Translate

Tuesday, February 12, 2013

habari na historia kuhusiana na kujihudhuru papa B.16


    
Maskani > Kanisa >  2013-02-12 09:48:37
A+A-Chapisha ukurasa huuTuma kwa e-mail

http://sw.radiovaticana.va/global_images/x.gif
http://sw.radiovaticana.va/global_images/x.gif
Mchakato wa kumtafuta Papa Mpya kuanzia tarehe Mosi, Machi 2013
http://sw.radiovaticana.va/global_images/x.gif
http://sw.radiovaticana.va/global_images/x.gif
http://media01.radiovaticana.va/imm/1_0_664106.JPGPadre Federico Lombardi akielezea kuhusu tamko la Baba Mtakatifu Benedikto wa kumi na sita la kung'atuka kutoka madarakani mintarafu sheria za Kanisa anasema kwamba, ili Kiti cha Khalifa wa Mtakatifu Petro kiweze kuwa wazi, lazima idhihirishe wazi kwamba, kujiuzuru huku kuwe ni huru na wala si lazima kukubaliwe na wote.

Hivi ndivyo alivyofanya Baba Mtakatifu Benedikto wa kumi na sita, Jumatatu tarehe 11 Februari 2013 wakati wa Mkutano na Dekania ya Makardinali. Baba Mtakatifu atang'atuka rasmi madarakani hapo tarehe 28 Februari 2013, saa 2:00 Usiku. Tangu wakati huo Kiti cha Khalifa wa Mtakatifu Petro kitakuwa wazi kadiri ya Sheria za Kanisa.

Padre Lombardi anasema, Baba Mtakatifu Benedikto wa kumi na sita alipohojiwa na Bwana Peter Seewald, mwandishi wa kitabu alionesha kwamba, kuna uwezekano mkubwa kwa Khalifa wa Mtakatifu Petro kujiuzuru wadhifa wake katika hali ya amani, anapojisikia kwamba, hana tena nguvu ya kuweza kulihudumia Kanisa kwa tija na ufanisi mkubwa kutokana na matatizo ya afya, akili na kiroho. Kwa mazingira kama haya Papa anapaswa na kulazimika kujiuzuru wadhifa wake.

Baba Mtakatifu Benedikto wa kumi na sita, anatarajiwa kuhamia Ikulu ndogo ya Castel Gandolfo, nje kidogo ya mji wa Roma, ili kukamilisha baadhi ya majukumu yake katika uongozi. Wakati huo huo, ukarabati wa nyumba atakamoishi Baba Mtakatifu Benedikto wa kumi na sita, mjini Vatican utakuwa unakamilika. Mchakato wa kumchagua Khalifa wa Mtakatifu Petro, utaanza rasmi hapo tarehe Mosi Machi 2013. Padre Lombardi anasema kwamba, bado tarehe rasmi haijapangwa, lakini hakutakuwa na haja ya kusubiri siku nane kama zinavyotajwa wakati wa maombolezo ya kifo cha Papa.

Katika kipindi cha majuma mawili katika mwezi Machi, Kanisa litakuwa na Papa Mpya. Baba Mtakatifu Benedikto wa kumi na sita, kwa unyenyekevu mkubwa hatahusika kwenye Mkutano wa kumchagua Papa mwingine wala kujihusisha na shughuli za uongozi wa Kanisa kadiri ya sheria za Kanisa. Wakati huu Kanisa litakuwa chini ya Dekano wa Makardinali ambaye kwa sasa ni Kardinali angelo Sodano na Kardinali Tarcisio Bertone.

Padre Federico Lombardi anahitimisha kwamba kusema kwamba, binafsi amepokea tamko la Baba Mtakatifu Benedikto wa kumi na sita la kung'atuka kutoka madarakani kwa mshangao na hamasa kubwa kutokana na uhuru wake wa ndani pamoja na kujali wajibu na utume wa Khalifa wa Mtakatifu Petro kwa ajili ya mafao ya Kanisa. Baba Mtakatifu Benedikto wa kumi na sita, ameonesha ushuhuda mkubwa wa uhuru wa maisha ya kiroho, busara na hekima katika kuliongoza Kanisa kwenye Karne ya 21 yenye changamoto nyingi.


Kanisa limelipokea Tamko la Baba Mtakatifu Benedikto XVI kwa mshangao mkubwa!
http://sw.radiovaticana.va/global_images/x.gif
http://sw.radiovaticana.va/global_images/x.gif
http://media01.radiovaticana.va/imm/1_0_664087.JPGKardinalo Angelo Sodano, Dekano wa Makardinali, Jumatatu tarehe 11 Februari 2013 kwa niaba ya Makardinali wenzake amemwambia Baba Mtakatifu Benedikto wa kumi na sita kwamba, wamepokea habari za kung'atuka kwake madarakani kwa mshangao mkubwa! Ni tamko linaloonesha upendo mkuu kwa Kanisa la Mungu.

Makardinali wataendelea kumwonesha mshikamano na ushirikiano wa dhati hasa wakati huu baada ya kufanya maauzi mazito kwa ajili ya mafao na ustawi wa Kanisa baada ya kuliongoza Kanisa Katoliki kwa takribani miaka 8. Ilikuwa ni tarehe 19 Aprili 2005 alipokubali kubeba dhamana ya uongozi wa Kanisa Katoliki, akajiweka chini ya ulinzi na usimamizi wa Bikira Maria, akifuata nyayo za watangulizi wake 265 waliowahi kuliongoza Kanisa Katoliki tangu Mtakatifu Petro, yapata miaka elfu mbili iliyopita.

Kardinali Sodano anabainisha kwamba, kabla ya tarehe 28 Februari 2013, saa 2:00 Usiku, watapata nafasi ya kutoa heshima na shukrani zao za dhati, kama ambavyo watafanya viongozi wa Kanisa, Waamini na Watu wenye mapenzi mema kutoka sehemu mbali mbali za dunia. Katika kipindi hiki cha mpito, Kanisa bado litaendelea kumsikiliza Baba Mtakatifu Benedikto wa kumi na sita, katika mahubiri yake Jumatano ya Majivu, Mama Kanisa anapokianza kipindi cha Kwaresima; kwenye Katekesi zake Jumatano, Mkutano pamoja na Makleri wa Jimbo kuu la Roma pamoja na tafakari zake wakati wa Sala ya Malaika wa Bwana.

Kanisa kuwatangaza watakatifu wapya watatu hapo tarehe 12 Mei 2013
http://sw.radiovaticana.va/global_images/x.gif
http://sw.radiovaticana.va/global_images/x.gif
http://media01.radiovaticana.va/imm/1_0_664094.JPGBaba Mtakatifu Benedikto wa kumi na sita katika mkutano maalum na Dekania ya Makardinali hapo tarehe 11 Februari 2013 ameridhiwa Wenyeheri wafuatao kutangazwa kuwa watakatifu hapo tarehe 12 Mei 2013.

1. Mwenyeheri Antonio Primaldo na Wenzake: wafiadini.
2. Laura wa Mtakatifu Catherina wa Siena Montoya y Upegui, Bikira na Mwanzilishi wa Shirika la Masista Wamissionari wa Bikira Maria Mkingiwa Dhambi ya Asili na Shirika la Mtakatifu Catherina wa Siena.
3. Maria Guadalupe garcia Zavala, Mwanzilishi mwenza wa Shirika la Wahudumu wa Mtakatifu Margharita Maria wa Maskini.

Baba Mtakatifu Benedikto wa kumi na sita, aliungana na Makardinali 51 kwa kusali pamoja Sala ya Kanisa pamoja na kutoa mahubiri mafupi. Baada ya kupata maelezo ya kina kuhusu Wenyeheri hawa kutoka kwa Kardinali Angelo Amato, Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa linaloshughulikia kuwatangaza waamini kuwa wenyeheri na watakatifu, aliuliza maoni ya Makardinali nao wakakubali, ili waweze kutangazwa na kuandikwa kwenye Orodha ya Majina ya Watakatifu wa Kanisa Katoliki.

Viongozi wa Jumuiya ya Kimataifa wanampongeza na kumshukuru Baba Mtakatifu Benedikto XVI kwa unyenyekevu na ujasiri mkuu!
http://sw.radiovaticana.va/global_images/x.gif
http://sw.radiovaticana.va/global_images/x.gif
http://media01.radiovaticana.va/imm/1_0_664092.JPGTamko la Baba Mtakatifu Benedikto wa kumi na sita alilolitoa Jumatatu tarehe 11 Februari 2013 kuhusu kung'atuka kwake kutoka madarakani kutokana na sababu za umri na afya, zimewashtua watu wengi kiasi cha kubaki wameshika tama!

Habari kutoka sehemu mbali mbali za dunia zinaonesha kutambua mchango wa Baba Mtakatifu Benedikto wa kumi na sita pamoja na kuupokea uamuzi wake kwa heshima na taadhima, kwani kitendo cha ujasiri, moyo mkuu, unyenyekevu na uwajibikaji. Ni maneno ya Rais Giorgio Napolitano wa Italia, ambaye hivi karibuni walikuwa pamoja kusikiliza Tamasha la muziki lililokuwa limeandaliwa kwa ajili ya Maadhimisho ya Kumbu kumbu ya Mkataba wa Laterano.

Kardinali Angelo Bagnasco, Rais wa Baraza la Maaskofu Katoliki Italia anasema, kwa mara nyingine tena, Baba Mtakatifu Benedikto wa kumi na sita, ameonesha mfano na kielelezo cha kuigwa kwa ajili ya mafao ya Kanisa, kwa kuamua kung'atuka kutoka madarakani kwa utashi na uhuru kamili. Kanisa Katoliki nchini Italia linamshukuru kwa mchango wake wa hali na mali katika maisha na utume wa Kanisa nchini Italia.

Naye Chancellor Angela Merkel wa Ujerumani anasema amezipokea habari hizi kwa mshtuko mkubwa kiasi cha kuamsha ndani mwake heshima kubwa kwa Baba Mtakatifu Benedikto wa kumi na sita kutokana na mikutano yao mjini Roma na alipopata fursa ya kutembelea Ujerumani kunako mwaka 2011. Anakumbuka kwa namna ya pekee hotuba yake kwa Bunge la Shirikisho la Wananchi wa Ujerumani kuhusu dhamana ya wanasiasa katika Jamii: kusimama kidete kulinda na kutetea haki na ukweli. Ni changamoto ambayo imeacha chapa ya kudumu katika maisha yake.

Rais Francois Hollande wa Ufaransa anasema kwamba, huu ni uamuzi mgumu unaopaswa kuheshimiwa, kwa namna ya pekee kabisa anampongeza Baba Mtakatifu Benedikto wa kumi na sita kwa ujasiri na unyenyekevu wa aina hii.

Waziri mkuu wa Uingereza David Cameron amemwandikia Baba Mtakatifu Benedikto wa kumi na sita, ujumbe wa matashi mema na kwamba, watu wengi watakosa hekima na busara yake kama Kiongozi mkuu wa Kanisa. Amejitahidi sana kuhakikisha kwamba, uhusiano kati ya Uingereza na Vatican unaendelea kuimarika.

Askofu mkuu Justin Welby wa Kanisa kuu la Cantebury ambaye pia ni Kiongozi Mkuu wa Jumuiya ya Waanglikani Duniani, anasema, amepokea kwa mshangao mkubwa taarifa za kung'atuka kwa Baba Mtakatifu Benedikto wa kumi na sita kutoka madarakani. Kuwa Khalifa wa Mtakatifu Petro ni dhamana nyeti na yenye heshima ya hali ya juu, inayohitaji kuwa na mwono mpana na ujasiri.

Askofu mkuu Welby anamshukuru Mwenyezi Mungu kwa zawadi ya uwepo wa Papa Benedikto wa kumi na sita aliyejitoa bila ya kujibakiza kuliongoza Kanisa: kwa maneno na matendo yake; kwa sala na huduma za kichungaji, kama mfuasi amini wa Kristo.

Viongozi wengi wanamkumbuka Baba Mtakatifu Benedikto wa kumi na sita kwa kuendelea kuhamasisha majadiliano ya kidini na kiekumene; huku akisimama kidete kulinda na kutetea: haki, amani, upendo na mshikamano katika Jumuiya ya Kimataifa, kwa kuongozwa na kanuni auni. Ni matumaini ya viongozi mbali mbali wa kidini kwamba, Kanisa Katoliki litaendeleza majadiliano ya kidini na kiekumene kwa ajili ya mafao ya wengi, amani na ustawi wa Jumuiya ya Kimataifa. Wanaendelea kumtakia afya njema, utulivu na amani ya ndani.

Ni uamuzi wa busara unaofumbata hali ya unyenyekevu na ujasiri mkuu, unaoacha chapa ya kudumu kwa watu wengi. Ni Kiongozi aliyeshirikiana na wengine kuhimiza tunu msingi za maisha ya binadamu. Kwa hakika, uamuzi wake unapaswa kuheshimiwa na kuthaminiwa. Amefanya jambo la msingi kwa wakati muafaka.




No comments:

Post a Comment