LIKIENDESHWA NA DEREVA ASIYEFAHAMIKA LILIMGONGA MPANDA PIKIPIKI NO T.215 CMM BOXER ILIYOKUWA IKIENDESHWA NA EMMANUEL S/O MGIMWA, MIAKA 59, MHEHE, AFISA KILIMO WA IDWELI NA KUSABABISHA KIFO CHAKE PAPO HAPO. CHANZO CHA AJALI NI DEREVA WA HIACE KUTAKA KULIPITA GARI LA MBELE YAKE BILA KUCHUKUA TAHADHARI. DEREVA ALIKIMBIA NA GARI MARA BAADA YA TUKIO HILO JUHUDI ZA KUMTAFUTA ZINAENDELEA. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI ANATOA WITO KWA MADEREVA KUWA MAKINI WANAPOTUMIA VYOMBO VYA MOTO KWA KUZINGATIA SHERIA ZA USALAMA BARABARANI ILI KUEPUSHA AJALI ZINAZOWEZA KUEPUKIKA. AIDHA ANATOA RAI KWA YEYOTE MWENYE TAARIFA JUU YA  MAHALI ALIPO MTUHUMIWA AZITOE KATIKA MAMLAKA HUSIKA ILI AKAMATWE NA SHERIA ICHUKUE MKONDO WAKE, VINGINEVYO AJISALIMISHE.


WILAYA YA MBEYA MJINI – AJALI YA GARI KUMGONGA MTEMBEA KWA
                                                         MIGUU NA       KUSABABISHA KIFO.

MNAMO TAREHE 06.09.2013 MAJIRA YA SAA 06:10HRS HUKO ISANGA BARABARA YA MBEYA/CHUNYA GARI NO. T.156 AHN SCANIA BUS LIKIENDESHWA NA DEREVA BARAKA S/O MGALULA, MIAKA 37, MSUKUMA NA MKAZI WA TABORA LILIMGONGA MTEMBEA KWA MIGUU AITWAYE KANUNU S/O PENJA, MIAKA 75, MNYAKYUSA NA MKAZI WA ISANGA NA KUSABABISHA KIFO CHAKE PAPO HAPO. CHANZO CHA AJALI NI MWENDO KASI. MWILI WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA KATIKA HOSPITALI YA RUFAA MBEYA.  DEREVA AMEKAMATWA NA GARI LIPO KITUONI. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI  ANATOA WITO KWA MADEREVA KUWA MAKINI WANAPOTUMIA VYOMBO VYA MOTO KWA KUZINGATIA SHERIA ZA USALAMA BARABARANI ILI KUEPUSHA AJALI ZINAZOWEZA KUEPUKIKA.


Signed by:

[DIWANI ATHUMANI - ACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA

Tuesday, September 3, 2013

watano wafariki dunia Mbeya




TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI
“PRESS RELEASE” TAREHE   30. 08. 2013.



WILAYA YA  MBARALI – AJALI YA  GARI KUMGONGA MTEMBEA KWA MIGUU
                                             NA   KUSABABISHA KIFO
.

MNAMO TAREHE 29.08.2013 MAJIRA YA  SAA 18:30HRS HUKO KATIKA KJIJI CHA MWAPIMBUKA  BARABARA YA  MBEYA/IRINGA WILAYA YA  MBARALI MKOA WA MBEYA. GARI T.877 CLX/T.242 CLV AINA YA  IVECO LIKIENDESHWA NA HABIBU S/O HASSAN, MIAKA 28, MLUGURU, MKAZI WA BUGURUNI DSM, LILIMGONGA MTEMBEA KWA MIGUU MTOTO PASTO D/O FURAHA, MIAKA 11, MNYIHA,MWANAFUNZI S/MSINGI IGURUSI DARASA LA PILI MKAZI WA KIJIJI CHA MWAPIMBUKA NA KUSABABISHA KIFO CHA CHAKE WAKATI ANAENDELEA KUPATIWA MATIBABU KATIKA KITUO CHA AFYA IGURUSI. MWILI WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA KATIKA KITUO HICHO CHA AFYA. CHANZO MWENDO KASI. MTUHUMIWA ALIKIMBIA NA KULITELEKEZA GARI  ENEO LA TUKIO MARA  BAADA YA   AJALI. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI ANATOA WITO KWA MADEREVA KUWA MAKINI WANAPOTUMIA VYOMBO VYA MOTO KWA KUZINGATIA SHERIA ZA USALAMA BARABARANI ILI KUEPUSHA AJALI ZINAZOWEZA KUEPUKIKA. AIDHA ANATOA RAI KWA YEYOTE MWENYE TAARIFA JUU YA  MAHALI ALIPO MTUHUMIWA AZITOE KATIKA MAMLAKA HUSIKA ILI AKAMATWE NA SHERIA ICHUKUE MKONDO WAKE, VINGINEVYO AJISALIMISHE MARA MOJA.


WILAYA YA  MBARALI – KUPATIKANA NA POMBE HARAMU YA  MOSHI
                                             [GONGO] NA   MTAMBO WA KUTENGENEZEA POMBE.


MNAMO TAREHE 29.08.2013 MAJIRA YA  SAA 08:00HRS HUKO RUJEWA MJINI WILAYA YA  MBARALI MKOA WA MBEYA. ASKARI POLISI WAKIWA KATIKA DORIA/MSAKO WALIMKAMATA EZEKIEL S/O JAKOBO, MIAKA 26, MBENA,MKULIMA MKAZI WA UHAVILA NA WENZAKE SITA WAKIWA NA POMBE HARAMU YA  MOSHI [GONGO] UJAZO WA LITA 25 PAMOJA NA MTAMBO MMOJA WA KUTENGENEZEA POMBE HIYO. WATUHUMIWA NI WATUMIAJI NA WAUZAJI WA POMBE HIYO. TARATIBU ZINAFANYWA ILI WAFIKISHWE MAHAKAMANI.  KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI ANATOA WITO KWA JAMII KUACHA KUTUMIA POMBE HARAMU YA  MOSHI[GONGO] KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NA NI HATARI KWA AFYA YA  MTUMIAJI.



WILAYA YA  MBARALI – AJALI YA  GARI KUMGONGA MTEMBEA KWA MIGUU
                                             NA   KUSABABISHA KIFO
.

MNAMO TAREHE 29.08.2013 MAJIRA YA  SAA 18:30HRS HUKO KATIKA KJIJI CHA MWAPIMBUKA  BARABARA YA  MBEYA/IRINGA WILAYA YA  MBARALI MKOA WA MBEYA. GARI T.877 CLX/T.242 CLV AINA YA  IVECO LIKIENDESHWA NA HABIBU S/O HASSAN, MIAKA 28, MLUGURU, MKAZI WA BUGURUNI DSM, LILIMGONGA MTEMBEA KWA MIGUU MTOTO PASTO D/O FURAHA, MIAKA 11, MNYIHA,MWANAFUNZI S/MSINGI IGURUSI DARASA LA PILI MKAZI WA KIJIJI CHA MWAPIMBUKA NA KUSABABISHA KIFO CHA CHAKE WAKATI ANAENDELEA KUPATIWA MATIBABU KATIKA KITUO CHA AFYA IGURUSI. MWILI WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA KATIKA KITUO HICHO CHA AFYA. CHANZO MWENDO KASI. MTUHUMIWA ALIKIMBIA NA KULITELEKEZA GARI  ENEO LA TUKIO MARA  BAADA YA   AJALI. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI ANATOA WITO KWA MADEREVA KUWA MAKINI WANAPOTUMIA VYOMBO VYA MOTO KWA KUZINGATIA SHERIA ZA USALAMA BARABARANI ILI KUEPUSHA AJALI ZINAZOWEZA KUEPUKIKA. AIDHA ANATOA RAI KWA YEYOTE MWENYE TAARIFA JUU YA  MAHALI ALIPO MTUHUMIWA AZITOE KATIKA MAMLAKA HUSIKA ILI AKAMATWE NA SHERIA ICHUKUE MKONDO WAKE, VINGINEVYO AJISALIMISHE MARA MOJA.


WILAYA YA  MBARALI – KUPATIKANA NA POMBE HARAMU YA  MOSHI
                                             [GONGO] NA   MTAMBO WA KUTENGENEZEA POMBE.


MNAMO TAREHE 29.08.2013 MAJIRA YA  SAA 08:00HRS HUKO RUJEWA MJINI WILAYA YA  MBARALI MKOA WA MBEYA. ASKARI POLISI WAKIWA KATIKA DORIA/MSAKO WALIMKAMATA EZEKIEL S/O JAKOBO, MIAKA 26, MBENA,MKULIMA MKAZI WA UHAVILA NA WENZAKE SITA WAKIWA NA POMBE HARAMU YA  MOSHI [GONGO] UJAZO WA LITA 25 PAMOJA NA MTAMBO MMOJA WA KUTENGENEZEA POMBE HIYO. WATUHUMIWA NI WATUMIAJI NA WAUZAJI WA POMBE HIYO. TARATIBU ZINAFANYWA ILI WAFIKISHWE MAHAKAMANI.  KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI ANATOA WITO KWA JAMII KUACHA KUTUMIA POMBE HARAMU YA  MOSHI[GONGO] KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NA NI HATARI KWA AFYA YA  MTUMIAJI.









[ DIWANI ATHUMANI – ACP ]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.