Translate

Sunday, October 13, 2013

Mbozi ajali yauwa mtoto wa miaka mitatu na kumjeruhi mama mtoto,Kyela jamaa akutwa na gramu 120 za madawa ya kulevya



TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI
PRESS RELEASE” TAREHE  09. 10. 2013.



              WILAYA YA  MBOZI - AJALI YA  GARI KUACHA NJIA, KUPINDUKA  NA
                                             KUSABABISHA KIFO NA MAJERUHI.
MNAMO TAREHE 08.10.2013 MAJIRA YA  SAA 16:00HRS HUKO KATIKA ENEO LA RELINI – MLOWO  BARABARA YA  MLOWO/KAMSAMBA  WILAYA YA  MBOZI MKOA WA MBEYA. GARI T.353 APR AINA YA  TOYOTA HILUX P/UP  LIKIENDESHWA NA DEREVA  ASIYEFAHAMIKA JINA WALA MAKAZI YAKE, LILIACHA NJIA NA KUPINDUKA KISHA KUSABABISHA KIFO CHA  MTOTO PETRO S/O KAUNDA, MIAKA 3,  KYUSA, PIA MAJERUHI KWA MAMA MZAZI WA MTOTO HUYO AITWAE FAUSTA D/O MBUBA, MIAKA 35, MNYIHA, MKULIMA, MKAZI WA KIJIJI CHA ITEMPULA AMBAYE AMELAZWA ZAHANATI YA NAZARETH - MLOWO. CHANZO KINACHUNGUZWA. DEREVA ALIKIMBIA MARA BAADA YA  TUKIO. MWILI WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA KATIKA ZAHANATI HIYO. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA  KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI  ANAENDELEA KUTOA WITO  KWA MADEREVA KUWA MAKINI WANAPOTUMIA VYOMBO VYA MOTO KWA KUZINGATIA SHERIA NA ALAMA  ZA USALAMA BARABARANI ILI KUEPUKA AJALI ZINAZOWEZA KUEPUKIKA. AIDHA ANATOA RAI KWA YEYOTE MWENYE TAARIFA JUU YA  MAHALI ALIPO MTUHUMIWA AZITOE KATIKA MAMLAKA HUSIKA ILI AKAMATWE NA SHERIA ICHUKUE MKONDO WAKE, VINGINEVYO AJISALIMISHE MWENYEWE.

        

WILAYA YA  KYELA  – KUPATIKANA NA BHANGI.


MNAMO TAREHE 08.10.2013 MAJIRA YA  SAA 16:00HRS HUKO ENEO LA MBUGANI WILAYA YA  KYELA   MKOA WA MBEYA.  ASKARI POLISI WAKIWA DORIA WALIMKAMATA FRANK S/O ARON, MIAKA 27,  KYUSA, MKULIMA, MKAZI WA MBUGANI   AKIWA NA BHANGI MISOKOTO 20 SAWA NA UZITO WA GRAM  120.  MTUHUMIWA NI MUUZAJI  NA MVUTAJI WA BHANGI. TARATIBU ZINAFANYWA ILI AFIKISHWE  MAHAKAMANI. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA  KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI  ANAENDELEA KUTOA WITO  KWA JAMII KUACHA KUTUMIA DAWA ZA KULEVYA  KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NA NI HATARI KWA AFYA YA MTUMIAJI.




 [DIWANI ATHUMANI - ACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.



No comments:

Post a Comment