TAARIFA YA JESHI LA
POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI
“PRESS RELEASE” TAREHE 20. 10. 2013.
WILAYA YA MBEYA
VIJIJINI - AJALI YA GARI KUMGOGA MTEMBEA KWA
MIGUU NA KUSABABISHA KIFO.
.
|
MNAMO TAREHE
19.10.2013 MAJIRA YA SAA 18:00HRS
HUKO KIJIJI CHA GARIJEMBE, KATA YA TEMBELE, TARAFA YA TEMBELE BARABARA YA MBEYA/TUKUYU WILAYA YA MBEYA. GARI LISILOFAHAMIKA NAMBA WALA DEREVA LILIMGONGA MTEMBEA KWA
MIGUU {MTOTO} AITWAYE LUSI D/O SAFARI,
MIAKA 12, MSAFWA, MWANAFUNZI WA DARASA LA SITA SHULE YA MSINGI GARIJEMBE NA
KUSABABISHA KIFO CHAKE WAKATI AKIPELEKWA HOSPITALINI. MWILI WA MAREHEMU
UMEHIFADHIWA KATIKA HOSPITALI YA RUFAA MBEYA. CHANZO CHA AJALI NI MWENDO KASI.
DEREVA ALIKIMBIA NA GARI MARA BAADA YA TUKIO NA MSAKO MKALI UNAENDELEA DHIDI
YAKE. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI
ATHUMANI ANATOA WITO KWA MADEREVA KUWA
MAKINI WANAPOTUMIA VYOMBO VYA MOTO KWA KUZINGATIA SHERIA NA ALAMA ZA USALAMA BARABARANI ILI KUEPUSHA AJALI
ZINAZOWEZA KUEPUKIKA. AIDHA ANATOA RAI KWA YEYOTE MWENYE TAARIFA JUU YA MAHALI
ALIPO MTUHUMIWA AZITOE KATIKA MAMLAKA HUSIKA ILI AKAMATWE NA SHERIA ICHUKUE
MKONDO WAKE, VINGINEVYO AJISALIMISHE MWENYEWE.
WILAYA
YA KYELA
- AJALI YA GARI KUMGONGA MPANDA BAISKELI
NA
KUSABABISHA
KIFO.
MNAMO TAREHE
19.10.2013 MAJIRA YA SAA 12:00HRS
HUKO KIJIJI CHA MPUNGUTI, KATA KATUMBA - SONGWE, TARAFA YA UNYAKYUSA, WILAYA YA KYELA, MKOA WA MBEYA. GARI NO T.318 BYH AINA YA CANTER LIKIENDESHWA NA DEREVA HAMZA S/O MSHANO, MIAKA 35,
MMAKONDE, LILIMGONGA MPANDA BAISKELI
AITWAYE JULIUS S/O MWAMBELO, MIAKA
38, MNYAKYUSA, NA MKAZI WA ITENYA NA
KUSABABISHA KIFO CHAKE PAPO HAPO. MWILI WA MAREHEMU UMEKABIDHIWA KWA NDUGU WA
MAREHEMU BAADA YA UCHUNGUZI WA DAKTARI. CHANZO CHA AJALI KINACHUNGUZWA. DEREVA
AMEKAMATWA NA GARI LIPO KITUONI. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA
MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI
ANATOA WITO KWA MADEREVA KUWA MAKINI WANAPOTUMIA VYOMBO VYA MOTO KWA
KUZINGATIA SHERIA NA ALAMA ZA USALAMA
BARABARANI ILI KUEPUSHA AJALI ZINAZOWEZA KUEPUKIKA.
WILAYA
YA MBEYA MJINI – KUFANYA FUJO UWANJA WA MPIRA.
MNAMO TAREHE
19.10.2013 MAJIRA YA SAA 18:30HRS
HUKO KATIKA UWANJA WA SOKOINE JIJI
NA MKOA WA MBEYA. DAVID S/O CHARLES,
MIAKA 23, KYUSA, MKULIMA NA MKAZI WA MAJENGO ANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI
MKOA WA MBEYA KWA KOSA LA KUFANYA FUJO
KATIKA UWANJA WA MPIRA WA SOKOINE KWA KUWARUSHIA JIWE WACHEZAJI WA TIMU YA
MPIRA WA JKT RUVU KATIKA MECHI DHIDI YA MBEYA CITY MARA BAADA YA MPIRA KUISHA
KITENDO AMBACHO SIO TU KUWA NI UVUNJIFU WA SHERIA BALI PIA NI AIBU KWA WANA
MBEYA NA WADAU WA MICHEZO. MTUHUMIWA AMEKAMATWA, TARATIBU ZINAFANYWE ILI
AFIKISHWE MAHAKAMANI. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA
POLISI DIWANI ATHUMANI ANATOA WITO KWA
MASHABIKI NA WADAU WA MPIRA KUACHA VITENDO VYA FUJO NA VURUGU WAKATI WA MECHI.
AIDHA ANATOA RAI KWA YEYOTE ATAKAYEONA MTU/WATU WAKIFANYA FUJO BADALA YA
KUFURAHIA/KUFUATILIA BURUDANI HUSUSANI KWENYE MECHI ZA LIGI KUU TANZANIA BARA
ZINAZOENDELEA ATOE TAARIFA MARA MOJA KWA MAMLAKA HUSIKA ILI HATUA ZA KISHERIA
DHIDI YAO ZICHUKULIWE .
Signed
by:
[DIWANI
ATHUMANI - ACP]
KAMANDA
WA POLISI MKOA WA MBEYA.
No comments:
Post a Comment