Translate

Sunday, September 8, 2013

wawili wafariki kwa ajali Mbeya mjini na Rungwe,Dereva wa Hiace asakwa baada ya kusababisha kifo na kukimbia



TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI
 “PRESS RELEASE” TAREHE   07. 09. 2013.


WILAYA YA RUNGWE – AJALI YA GARI KUMGONGA MPANDA PIKIPIKI NA      
                                                KUSABABISHA KIFO.

MNAMO TAREHE 06.09.2013 MAJIRA YA SAA 17:00HRS HUKO ISYONJE BARABARA YA MBEYA/TUKUYU WILAYA YA RUNGWE MKOA WA MBEYA. GARI NO T.906 AJK T/HIACE LIKIENDESHWA NA DEREVA ASIYEFAHAMIKA LILIMGONGA MPANDA PIKIPIKI NO T.215 CMM BOXER ILIYOKUWA IKIENDESHWA NA EMMANUEL S/O MGIMWA, MIAKA 59, MHEHE, AFISA KILIMO WA IDWELI NA KUSABABISHA KIFO CHAKE PAPO HAPO. CHANZO CHA AJALI NI DEREVA WA HIACE KUTAKA KULIPITA GARI LA MBELE YAKE BILA KUCHUKUA TAHADHARI. DEREVA ALIKIMBIA NA GARI MARA BAADA YA TUKIO HILO JUHUDI ZA KUMTAFUTA ZINAENDELEA. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI ANATOA WITO KWA MADEREVA KUWA MAKINI WANAPOTUMIA VYOMBO VYA MOTO KWA KUZINGATIA SHERIA ZA USALAMA BARABARANI ILI KUEPUSHA AJALI ZINAZOWEZA KUEPUKIKA. AIDHA ANATOA RAI KWA YEYOTE MWENYE TAARIFA JUU YA  MAHALI ALIPO MTUHUMIWA AZITOE KATIKA MAMLAKA HUSIKA ILI AKAMATWE NA SHERIA ICHUKUE MKONDO WAKE, VINGINEVYO AJISALIMISHE.


WILAYA YA MBEYA MJINI – AJALI YA GARI KUMGONGA MTEMBEA KWA
                                                         MIGUU NA       KUSABABISHA KIFO.

MNAMO TAREHE 06.09.2013 MAJIRA YA SAA 06:10HRS HUKO ISANGA BARABARA YA MBEYA/CHUNYA GARI NO. T.156 AHN SCANIA BUS LIKIENDESHWA NA DEREVA BARAKA S/O MGALULA, MIAKA 37, MSUKUMA NA MKAZI WA TABORA LILIMGONGA MTEMBEA KWA MIGUU AITWAYE KANUNU S/O PENJA, MIAKA 75, MNYAKYUSA NA MKAZI WA ISANGA NA KUSABABISHA KIFO CHAKE PAPO HAPO. CHANZO CHA AJALI NI MWENDO KASI. MWILI WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA KATIKA HOSPITALI YA RUFAA MBEYA.  DEREVA AMEKAMATWA NA GARI LIPO KITUONI. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI  ANATOA WITO KWA MADEREVA KUWA MAKINI WANAPOTUMIA VYOMBO VYA MOTO KWA KUZINGATIA SHERIA ZA USALAMA BARABARANI ILI KUEPUSHA AJALI ZINAZOWEZA KUEPUKIKA.


Signed by:

[DIWANI ATHUMANI - ACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA

No comments:

Post a Comment