Na Thompson Mpanji,Dar
WANAWAKE nchini wameendelea
kupataza sauti zao kwa tume ya Katiba kuwekwa wazi na kutamka bayana
masuala yanayohusu wanawake katika rasimu ya katiba mpya ya Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania ikiwemo katika eneo la Tunu za Taifa kwa kuongeza
neno Usawa wa jinsia.
Hayo yamesemwa na
mwezeshaji katika jukwaa la Katiba Ruth Meena katika viwanja vya makao makuu ya Mtandao wa
Jinsia Tanzania
(TGNP),Mabibo,jijini hapa wakati wa maadhimisho ya Tamasha la miaka 20 ya
shirika hilo
tangu kuanzishwa.
Meena amesema katika
Katiba mpya inayotarajiwa kuundwa ni muhimu kutoa kipaumbele na kuingizwa
kmasuala ya wanawake ambayo hayataleta mkanganyiko kwa namna yeyote
ili mambo ya msingi yaendelea kuchukuliwa uzito.
Mwezeshaji huyo amesema usawa
wa jinsia lazima utiririke katika katiba yote kwani
ndiyo msingi mkuu huku akidai haki za wanawake lazima zibainishwe kwa
uwazi,haki za mtoto hasa wa kike ziwekwe bayana kwani wanafahamu
muktadha wa jamii katika kumbagua mtoto wa kike.
Meena alisema mila na
desturi zinazokinzana na wanawake zibatilishe na katiba
mpya iseme kwa uwazi,miiko watakayopewa viongozi watakawaongoza
ioneshe kupinga ukatili sanjari na vyama vya siasa kupewa
mipaka katika kampeni kuhusu matumizi ya pesa ili nchi isije kuongozwa
na fedha chafu.
Awali kabla ya kuanza kwa
mjadala wa jukwaa la katiba ,vijana kutoka jukwaa la wanaharakati
wanawake (WFF) kutoka TGNP walitumbuiza kwa ngonjera huku baadhi
ya washiriki wakishangilia ubeti mmoja uliowavuita wengi.
Akianzisha ubeti huo mmoja wa
wanaharakati hao,Aisha Kijawala aliuliza machangudoa wateja wake nani
ambapo wenzake walijibu kuwa ni Mawaziri,Wabunge,Mapolisi na wengine
wengi ubeti uliowainua washiriki wote katika tamasha hilo la TGNP huku
wakiwatuza fedha.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment