Translate

Saturday, December 27, 2014

MWENYEKITI WA CHAMA CHA MAPINDUZI(CCM) MBEYA AMSHUKIA WAZIRI MKUU MSTAAFU,WAANDISHI MBEYA WALALAMIKIA KUSAMBAZWA NA KUANDALIWA KWA HOTUBA YA SUMAYE DAR ES SALAAM KABLA YA HAJAWASILI MBEYA





Na Thompson Mpanji

MWENYEKITI  wa Chama cha mapinduzi (CCM) Wilaya ya Mbeya mstaafu,Allan Mwaigaga amemtaka  Waziri Mkuu mstaafu, Frederick Sumaye, kuwaonesha watanzania njia bora na mbadala ya kuwachagua viongozi wasionuka rushwa kwani kuwataadharisha pekee haitasaidia kukomesha vitendo hivyo:sauti na picha ya taarifa ya Mwenyekiti Mwaigaga inapatikana katika You tube mwamfumu kapembamoto.


Aidha baadhi ya waandishi wa habari  mkoani mbeya wamelalamikia hatua ya Waziri mkuu huyo mstaafu  kufanya ziara jijini Mbeya ilhali habari tayari alishaiandaa na kuisambaza kwa wahariri katika vyombo vya habari  jijini Dar es salaam.

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake,uyole,jijini Mbeya Mwaigaga ambaye pia ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Mwaji group amesema Sumaye  hasiwe anawahutubia na kuwataadharisha watanzania kuwa makini na viongozi  wanaotafuta uongozi  kwa kutoa rushwa  huku haoneshi njia ya kuwabaini viongozi hao.

"Sumaye ni mwenzangu  na kaka yangu vijana wa zamani wameshatangulia mbele za haki,tumebaki sisi vijana wa kati kwa hiyo tuwaelekeze njia mbadala  ya kuwabaini viongozi hao wanaonuka rushwa,vinginevyo tutakuwa tunatwanga maji kwenye kinu,sisi viongozi   na vijana wa kati tunalipotosha taifa,kuna ombwe kubwa la maadili ndani ya taifa letu,"alisema.

Aliwageukia waandishi wa habari kuwaonya kuwa licha ya kuwa hawatambuliki rasmi kama mhimili wa nne wa Taifa  lakini ndivyo ilivyo hivyo wajitambue kuwa  wao ndiyo kioo na tegemeo la utulivu na amani wa nchi yeyote hivyo wasikubali kuyumbishwa na kununuliwa na viongozi wala rushwa na kupotosha jamii,

 Siku chache zilizopita Sumaye  akihutubia katika tamasha la uimbaji na kuliombea  lililofanyika  kwenye uwanja wa Sokoine jijini Mbeya.amesema Tanzania inastahili kuongozwa na utawala unaomuogopa Mungu ili kuondokana na vyanzo vinavyohatarisha kuondoka kwa amani nchini.

Katika hotuba yake iliyopatikana jijini Dar es Salaam kwa njia ya barua pepe, Sumaye alisema masuala ya amani yanapojadiliwa nchini, ni lazima kujikumbusha ni nini hasa kinachoharibu hali iliyopo sasa.

 “Kwanza, ni lazima tupambane na mambo yale ambayo ni chukizo mbele za Mungu na tuweke madarakani utawala unaomwogopa Mungu. Wapo watu wanaodhani tukipiga tu magoti Mungu atatuhesabia haki,” alisema.

Alitoa mfano wa Israeli likiwa taifa teule la Mungu, jinsi wafalme wao walipoacha njia za haki na kufanya matendo maovu na Mungu aliwaadhibu, akawaangamiza kwa kuuawa na maadui wao kama Wafilisti au Wakaldiyo.

 “Hivyo ni lazima tuwe tunatenda matendo mema ndipo Mungu tukimwomba atatujalia amani,” alisema na kukumbusha kuwa Waisrael mara zote walipoharibikiwa, walikuwa na mtawala mbovu.

“Hata katika nyakati zetu nchi nyingi zinazopoteza amani mchango mkubwa unatokana na kiongozi mkuu wa nchi husika,” alisema.

Alisema kutokana na hali hiyo, Watanzania wanapaswa kujiandaa kumpata Rais bora katika Uchaguzi Mkuu wa mwakani.

Alisema yapo mambo muhimu ya kuangalia katika uchaguzi huo, akitoa mfano wa kukemea maovu na kumpata kiongozi bora, mambo yanayohitaji umakini mkubwa.

Kwa mujibu wa Sumaye, Rais ajaye anapaswa kuwa mzalendo kwa nchi na wananchi wake, mwenye upeo, kutii utawala wa sheria na demokrasia, kuweka madarakani serikali inayowajibika kwa umma, kupambana na umasikini na ukosefu wa ajira.

Pia, alisema Rais ajaye anapaswa kuwa na utashi wa kuboresha huduma za jamii, kupambana na rushwa, ufisadi, dawa za kulevya na maovu mengine kama ujambazi, mauaji na ubakaji.

Sumaye aliongeza kuwa Rais atakayechukua nafasi ya Rais Jakaya Kikwete, anastahili kuwa na uwezo wa kukuza uchumi imara, kusimamia mapato na matumizi ya fedha za umma.

Alisema kwa hali hiyo, Uchaguzi Mkuu wa mwakani ni kigezo muhimu cha kulinda amani na utulivu na akaongeza, “tunaiomba Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) vyombo vyote vinavyosimamia uchaguzi watende haki bila kupinda hata kidogo.”

Alisema haki ikitendeka pasipo kutia shaka, uchaguzi huo utakuwa wa amani na utulivu utadumu nchini.

Aidha, Sumaye aliviasa vyama vya siasa kuwasimamia wanachama na washabiki wao ili washiriki kuilinda amani wakati wa uchaguzi huo.

Sumaye ni mmoja wa wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wanaotajwa kutia nia ya kuwania urais kupitia chama hicho.

Hata hivyo, Sumaye alishaweka wazi kuwa ikiwa CCM italipitisha jina na mgombea anayekabiliwa na tuhuma za ufisadi wa aina tofauti, hatakuwa tayari kumuunga mkono ikibidi hatakuwa pamoja na waliomo katika chama hicho.



No comments:

Post a Comment