Wanawake ni wadau wakuu wa maendeleo endelevu!
Kardinali Osca Rodriguez Maradiaga, Rais wa Shirikisho la
Mashirika ya Misaada ya Kanisa Katoliki Kimataifa anasema, Siku ya Wanawake
Duniani kwa Mwaka 2014 inalenga kutambua uwezo wa wanawake katika mchakato wa
maendeleo endelevu sanjari na kutafuta suluhu ya ukosefu wa uhakika wa usalama
wa chakula duniani. Wanawake sehemu mbali mbali za dunia wamekuwa mstari wa
mbele katika kuchangia mustakabali wa maendeleo ya familia na jamii
zinazowazunguka.Wanawake wakiwezeshwa wanaweza kuchangia katika maendeleo endelevu ya Jumuiya ya Kimataifa. Caritas Internationalis kwa kushirikiana na Mfuko wa Fidel Gotz, katika Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani, watatoa jumla ya Euro elfu kumi kwa makundi mawili: Kundi la kwanza ni lile linalotekeleza miradi inayofadhiliwa na Caritas Internationali na sehemu ya pili, Mashirika mengine ya misaada yanayojipambanua kwa kuwajengea uwezo wanawake uwezo kiuchumi. Tuzo hii itatolewa hapo tarehe 16 Oktoba 2014 wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Chakula Duniani.
No comments:
Post a Comment