Translate

Friday, October 25, 2013

akamatwa na noti bandia mbeya,wawili akiwepo msukuma mkokoteni na mpanda baiskeli wafariki dunia kwa kugongwa na gari





TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI
“PRESS RELEASE” TAREHE 25. 10. 2013.


WILAYA YA MBARALI – AJALI YA GARI KUMGONGA MPANDA BAISKELI NA   KUSABABISHA
                                          KIFO.

MNAMO TAREHE 24.10.2013 MAJIRA YA SAA 21:10HRS HUKO KATIKA KIJIJI CHA ITAMBOLEO  KATA YA  IGURUSI,  TARAFA YA  ILONGO BARABARA YA  MBEYA/IRINGA  WILAYA YA  MBARALI MKOA WA  MBEYA.  GARI T.201 ARU /T.497 BDG AINA YA SCANIA LIKIENDESHWA NA DEREVA ASIYEFAHAMIKA JINA WALA MAKAZI YAKE, LILIMGONGA MPANDA BAISKELI YESAYA S/O MEDSON,  MIAKA 39,   MUWANJI,  MKULIMA,  MKAZI ITAMBOLEO NA KUSABABISHA KIFO CHAKE PAPO HAPO. CHANZO NI MWENDO KASI. MWILI WA MAREHEMU UMEFANYIWA UCHUNGUZI NA KUBABIDHIWA NDUGU KWA AJILI YA MAZISHI. DEREVA ALIKIMBIA MARA BAADA YA AJALI NA KULITELEKEZA GARI ENEO LA TUKIO. KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI ROBERT MAYALA ANATOA WITO KWA MADEREVA KUWA MAKINI WANAPOTUMIA VYOMBO VYA MOTO KWA KUZINGATIA SHERIA NA ALAMA ZA USALAMA  BARABARANI ILI KUEPUSHA AJALI ZINAZOWEZA KUEPUKIKA. AIDHA ANATOA RAI KWA YEYOTE MWENYE TAARIFA JUU YA MAHALI ALIPO MTUHUMIWA AZITOE KATIKA MAMLAKA HUSIKA ILI AKAMATWE NA SHERIA ICHUKUE MKONDO WAKE, VINGINEVYO AJISALIMISHE MWENYEWE.


WILAYA YA MBEYA MJINI - AJALI YA GARI KUMGONGA MSUKUMA
                                                                        MKOKOTENI NA KUSABABISHA KIFO.

MNAMO TAREHE 24.10.2013 MAJIRA YA SAA 05:45HRS HUKO KATIKA ENEO LA MWANJELWA, KATA YA RUANDA, TARAFA YA IYUNGA BARABARA YA MBEYA/IRINGA JIJI NA MKOA WA MBEYA.  GARI T.600 AJF AINA YA TOYOTA COROLA LIKIENDESHWA NA DEREVA WAZIRI S/O SANGA, MIAKA 27, MKINGA, MKAZI WA KADEGE LILIMGONGA MSUKUMA MKOKOTENI   BENARD S/O MWASAKIBAKI, MIAKA 21,   KYUSA, MKULIMA, MKAZI MWANJELWA  NA KUSABABISHA KIFO CHAKE PAPO HAPO. CHANZO NI MWENDO KASI. MWILI WA MAREHEMU UMEFANYIWA UCHUNGUZU NA KUBABIDHIWA NDUGU KWA AJILI YA MAZISHI. DEREVA AMEKAMATWA TARATIBU ZA KISHERIA ZINAFANYWA ILI AFIKISHWE MAHAKAMANI. KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI ROBERT MAYALA ANATOA WITO KWA MADEREVA KUWA MAKINI WANAPOTUMIA VYOMBO VYA MOTO KWA KUZINGATIA SHERIA NA ALAMA ZA USALAMA BARABARANI ILI KUEPUSHA AJALI ZINAZOWEZA KUEPUKIKA.

WILAYA YA  MBEYA  – KUPATIKANA NA NOTI BANDIA.


MNAMO TAREHE 24.10.2013 MAJIRA YA  SAA 08:00HRS HUKO KATIKA ENEO LA SOWETO,  KATA YA  SOWETO , TARAFA YA IYUNGA  JIJI NA  MKOA WA MBEYA.  FELEX S/O MWAMPAMBA, MIAKA 23, MNDALI, MKULIMA, MKAZI WA ILOLO   ALIKAMATWA AKIWA NA NOTI BANDIA MBILI ZA TSHS 10,000/= KILA MOJA ZENYE NAMBA- AA-4248048 NA BC-2937831. MBINU NI KUTAKA KUNUNUA MAHITAJI KATIKA DUKA LA ALFRED S/O THADEI @ SANGA, MIAKA 24, MKINGA, BIASHARA, MKAZI WA MAMA JOHN. TARATIBU ZA KISHERIA ZINAFANYWA ILI AFIKISHWE MAHAKAMANI. KAIMU  KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA  KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI  ROBERT MAYALA ANATOA WITO KWA JAMII KUCHUKUA TAHADHARI KWA MATUMIZI YA PESA HASA NOTI ILI KUEPUKA MATATIZO YANAYOWEZA KUEPUKIKA. AIDHA ANATOA RAI KWA YEYOTE MWENYE TAARIFA JUU YA MTU/WATU AU MTANDAO UNAOJIHUSISHA NA UTENGENEZAJI/USAMBAZAJI WA NOTI BANDIA  AZITOE KATIKA MAMLAKA HUSIKA ILI WAHUSIKA WAKAMATWE NA SHERIA ICHUKUE MKONDO WAKE.




[ ROBERT MAYALA - ACP ]
KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.

No comments:

Post a Comment