Translate

Friday, March 8, 2013

yanayojiri vikao vya kumchagua papa na historia ya mapapa tangu Mtume Petro,mjuwe papa aliyedumu kwa mwezi mmoja na sifa za wengine

BABA  Mtakatifu Benedikto wa kumi na sita, mara baada ya kuondoka mjini Vatican, kuanzia tarehe 28 Februari 2013 anaaishi kwenye Ikulu Ndogo ya Castel Gandolfo, nje kidogo ya mji wa Roma, hadi mwanzoni mwa Mwezi Mei na  baadaye atahamia kwenye Monasteri ya "Mater Ecclesiae" iliyoko mjini Vatican ambayo kwa sasa inafanyiwa ukarabati mkubwa, ulioanza tangu Novemba 2012 na unatarajiwa kukamilika hivi karibuni. Hapa ni mahali ambapo Baba Mtakatifu Benedikto wa kumi na sita, ameadhimisha Ibada ya Misa Takatifu mara mbili.

Mkutano wa Dekania ya Makardinali wenye dhamana ya kumchagua Papa mpya, unaojulikana kama "Conclave" maana yake "kufungiwa na ufunguo" unatarajiwa kufanyika kati ya tarehe 15 hadi 20 Machi 2013, ili kutoa nafasi kwa Makardinali kutoka sehemu mbali mbali za dunia kuweza kuwasili na hatimaye kushiriki katika tukio muhimu katika maisha na utume wa Kanisa. Kunaweza kutokea mabadiliko, ikiwa kama Makardinali wenye dhamana ya kupiga kura watakuwa tayari wamekwisha wasili mjini Roma.

Kikao cha Tano cha Makardinali -bado hakuna tarehe ya kuanza kwa Conclave ambapo  Alhamis, machi,7,2012 asubuhi, Makadinali waliendelea na mkutano wao , wakiwa na kikao cha tano, cha kuelekea Mkutano wa Conclave, Na jioni waliketi katika kikao cha sita.


Mkurugenzi wa ofisini ya Habari Vatican, Padre Federico Lombardi, akitoa muhtasari kwa wanahabari: juu ya kikao cha tano, alifahamisha kwamba, bado haijulikani tarehe ya kuanza Conclave. Alitaja idadi ya Makardinali waliohudhuria kikao cha tano kuwa 152. Na kwamba , alikuwa akikosekana Kardinali mmoja tu mwenye haki ya kupiga kura nae ni Kardinali Pham Minh Man, wa Vietnam aliyekuwa akitarajiwa kuwasili Alhamis.

Padre Lombardi, katika mkutano huu, aliwataka wanahabari kusikiliza kinachoelezwa na Ofisi ya habari ya Vatican na kujiepusha na uvumi unaotolewa na wanahabari wasiojua taratibu za mkutano wa Makardinali Consistori na Conclave, kama baadhi ya vyombo vya habari vilivyo ripoti juu ya Ibada za Misa zinazojulikana kwa jina la “Pro eligendo Pontifici ”, wakidhani Ibada hiyo, itakayoadhimisha Jumatatu katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro ndiyo mwanzo wa Conclave. Hiyo si kweli.


Padre Lombardi amefafanua kwamba, Ibada hizo za Pro Eligendo Pontifici zinaweza kuadhimishwa nyingi tu , kwani hutolewa kwa nia za kuombea baraka vikao vya Conclave na  hivyo, aliendelea, -“Missa Pro eligendo Pontifice” ni Misa inayoweza kuadhimishwa na Padre yeyote, katika siku hizi, kwa nia ya kuomba Roho Mtakatifu alisaidie Kanisa , katika hali hii ya Kiti cha Petro kuwa kitupu na  hivyo si kila Ibada ya Misa Pro eligendo Pontifici, huwa na nia ya kufungua vikao vya Conclave.


Pia katika kikao cha alhamis asubuhi , walichaguliwa wasaidizi wapya wa watatu wa Camerlengo , nao ni Kardinali Boutros Rai Patriaki wa Maronite, akiwakilisha Maaskofu Makardinali , Kardinali Monsengwo kwa Makardinali Mapadre, na Kardinali De Paolis kwa Makardinali Mashemasi, wote watatu watakuwa wasaidizi wa mstari wa Mbele katika dawati la Camerlengo. Kazi watakao ifanya kwa muda wa siku tatu .


Aidha katika kikao hiki cha Tano,katika umoja wao kama Decania ya Makardinali walituma salaam zao za rambirambi , Venezuela , kufuatia kifo cha Rais wa Venezuela Hugo Chavez na  pia, waliendelea kusikiliza michango na maoni , kati ya walioshiriki kutoa hoja, kwanza, ni wale wanaohusika na idara za uchumi , Kardinali Versaldi, Calcagno na Bertello. Versaldi ni Gavana wa Mambo ya Uchumi, rais wa APSA, Tawala za urithi wa Kiti cha Kitume, na Bertello ni Rais wa Utawala Vatican.

Makardinali wanaendelea kusali, kutafakari na kushirikishana mang'amuzi, matatizo, changamoto, fursa za vipaumbele kwa Kanisa katika mapambazuko ya Millenia ya tatu ya Ukristo, wakati huu wanapojiandaa kumchagua Khalifa wa Mtakatifu Petro, baada ya Baba Mtakatifu Benedikto wa kumi na sita, kung'atuka kutoka madarakani na sasa anaendelea kulisindikiza Kanisa kwa njia ya sala na tafakari ya kina.

Makardilai  wanaendelea na  mchakato wa kumchagua Baba Mtakatifu wa  266  kushika wadhifa wa halifa wa mtume Petro  iliyoachwa wazi na Joseph Latzinger ambaye alikuwa ni Baba Mtakatifu wa XVI aliyeamua kujihudhuru februari,28 ,2013 majira ya saa 2.00 usiku.

“Baada ya kujichunguza  nafsi yangu mbele ya mwenyezi mungu,nimefikia uamuzi kuwa uwezo wangu na afya afya,ukiambatana na umri mkubwa ni mambo yatakayokwaza jitihada zangu za kuendelea kuliongoza Kanisa katoliki.”

Haya ni maneno machache  aliyoweza kuzungumza Baba Mtakatifu Benedicto  wakati akitoa sababu za kung’atuka kwake.

Tukio hili la papa limeelezewa kuwashtua wakatoliki walio wengina kwa mujibu wa msemaji wa vatcan Padre Federico Lombardi alisema kuwa hata wasaidizi wake wa karibu sana wa papa hawakuwa na tetesi zozote juu ya tukio hilo.

Kutokana na tukio hilo maoni ama fikra mbalimbali  zimeibuliwa  na watu  tofauti tofauti kutoka kila pembe ya dunia  kwani wapo waliolihusisha tukio hilo  na  kashfa ambazo hazitajwi na hivyo kuishia ni hisia za kashfa na wengine kuhusisha na masuala ya freemasons alimradi kila mmoja akifikiria anavyoona yeye  lakini msimamo umebakia pale pale kama alivyosema yeye mwenyewe  papa  sababu za kuachia kiti hicho cha halifa wa mtume Petro.

lmeelezwa kuwa  tukio la kujihudhuru kwa Papa kwa mara ya mwisho limetokea  miaka 600 iliyopita  ambapo Baba Mtakatifu Gregory wa 205 mzaliwa wa Venice ambaye alichaguliwa  oktoba,18,1406 ambaye alifariki mwaka 1417, alijihudhuru,kwani ilikuwa ni kipindi cha huzuni sana kukiibuka madai matatu  na   kutokana na upinzani wa kidini wa nchi za magharibi na nafasi yake kuchukuliwa na Baba Mtakatifu  Martin,mzaliwa wa roma ilikuwa Novemba,21 mwaka 1417.

Mrithi huyo wa papa aliyejihudhuru  alisheherekea   ujio wa roho mtakatifu mwaka 1423 na kwa mara ya kwanza  lango kuu la  roho mtakatifu lililopo  katika jumba la Basilica la Mtakatifu John lateran lilionekana wazi.

Katika makala hii tutakuwa na mfululizo wa kusoma yanayoendelea kujiri katika vikao vya makardinali,mjini Vatican katika mchakato wa kumchagua Papa mrithi wa papa benedicto sanjari na   kuangalia historia ya  mapapa tangu wa kwanza ambaye alikuwa  mtume Petro mzaliwa wa Bethsaida nchini Galilaya aliyeanza kushika kiti hicho na kufariki juni,29 mwaka 47 hadi papa wa 265 aliyejihudhuru februari,28,2013  na baadhi yao tutaziona sifa zao.

Baada ya kifo cha Mtume Petro  nafasi yake  ilichukuliwa na Baba Mtakatifu Linus kutoka Voltera aliyezaliwa mwaka 67 na alifariki septemba,23 mwaka 76 baada ya kuagiza kuwa mwili wake uchomwe moto jirani na  eneo la St.Peter square huyu ndiye aliyeanzisha nafasi ya uaskofu na alianza na maaskofu 15 aliowateua na alikataa katu katu wanawake kuwa viongozi(wachungaji).

Mwaka 76 alichaguliwa  Baba Mtakatifu mwenye asili ya kutoka nchini Roma aliyeitwa Cletus ambaye alifariki  mwaka 88 na kuteuliwa papa mwingine mromani baba Mtakatifu Clement mwaka huo huo  aliyekuja kufariki mwaka 88,papa huyu anakumbukwa kwa kuanzisha kuitikia katika sala neno “amen.”

Baba Mtakatifu mwenye asili ya Kigiriki Evaristus  alifanikiwa kwa kiasi kikubwa kuongeza idadi ya waumini,alifanikiwa kugawa miji kuwa parokia.

 Baba Mtakatifu Evaristus  alichaguliwa mwaka 97 na alidumu katika kiti chake cha uhalifa wa mtume Petro hadi mwaka 105 alipofariki dunia  na mwaka huo huo alichaguliwa papa mroma aliyefahamika kwa jina la Baba Mtakatifu Alexander I ambaye alidumu kwa miaka 15  hadi  mwaka 115 alipofariki na atakumbukwa kwa  kuanzisha huduma ya matumizi ya maji ya baraka na sakramenti takatifu.

Baba Mtakatifu Sixtus I mroman ambaye alikuja kuchomwa moto naye alifariki mwaka 125 na kuchaguliwa Papa mgiriki aliyetambulika kama Baba mtakatifu Telesphorus ambaye alichaguliwa mwaka 125 hadi 136.

Baba Mtakatifu Hyginus  alichaguliwa mwaka 136 aliendelea na utume wake hadi mwaka   140 mauti yalipomfika na hatimaye  Baba Mtakatifu Pius I  mzaliwa wa Aquileia alichaguliwa  mwaka huo na ndiye aliyechagua  tarehe ya Jumapili ya kwanza  ya siku kuu ya pasaka baada ya mwezi machi.

Baada ya kufariki Baba Mtakatifu Pius I mwaka 155 alichaguliwa Baba Mtakatifu Anicetus  mzaliwa wa Syria mwaka huo huo kurithi kiti hicho  hadi mwaka 166  alipofariki na nafasi yake kurithiwa na Papa Soter ambaye aliitwa  Baba Mtakatifu wa upendo aliyekuja kufariki baadaye mwaka 175.

Alifuatiwa na Baba Mtakatifu Eleutherius aliyedumu hadi mwaka 189,akafuata Baba Mtakatifu Victor kutoka Bara la Afrika aliyeongoza kanisa hilo hadi mwaka 199,huyu ndiye papa aliyeruhusu kutumika kwa maji ya aina yeyote yawe mengi ama  machache katika ubatizo  katika tukio la aina yeyote.

Kumbukumbu zinaonesha kuwa alikuwa ni papa aliyepinga Maaskofu wa Asia na Afrika  kusheherekea siku kuu ya pasaka kwa mapokeo ya kiyahudi na hivyo kudumisha utamaduni wa  kutoka Roma.

Baba mtakatifu wa 15 alikuwa Zephyrinus mzaliwa wa roma aliyechaguliwa mwaka 199 na katika uongozi wake aliagiza vijana wenye umri wa miaka kuanzia 14 na kuendelea kupata komunio ya kwanza wakati wa pasaka na alikuja kufariki mwaka 217.

Baba Mtakatifu Calixtus Mzaliwa wa Roma alichaguliwa mwaka 217 na kufariki mwaka 222 nafasi yake ikashikwa mwaka huo huo  na Baba Mtakatifu Urban 1, hadi mwaka 230 alipofariki,Papa Pontian raia wa Roma  alichaguliwa  agosti,28 mwaka 230 na kufariki sept,28,235 katika kisiwa kidogo cha Travolara.

Baba Mtakatifu Anterus  Mzaliwa wa Magna Grecia nchini Uingereza alidumu kwa mwezi mmoja katika kiti chake baada ya  Disemba,21 mwaka 236 aliuguwa na kufariki mwezi huo huo ambapo januari,10,236 alichaguliwa papa mwingine Fabian mzaliwa wa Roma kuziba nafasi hiyo ambaye alidumu hadi januari,20,250 na alifariki akiwa mikononi mwa mkuu wa himaya aliyetajwa kwa jina la Maximus.

Baba Mtakatifu Anterus alikuwa ni papa wa 19 tangu kwa Mtume Petro na hivyo wiki ijayo usikose kumfahamu papa aliyemrithi papa Anterus huku ukiendelea kufahamu yanayoendelea kujiri katika vikao vinavyoendelea mjini Vatcan.

Makala haya ni  kwa msaada wa idhaa ya Kiswahili ya radio Vatican

tmpanji@yahoo.com/www.mwanamaimpanji.blogspot.com

0712 239272.




No comments:

Post a Comment