Translate

Tuesday, November 10, 2009

karibuni nyote

karibu wapendwa mabibi na mabwana katika safu hii ya kuzungumzia masuala mbalimbali yanayotuzunguka katika dunia hii.

Asante,

Thompson Mpanji,Mbeya,Tanzania.

3 comments:

  1. karibu wapendwa mabibi na mabwana katika safu hii ya kuzungumzia masuala mbalimbali yanayotuzunguka katika dunia hii.

    Asante,

    Thompson Mpanji,Mbeya,Tanzania.

    ReplyDelete
  2. Na Thompson Mpanji,Mbeya

    MLIPUKO wa homa ya mafua ya nguruwe (African Swine fever) unaoendelea kuwatafuna na kuwateketeza wanyama aina ya Nguruwe mkoani hapa na Wilaya zake hata kuwatia umaskini baadhi ya wafugaji,umeathiri kwa kiasi kikubwa zoezi zima la utoaji wa misaada inayotolewa na Shirika la Caritas na maendeleo Jimbo katoliki la Mbeya ambalo watoto yatima na wanaoishi katika mazingira magumu,wazazi na walezi wao ilikuwa ni msaada mkubwa kwao katika kujikimu na hali ya maisha .

    Akiongea katika Mkutano wa kazi wa Caritas Mbeya,Mratibu wa kitengo cha Jali watoto,Shirika hilo,Pendo Mwaipopo alisema kuwa misaada ya mifugo ya Nguruwe waliyokuwa wakiitoa kwa wazazi na walezi wa watoto yatima na wanaoishi katika mazingira magumu ili waweze kuwasaidia watoto hao kwa huduma na mahitaji mbalimbali ya shule na nyumbani imeingia dosari baada ya Nguruwe waliowatoa kufa kutokana na ugonjwa huo na hivyo kulazimika kusitisha kuitoa.

    Mwaipopo alisema zaidi ya Nguruwe 50 ambao walitolewa msaada na Shirika la Caritas Mbeya kwa wazazi na walezi wa watoto yatima na wanaoishi katika mazingira magumu katika Kata za Iganjo,Iduda,Iganzo na Itenzi wamekufa kutokana na mlipuko wa ugonjwa huo na hivyo kuziacha familia hizo zikiwa hazina chanzo wala mradi wa kuwaingizia fedha kwa ajili ya mahitaji mbalimbali ya kila siku.

    Ametaja idadi katika mabano ya wanyama hao waliokufa katika Kata zilizopatiwa misaada hiyo kuwa ni Iganjo (12),Iduda (11),Iganzo(14) na Itezi (13) na kwamba Shirika limekuwa likitegemea misaada kutoka kwa wafadhiri mbalimbali ambao wamekuwa wakitoa fedha kwa awamu na kuzingatia mahitaji na bajeti iliyoombwa hivyo upo umuhimu wa kujaribu kuliangalia suala hilo upya kwa ajili ya kuziokoa familia hizo zilizoingia katika wakati mgumu bila matarajio.

    Naye Msimamizi wa kituo cha kulea watoto yatima na wanaoishi katika mazingira magumu cha Mtakatifu Kizito kilichopo Mwanjelwa kinachoendesha na Caritas Mbeya,Frola Maketa alisema jumla ya Nguruwe watatu wamekufa katika Kata ya Iwambi na kwamba jitihada zinafanyika ili kubadilisha mradi huo kwa wazazi na walezi ambao bado hawajapatiwa msaada huo kwa kuwasaidia Mbuzi ama kuku.

    Kwa upande wake,Mratibu wa Caritas Mbeya,Anthony Kisengo amewashauri waratibu hao kuangalia upya misaada wanayotoa kwa walengwa baada ya kuathiriwa na ugonjwa huo ili jamii ziweze kupata matunda mapema ya mifugo kama ilivyo kwa Nguruwe na kuku ambao wamekuwa wakizaa watoto wengi kwa wakati mmoja kwa muda mfupi, tofauti na mbuzi anayezaa mtoto mmoja baada ya miezi sita,jambo ambalo litawapa wakati mgumu familia za watoto yatima na wanaoishi katika mazingira magumu kutunza na kujikimu na hali ngumu ya maisha.

    Mwisho.

    ReplyDelete
  3. Na Thompson Mpanji,Chunya



    IDADI ya wataalamu wa tiba ya kikombe inazidi kuongezeka baada ya ‘Babu’Mchungaji mstaafu Ambilikile Mwasapile wa Loliondo, wilayani Chunya Mlemavu wa asiyeona ameibuka na kudai kutibu magonjwa sugu yote ukiwemo Ukimwi,kwa kunywa kikombe kimoja ambapo maelfu ya wananchi wanamiminika kupata tiba hiyo inayodaiwa kutibu kwa matazamio ya muda wa siku 43.



    Hata hivyo taarifa za uhakika zilizolikia gazeti hili zinasema kuwa msaidizi wa mlemavu huyo, aliyemsindikiza kwenda kuchimba dawa hiyo anadaiwa kutouona mti huo kwa mara ya pili baada ya kumtoroka bosi wake na kwenda katika msitu kwa lengo la kuichukua dawa hiyo ili aifanyie biashara.



    Wakiongea na mwandishi wa habari hizi baadhi ya wananchi wa Kijiji ch Mbuyuni wamesema wameanza kupata huduma hiyo bure tangu,aprili,7 mwaka huu na kwamba kuanzia jana mtaalamu huyo ameanza kutoa tiba ya kikombe kwa familia nzima kuchangia kiasi cha sh.500.



    Akisimulia kuibuka kwa mtaalamu huyo mmoja wa wakazi wa Kijiji cha Mbuyuni,Nico Haule amesema mlemavu huyo ambaye ni mkazi wa Kijiji hicho amedai kuoteshwa mara kadhaa na babu yake marehemu lakini alikuwa akidharau hadi ilipofikia siku hiyo alipomuomba kijana mmoja amsindikize kuelekea katika milima ya Iseche,Tarafa ya kwimba,wilayani humo.



    Msaidizi wa mtaalamu huyo,kaburi Mwankumbi alisema kuwa aliombwa na Mahela kumsindikiza katika msitu wa milima ya Iseche na Mkwajuni na baada ya kufika huko alishangaa kumwambia walipokuwa wakielekea syo ulipo mti huo na kuelekeza eneo jingine ambapo kipofu huyo alirudi kinyume nyume na kuukamata mti huo na kumwelekeza auchimbe na kurudi nao nyumbani.



    “Tulichemsha mti huo na akanywa yeye na mimi na majirani sita akiwemo mdogo wake wa kike ambaye ni mja mzito siku ya pili watu baada ya kupata taarifa walifika wengi,nami nilipoona anatoa tiba hiyo bure nikamkimbia ili nikauchimbe mti ule na kuwauzia watu lakini nilishangaa sikuuona kabisa na niliporudi kumwambia (Mahela)alicheka,”alisema Mwankumbi.



    Ofisa Mtendaji wa Kata ya Mbuyuni,Romwad Mwashiuya amethibitisha kuibuka kwa mkazi huyo wa Mbuyuni aliyemtaja kwa jina la Simon Patson Mahela ambaye ni mlemavu wa macho na anaishi kwa msaada wa kuongozwa.



    Mwashiuya alisema, baada ya uongozi kupata taarifa hiyo walifika nyumbani kwake na kuukuta umati wa watu zaidi ya 300 wakiendelea kupata tiba hiyo na baada ya kumhoji aliwaelekeza na hatimaye walichukuwa hatua za awali za kumuongezea vikombe kwani alikuwa akitumia kikombe kimoja kuwanyweshea watu wote,pamoja na kumpatia pipa la kuchemshia dawa sanjari na kuboresha hali ya vyoo.



    Ofisa wa Afya,Bw.Nicholaus Likokolo alisema baada ya kufika katika eneo hilo wameshauri huduma za choo ziboreshwe na kwamba ingawa yupo nje kikazi lakini amepata taarifa kuwa mganga wa kituo cha Afya Mbuyuni amefika pia na kushauri kuchukuwa sample ya dawa na kuipeleka kwa mganga mkuu wa wilaya ya chunya ili aweze kuifikisha kwa mkemia mkuu kwa uchunguzi zaidi.



    Wakati huo huo,Katika mtaa wa mianzini,Kata ya mabatini,jijini Mbeya,babu mtoto jafari fikiri amesikika akiwatangazia wananchi wanaokwenda kunywa kikombe kwake kuwa mtu yeyyote atakayefika kwa nia ya kumjaribu ataona cha mkata kuni.



    Taarifa hiyo amekuwa akiitoa mganga huyo kufuatia kuumbuka kwa mzee mmoja ambaye anadaiwa kufika kumjaribu na kuichafua huduma hiyo ambayo imekuwa kimbilio la wananchi walio wengi kutoka wilaya mbali mbali za mkoa wa Mbeya ambao wanashindwa kusafiri kufika katika kijiji cha samunge,wilayani Loliondo kwa mchungaji babu Ambilikile mwasapila.



    Hata hivyo kuna taarifa ya kupata madhara baadhi ya wananchi waliokunywa dawa hiyo na kukiuka masharti ya kunywa pombe,kuvuta sigara,kutokunywa dawa ya aina yeyote na kutofanya tendo la ndoa kwa muda wa siku nane baada ya kunywa vikombe viwili vya tiba hiyo.



    Mwisho.

    ReplyDelete