HOSPITALI ya Mtakatifu Joseph Mission Peramiho inatangaza huduma ya matibabu
ya ugonjwa wa fistula kwa akina mama bure
ikiwemo chakula na nauli ya
kumfikisha hospitali na kumrudisha.
Fistula ni ugonjwa unaopelekea mwanamke kuvuja mkojo au haja kubwa au vyote kwa pamoja bila
mgonjwa kuweza kujizuia ambapo
hutokea baada ya kujifungua na madhara
yake ni makubwa ikiwa ni pamoja na
kutengwa na wenzi wao na jamii kwa
ujumla kutokana na harufu mbaya ya mkojo na haja kubwa.
Katika taarifa yake
iliyosambazwa katika majimbo,parokia,makanisa mbalimbali ,Dkt.Gaudens Komba
kwa niaba ya Mganga mkuu wa St.joseph’s Mission Hospital Peramiho amesema
Hospitali ya misheni peramiho iliyoko wilayani songea,mkoani Ruvuma itaendesha
mpango maalum wa kutoa matibabu kwa akina mama wenye fistula kuanzia mwezi
aprili,29 hadi mei,11,2013.
Dkt.Komba alisema katika mpango huo wagonjwa wote
watakaojitokeza watapatiwa huduma za nauli ya kumfikisha hospitali ya Peramiho,matibabu
ya ugonjwa wa fistula bure,chakula bure akiwa hospitalini na nauli ya
kumrudisha nyumbani baada ya matibabu.
Mganga huyo alisema
kwa wale wenye matatizo hayo wanaweza kuwasiliana na Hospitali ya
peramiho kupitia nambari za simu ili kupangiwa utaratibu:0754/0784/0715 662029
ama wagonjwa wafike Hospitali ya peramiho kuanzia aprili,28,2013 tayari kwa
matibabu.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment