Translate

Sunday, October 13, 2013

ajali zauwa Mbarali na Mbeya vijijini


TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI
 “PRESS RELEASE” TAREHE   13. 10. 2013.



WILAYA YA MBARALI - AJALI YA GARI KUMGONGA MTEMBEA KWA MIGUU NA  
                                         KUSABABISHA KIFO.

MNAMO TAREHE 12.10.2013 MAJIRA YA SAA 17:30HRS HUKO MSWISWI WILAYA YA MBARALI MKOA WA MBEYA BARABARA YA MBEYA/IRINGA. GARI NO T.793 CDF AINA YA SUZUKI LIKIEDNESHWA NA DEREVA JOSHUA S/O BRUNO SANGA, MIAKA 41, MKINGA NA MKAZI WA MAKAMBAKO ALIMGONGA MTEMBEA KWA MIGUU AITWAYE FRANK S/O NGUKU, MIAKA 45, MBENA, MKAZI WA MSWISWI NA KUSABABISHA KIFO CHAKE PAPO HAPO. MWILI WA MAREHEMU UMEKABIDHIWA KWA NDUGU ZAKE KWA AJILI YA MAZISHI BAADA YA  KUFANYIWA UCHUNGUZI NA DAKTARI WA SERIKALI.  CHANZO CHA AJALI NI MWENDO KASI. DEREVA AMEKAMATWA, TARATIBU ZINAFANYWA ILI AFIKISHWE MAHAKAMANI.  KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI  ANATOA WITO KWA MADEREVA KUWA MAKINI WANAPOTUMIA VYOMBO VYA MOTO KWA KUZINGATIA SHERIA ZA USALAMA BARABARANI ILI KUEPUSHA AJALI ZINAZOWEZA KUEPUKIKA.


WILAYA YA MBEYA VIJIJINI - AJALI YA PIKIPIKI KUGONGANA NA  
                                                    KUSABABISHA KIFO NA MAJERUHI.

MNAMO TAREHE 12.10.2013 MAJIRA YA SAA 22:30HRS HUKO MASHIWAWALA MBALIZI BARABARA YA MBEYA/TUNDUMA WILAYA YA  MBEYA VIJIJINI MKOA WA MBEYA. PIPIKIPI NO. T. 908 CBC AINA YA SHINEY IKIENDESHWA NA DEREVA EMANUEL S/O NGAO, MIAKA 25, MNDALI, MKAZI WA MBALIZI ILIGONGANA NA PIKIPIKI NO. T 298 BZK AINA YA T/BETTER ILIYOKUWA IKIENDESHWA NA DEREVA ATUPOKILE S/O ANGOLILE, MIAKA 34, MNYAKYUSA, MKAZI WA MBALIZI NA KUSABABISHA KIFO CHA MWARABU S/O ? ANAEKADIRIWA KUWA NA UMRI KATI 30-35 ALIYEKUWA ABIRIA KATIKA PIKIPIKI NO. T.298 BZK  NA KUSABABISHA MAJERAHA KWA MADEREVA WA PIKIPIKI HIZO. CHANZO CHA AJALI KINACHUNGUZWA.  MWILI WA MAREHEMU UMAHIFADHIWA KATIKA HOSPITALI YA RUFAA MBEYA NA MAJERUHI WAMELAZWA HOSPITALINI HAPO. PIKIPIKI ZIPO KITUONI.  KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI  ANATOA WITO KWA MADEREVA KUWA MAKINI WANAPOTUMIA VYOMBO VYA MOTO KWA KUZINGATIA SHERIA ZA USALAMA BARABARANI ILI KUEPUSHA AJALI ZINAZOWEZA KUEPUKIKA.


Signed by:
[DIWANI ATHUMANI - ACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA

No comments:

Post a Comment