Translate

Saturday, October 5, 2013

WILAYA YA ILEJE – MAUAJI.





TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI
“PRESS RELEASE” TAREHE 02. 10. 2013.


WILAYA YA  ILEJE – MAUAJI.


MNAMO TAREHE 01.10.2013 MAJIRA YA SAA 12:00HRS HUKO KATIKA KIJIJI CHA IZUBA WILAYA YA ILEJE MKOA WA MBEYA. SIKWITA D/O NAMWOVE, MIAKA 70, MLAMBYA,  MKULIMA,  MKAZI WA KIJIJI CHA IZUBA ALIUAWA KWA KUKATWA PANGA SHINGONI NA MOHAMED S/O MWAMAHONJE, MIAKA 36, MKULIMA, MLAMBYA, MKAZI WA KIJIJI CHA IZUBA. MBINU NI KUMVIZIA MAREHEMU AKIWA JIKONI NYUMBANI KWAKE NA KUMUUA. CHANZO NI IMANI ZA KISHIRIKINA BAADA YA MTUHUMIWA KUMTUHUMU MAREHEMU KUWA ANAMLOGA. MWILI WA MAREHEMU UMEFANYIWA UCHUNGUZI NA DAKTARI WA SERIKALI NA KUKABIDHIWA NDUGU KWA MAZISHI. TARATIBU ZINAFANYWA ILI AFIKISHWE MAHAKAMANI. KAMANDA WA POLISI  MKOA WA MBEYA  KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI  ANAENDELEA KUTOA WITO KWA  JAMII KUACHA KUSADIKI IMANI POTOFU ZA KISHIRIKINA KWANI ZINALETA  MADHARA MAKUBWA KATIKA JAMII.


WILAYA YA MBEYA MJINI – KUPATIKANA NA BHANGI.

MNAMO TAREHE 01.10.2013 MAJIRA YA SAA 09:00HRS HUKO KATIKA MTAA WA ITIJI JIJI NA MKOA WA MBEYA.  ASKARI POLISI WAKIWA DORIA/MSAKO WALIMKAMATA MOSES S/O SAID MIAKA 17, KYUSA, MKULIMA NA MKAZI WA ITIJI AKIWA NA BHANGI KETE 14 SAWA NA UZITO WA GRAM 70. MBINU NI KUFICHA BHANGI HIYO KATIKA KIBANDA CHAKE CHA BIASHARA YA KUUZA SIGARA. MTUHUMIWA NI MVUTAJI NA MUUZAJI WA BHANGI. TARATIBU ZINAFANYWA ILI AFIKISHWE MAHAKAMANI. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI  ANATOA WITO KWA JAMII  KUACHA KUTUMIA DAWA ZA KULEVYA KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NA NI HATARI KWA AFYA YA  MTUMIAJI.



Signed by:
[DIWANI ATHUMANI - ACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.


No comments:

Post a Comment