Translate

Monday, November 26, 2012

mwanamke anayetuhumiwa kumtesa hadi kukatwa mkono mtoto Aneth kizimbani

Na Thompson Mpanji,Mbeya
 
MWANAMKE anayetuhumiwa kumtesa kumlisha kinyesi na kumchoma moto  mtoto wa kaka  yake  kumfungia ndani,  amepandishwa    kizimbani kwa mara ya pili    katika mahakama ya Wilaya ya Mbeya kujibu shtaka linalomkabili.
 
 
Mwendesha mashtaka wa Serikali, Achiles Mulisa ameileza  Mahakama kuwa Mtuhumiwa Wilvina Mkandala (24) Mkazi wa Majengo jijini humo  alitenda kosa la kusababisha majeraha akiwa na nia ovu ambayo imemsababishia ulemavu mtoto  Aneth Gasto (4).
 
 
Mulisa akisoma mashtaka hayo mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi wa mahakama hiyo Gilbert Ndeuruo amesema kosa hilo ni kinyume cha kanuni ya adhabu kifungu  cha 222(a) sura ya 16 kama ilivyorejewa mwaka 2002.
 
 Kutokana na hali hiyo mwendasha mashitaka huyo ameileza mahakama kuwa kesi inayo mkabili mwanamke huyo ilihitaji mashahidi sita   ambao ni Dactari aliye mfanyia upasuaji mtoto huyo   mwenyekiti wa Mtaa na barozi wake pamoja na Askari mpelelezi wa kesi hiyo na mtoto mwenye .
 
 
Amesema teyari mashahidi wanne kati ya sita wamekwisha toa ushahidi wao mahakani hapo .
 
 
Kutokana na kosa hilo mshtakiwa amekana shitaka hilo ambapo alirudishwa mahabusu hadi Novemba 27 Mwaka huu kesi hiyo itakapotajwa tena.
 
 
Amesema upande wa Jamhuri unamashahidi wanne ambao watatu kati yao teyari wamekwsha toa ushahidi wao katika mahakama hiyo .
 
 
Amewataja mashahidi hao kuwa ni Mwenyekiti wa Mtaa wa Majengo Shuku Mwakanyamale, Daktari anayemtibu mhanga katika Hospitali ya Rufaa ya Mbeya Dr. Paul Kasubi  na Habiba Mwakanyamale.
 
 
Wengine ni Askari Polisi aliyepeleza kesi hiyo WP Pudensia na Mtoto mwenyewe  ambao wako tayari kufika mahakamani na kutoa ushahidi wao mbele ya mahakama.
 
 
Awali mshatakiwa huyo aliieleza mahakama kuwa na uhusiano na mtoto  huyo ambapo pia alikiri kuwa na taarifa za kile kinachoendelea juu ya matibabu ya mtoto huyo na kuhusu kukatwa kwa mkono wake wa kushoto na kufungwa bandeji ngumu(POP) kwenye mkono uliobaki.
 
 
 

No comments:

Post a Comment