Translate

Tuesday, January 14, 2014

Jan,13,2014 matukio ya uvutaji wa banghi na unywaji wa pombe haramu ya gongo yatagonga vichwa vya habari Mbeya




TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI
“PRESS RELEASE” TAREHE 14.01. 2014.

WILAYA YA MBEYA MJINI – AJALI YA PIKIPIKI KUGONGA GARI NA
                                                   KUSABABISHA VIFO.

MNAMO TAREHE 13.01.2014 MAJIRA YA SAA 04:30HRS HUKO KATIKA ENEO LA SAE, KATA YA MWAKIBETE, TARAFA YA IYUNGA, JIJI NA MKOA WA MBEYA BARABARA YA MBEYA/NJOMBE. PIKIPIKI T.436 CLP AINA YA T-BETTER IKIENDESHWA NA GABRIEL S/O NGALELE, MIAKA 24, KYUSA, MKAZI WA UYOLE   ILIGONGA KWA NYUMA GARI T.684 BVY AINA YA SCANIA LILILOKUWA LIMEEGESHWA NA DEREVA ASIYEFAHAMIKA JINA WALA MAKAZI YAKE NA KUSABABISHA KIFO CHA MWENDESHA PIKIPIKI HUYO PIA KUSABABISHA KIFO KWA ABIRIA ALIYEKUWA KATIKA PIKIPIKI HIYO AMBAYE HAFAHAMIKI JINA WALA MAKAZI YAKE JINSI YA KIKE. CHANZO CHA AJALI KINACHUNGUZWA. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA MADEREVA KUWA MAKINI WANAPOTUMIA VYOMBO VYA MOTO KWA KUZINGATIA SHERIA NA ALAMA ZA USALAMA BARABARANI ILI KUEPUKA AJALI ZINAZOWEZA KUEPUKIKA.

WILAYA YA MBEYA MJINI – KUPATIKANA NA POMBE HARAMU YA MOSHI
                                                 [GONGO].

MNAMO TAREHE 13.01.2014 MAJIRA YA SAA 11:40HRS HUKO UYOLE VILABUNI, KATA YA IGAWILO, TARAFA YA IYUNGA, JIJI NA MKOA WA MBEYA, ASKARI POLISI WAKIWA DORIA/MSAKO WALIMKAMATA JOSEPH S/O MWAKISA, MIAKA 38, KYUSA, MKULIMA MKAZI WA NSALAGA NA WENZAKE WANNE WAKIWA  NA POMBE YA  MOSHI [GONGO] UJAZO WA LITA MOJA NA NUSU [1 ½ ]. WATUHUMIWA NI WATUMIAJI WA POMBE HIYO. TARATIBU ZA KISHERIA ZINAFANYIKA DHIDI YAO.  KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA JAMII  KUACHA TABIA YA KUTUMIA POMBE HARAMU YA MOSHI KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NA NI HATARI KWA AFYA YA MTUMIAJI.

WILAYA YA MBEYA MJINI - KUPATIKANA NA POMBE HARAMU YA 
                                                               MOSHI [GONGO].

MNAMO TAREHE 13.01.2014 MAJIRA YA SAA 14:30HRS HUKO MWANJELWA,  KATA YA  MAANGA, TARAFA YA  IYUNGA, JIJI NA MKOA WA MBEYA, ASKARI POLISI WAKIWA DORIA/MSAKO WALIMKAMATA SUMA D/O MWAMPIKI, MIAKA 29, KYUSA, MKULIMA MKAZI WA ILOLO NA WENZAKE WANNE WAKIWA  NA POMBE YA  MOSHI [GONGO] UJAZO WA LITA MOJA NA NUSU [1 ½ ]. WATUHUMIWA NI WATUMIAJI WA POMBE HIYO. TARATIBU ZA KISHERIA ZINAFANYIKA DHIDI YAO. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA JAMII HASA VIJANA KUACHA TABIA YA KUTUMIA POMBE HARAMU YA MOSHI KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NA NI HATARI KWA AFYA YA MTUMIAJI.





WILAYA YA MBEYA MJINI - KUPATIKANA NA POMBE HARAMU YA 
                                                               MOSHI [GONGO].

MNAMO TAREHE 13.01.2014 MAJIRA YA SAA 14:30HRS HUKO MWANJELWA,  KATA YA  MAANGA, TARAFA YA  IYUNGA, JIJI NA MKOA WA MBEYA, ASKARI POLISI WAKIWA DORIA/MSAKO WALIMKAMATA TUKULAMBA D/O ASTON, MIAKA 30, KYUSA, MKULIMA MKAZI WA MAFIATI  AKIWA  NA POMBE YA  MOSHI [GONGO] UJAZO WA LITA TATU [03] .MTUHUMIWA NI MTUMIAJI  NA MUUZAJI WA POMBE HIYO. TARATIBU ZA KISHERIA ZINAFANYIKA DHIDI YAKE. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA JAMII KUACHA TABIA YA KUTUMIA POMBE HARAMU YA MOSHI KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NA NI HATARI KWA AFYA YA MTUMIAJI.

WILAYA YA MBEYA MJINI - KUPATIKANA NA BHANGI.

MNAMO TAREHE 13.01.2014 MAJIRA YA SAA 10:00HRS HUKO ITEZI, KATA YA  ITEZI, TARAFA YA  IYUNGA, JIJI NA MKOA WA MBEYA, ASKARI POLISI WAKIWA DORIA/MSAKO WALIMKAMATA FRED S/O MBOGELA, MIAKA 24, KYUSA, MKULIMA MKAZI WA UYOLE  AKIWA  NA BHANGI KETE TATU [03] SAWA NA UZITO WA GRAM 15 .MTUHUMIWA NI MTUMIAJI  NA MUUZAJI WA BHANGI HIYO. TARATIBU ZA KISHERIA ZINAFANYWA DHIDI YAKE. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA JAMII HASA VIJANA KUACHA TABIA YA KUTUMIA DAWA ZA KULEVYA KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NA NI HATARI KWA AFYA YA MTUMIAJI.

WILAYA YA KYELA – KUPATIKANA NA POMBE HARAMU YA MOSHI [GONGO].

MNAMO TAREHE 13.01.2014 MAJIRA YA SAA 17:30HRS HUKO KATIKA KIJIJI CHA KATUMBATUKUYU, KATA YA  IBHIGI, TARAFA YA  UKUKWE, WILAYA YA  RUNGWE, MKOA WA MBEYA, ASKARI POLISI WAKIWA DORIA/MSAKO WALIMKAMATA VICK D/O EMANUEL, MIAKA 20, KYUSA, MKULIMA MKAZI WA KATUMBA  AKIWA  NA POMBE YA  MOSHI [GONGO] UJAZO WA LITA MBILI [02]. MTUHUMIWA NI MTUMIAJI NA MUUZAJI WA POMBE HIYO. TARATIBU ZA KISHERIA ZINAFANYWA DHIDI YAKE.  KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA JAMII  KUACHA TABIA YA KUTUMIA POMBE HARAMU YA MOSHI KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NA NI HATARI KWA AFYA YA MTUMIAJI.


Signed by:
[AHMED Z. MSANGI – SACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.




No comments:

Post a Comment