Translate

Sunday, February 3, 2013

Saturday, February 2, 2013

Caritas yazidi kushikamana na wenye magumu ulimwenguni

Mshikamano wa Caritas na wananchi wanaoteseka kutokana na vita nchini Mali



Shirika la Misaada la Kanisa Katoliki Uswiss, Caritas limetoa kiasi cha Franc za Kiswiss Laki moja, kama sehemu ya mchango wake kwa ajili ya kuwasaidia watu wasiokuwa na makazi nchini Mali, wanaokimbia vita inayoendelea nchini humo kati ya Vikosi vya Wanajeshi kutoka Ufaransa na Waasi wa Mali. Wahamiaji wengi ni wale wanaotoka Kaskazini mwa Mali na kukimbilia Kati na Kusini; ambako kwa sasa kunaonekana kuwa na unafuu wa ulinzi na usalama.

Taarifa zinaonesha kwamba, kuna zaidi ya watu 9,000 waliokimbilia katika nchi jirani ilikutafuta hifadhi ya maisha yao na wanaendelea kuhudumiwa na wananchi katika maeneo haya. Lakini, kutokana na wingi wa watu na ukosefu wa rasilimali fedha, chakula na mablanketi, wahamiaji hawa wamejikuta wanakabiliana na hali ngumu zaidi. Wanawake na watoto ndio wanaoathirika zaidi kutokana na kinzani pamoja na migogoro ya kijamii inayoendelea sehemu mbali mbali za dunia.

Msaada uliotolewa na Caritas unalenga kutoa walau lishe kwa watoto wanaokabiliwa na utapiamlo wa kutisha, ambao umeongezeka kwa asilia sita pamoja na dawa za kudhibiti magonjwa ya milipuko.

Baba wa Taifa alithamini na kuheshimu uhuru wa kidini, akakazia umoja na mshikamano wa kitaifa!




Mwalimu Julius Kambarage Nyerere alikuwa ni Mchamungu na alipenda kusali na kuwaona watanzania wenzake wakiabudu na kukiri imani kadiri ya dini na madhehebu yao, kama njia ya kukuza na kudumisha uhuru wa kidini, ambayo ni haki msingi ya kila mwanadamu. RealAudioMP3
Katika mahojiano maalum na Radio Vatican, Askofu Michael Msonganzila wa Jimbo Katoliki Musoma, Tanzania anasema kwamba, Mwalimu Nyerere baada ya kung’atuka kutoka madarakani, alitamani kujenga Kanisa ili aweze kupata mahali pa kusali, karibu na nyumbani kwake Kijijini Butiama. Alifanikiwa kupata msaada wa fedha, akajenga Kanisa la Bikira Maria Mama wa Damu Azizi ya Yesu, ambalo kwa sasa ni Kanisa la Parokia ya Butiama, Jimbo Katoliki Musoma.
Baba wa Taifa aliguswa mno na mahitaji ya Waamini wa dini ya Kiislam, Kijijini Butiama, akatafuta msaada wa fedha ili kuwajengea Msikiti mkubwa na mzuri, ambao hadi leo hii umebaki kumbu kumbu tosha kabisa kwamba, kwa hakika Mwalimu Nyerere alikuwa ni mtu aliyejikita katika majadiliano ya kidini, akaheshimu uhuru wa kidini. Askofu Msonganzila anasema, msaada wa ujenzi wa Msikiti wa Butiama kwa Baba wa Taifa ni mchango kutoka kwa Hayati Mohamed Ghaddafi wa Libya.
Kumbe, uvumi kwamba, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere aliwanyanyasa na kuwabeza waamini wa dini ya Kiislam nchini Tanzania hauna msingi wowote ni njama za kutaka kuvuruga amani, utulivu na mshikamano wa watanzania. Mwalimu Nyerere alikazia zaidi na zaidi umoja na mshikamano wa kitaifa, akapinga kwa nguvu zote ukabila, udini na ubaguzi.
Miaka michache tu baada ya kifo chake, watanzania wameanza kubaguana kwa misingi ya: itikadi na vyama vya kisiasa, wakanuniana! Wameingia katika misimamo mikali ya kidini: wakaanza kuchomeana Makanisa. Wameanza pia kubaguana kwa “Mabucha ya nyama”, jambo ambalo halikuwa na uzito wa pekee miaka kadhaa iliyopita, watanzania waliheshimiana na kuthaminiana kwa tofauti zao za Kiimani, wakatambuana kuwa wao jambo la msingi ni Utanzania unaowaunganisha na wale si kabila wala dini ya mtu!
Mtwara kunafuka moto! Rasilimali na utajiri wa nchi ambao unapaswa kuwa ni mali ya watanzania wote unawagawa watanzania! Watanzania wanakoelekea si pazuri!
Akiwa mjini Addis Ababa Rais Jakaya Kikwete wa Tanzania amesikika akisema “Nakaribisha kwa mikono miwili pendekezo la APRM kuwa serikali isimamie kwa uangalifu tofauti za kidini nchini. Kama mnavyojua, Tanzania imekuwa na amani na utulivu kwa sababu tumekuwa na bahati kutokuwa na ugomvi wa kikabila, kidini ama yale ya kutokana na rangi za watu. Hali hii inatokana na ukweli kuwa tumetunga na kuwa na sera zisizokuwa za kibaguzi kwa wananchi wetu kwa misingi ya kabila, dini, rangi ama sehemu anakotoka Mtanzania. Ni sera nzuri na tutazidumisha.”
Aliongeza: “Uzuri kuhusu dini katika Tanzania ni kwamba tunaamini na kudumisha uhuru wa kuabudu kwa kila mtu. Serikali haina dini. Lakini tunajua fika kuhusu hatari zinazoweza kusababishwa na wanasiasa na viongozi wa dini wenye malengo ya kuchochea fujo za kidini. Hatutayumba wala kusita kupambana ipasavyo na watu wa namna hiyo. Pale ambako uchochezi wa kidini unafikia kiwango cha kuhatarisha amani ya nchi ama uvunjifu wa amani na sheria, dola ina haki ya kuingilia kati.”

Thursday, January 31, 2013

Mwanamke anayedaiwa kumuuza mtoto aibuka mafichoni aweka mambo hadharani ni baada ya kumnasa anapoishi na mgahawani,Mama mkubwa anayedaiwa kuwa msimamizi wa kituo cha yatima naye aibukia katika semina ya kiroho atoa ufafanuzi

Na Thompson Mpanji,Mbeya
SAKATA la mwanamke mmoja Mkazi wa Mtaa wa Ikuti,Kata ya Iyunga, jijini Mbeya kutuhumiwa kumuuza mtoto aliyemzaa mwenyewe kwa raia wa kigeni wanaomiliki kituo kimoja cha watoto yatima cha jijini hapa limezidi kuchukuwa sura mpya kunaswa na mwandishi wa habari hizi akiwa mafichoni na kuweka mambo hadharani huku anayedaiwa kuwa msimamizi wa kituo cha Care and Share-Children's home Anna Kasile akiibukia katika semina ya Makatekista akikiri kumsaidia mwanamke huyo na amekuwa akizushiwa kuuza watoto.
Aidha Anna Kasile ambaye anadaiwa kuwa ni mama mkubwa,msimamizi wa kituo aliyedaiwa kuwa muda wote na wazungu hao amepasua ukweli katika semina ya Mapadre,watawa wa kike na kiume na makatekista kuhusu kilichotokea.
Akizungumza na mwandishi wa habari hizi,Amina Nganile (29)ambaye anafanyakazi ya kupika chakula katika mgahawa wa baa moja iliyopo katikati ya Mwanjelwa na Kabwe (jina tunalihifadhi),jijini hapa alikiri kuingia mkataba wa kutunza mimba na wazungu waliopelekwa na Mama yake mkubwa (Anna Kasile) baada ya kuuguwa nusuraya kufa.
Amina alisema yeye ni mama wa watoto wawili akiwemo Agapto mwenye umri wa miaka minne na huyo aliyemzaa Novemba,2013 ambaye anatunzwa katika kituo cha care and share cha Simike kinachosimamiwa na Kasile ambaye ni mama yake Mkubwa.
"Sina hamu na wanaume kwa sababu aliyenizalisha awali hamtunzi mtoto na huyu aliyenizalisha anaitwa Amos Mfanyakzi wa stela Farm ni mkazi wa Kyela hajanitunza wakati wa mimba,niliugua nusura nipoteze maisha na hivyo nilitaka kuitoa lakini Mama Kasile alinisaidia kunipeleka Hospitali wakanipima Ultra Sound na kukuta mtoto yupo hai nami nikatibiwa hadi kupona na nikajifunguwa salama,"amesema.
Ameongeza"nilijifunguwa mtoto wa kiume mwenye uzito wa kilo tatu na siyo kilo nne na kwamba nilikaa naye baada ya muda nikawakabidhi mtoto waende kumtunza na mimi nililazwa na baadaye nikatoka na ninaendelea vizuri na mtoto ninakwenda kumuona."
Alipoulizwa kuhusu mkataba wa kumtunza mtoto hadi baada ya kufikia umri wa mika 18 ndipo atamchukuwa alikiri na kusema ni bora aendelee kukaa huko huko kwa sababu hali yake kiuchumi ni mbaya hata kufikia kudaiwa fedha za mkopo alizokopa katika shirika la mikopo la Eclof Mbeya baada ya kuuguwa na mdogo wake kuufilisi mradi wa mkaa aliomuachia.
"Nilikuwa na stoo ya Mkaa nikiuza kwa madebe na magunia lakini baada ya kuuguwa nilimkabidhi mdogo wangu aendeshe biashara hiyo lakini ilikufa,kwa hiyo nililazimika kuuza kila kitu changu na sasa ninaishi kwa rafiki yangu Nzovwe,hapa nimepata kibarua ninalipwa Sh.2,000 kwa siku sh.1400 pesa ya kula na Sh.600 pesa ya nauli ya dala dala,hali ni mbaya na ninashindwa kulipa deni,"amesema.
Hata hivyo Amina alisema hataki kusikia juu ya wanaume kwa sababu ni wauaji wanapokutaka kimapenzi wana ahadi lukuki lakini baada ya kujifunguwa wanakukana hali inayoweza kusababisha kujiuwa ama kufanya jambo lolote baya kwa hasira baada ya kuchanganyikiwa na anamshukuru Anna Kasile kwa kumnusuru yeye na mtoto wake.
Anna kasile akitoa mada inayozungumzia utetezi wa uhai alisema tangu ajiunge na mikakati hiyo ya kunusuru maisha ya watoto na Prolife amekuwa akikumbana na mikasa mingi ikiwemo kuhojiwa na watu wa ikulu kuwa anajishughulisha kuuza watoto anaowaokota jambo ambalo siyo la kweli.
Akizungumzia suala la Amina amesema baada ya kusikia anataka kutoa mimba kutokana na kutomjuwa mwanaume aliyempa uja uzito huo alilazimika kumsaiia na kuzungumza na wazungu akina Kaufmann waliokubali kumtunza na kumuuguza hadi akapona na kujifunguwa salama na kwamba mtoto yupo hai anaendelea kulelewa katika kituo chake hadi atakapofikia miaka 18 atamchukuwa.
Amesema walilazimika kufika kwa Mwanasheria Mwakolo kwa ajili ya kuwekeana mkataba wa kumtunza mtoto huyo ambapo amedai walilazimika kutoa sh.100,000 kama ada baada ya kuomba kupunguziwa kutoka Sh.150,000.
Wakili Mwakolo hakuweza kupatikana licha ya kumuomba miadi ya kuonana naye kupitia simu yake ya kiganjani baada ya kuomba ufafanuzi wa sheria iliyotumika katika makubaliano ya mkataba wa kutunza mimba sanjari na kufika ofisini kwake januari,29 na 30,2013 bila mafanikio ya kuonana naye.
Ofisa wa Idara ya ustawi wa jamii Mkoa wa Mbeya,Tobias Mwalwego akizungumza na KIONGOZI amethibitisha kupokea mkataba wa makubaliano kutoka kwa wasamaria wema waliolalamikia suala hilo na kwamba kwa kifupi hawakifahamu kituo hicho.
"Leo(januari,30) asubuhi tulikuwa tunajadili mkataba huo ni kitu cha kushangaza wala hakipo katika sheria na taratibu za kuasili mtoto,na ukiangalia kipengere cha nne cha masharti hayo(Kwamba baada ya mtoto kufikisha umri wa miaka 18 MAMA MZAZI ataruhusiwa kumchukuwa mtoto wake) hakiingii akilini kwa sababu atakosa haki za msingi za malezi na mapenzi ya mama,wakati Mama yake yupo,"amesema.
Aidha Ofisa huyo amesema hana uhakika kama kituo cha Care and Share-children's home kama kimesajiliwa kisheria kwa sababu katika idara ya ustawi wa jamii Mkoa wa Mbeya haikitambui wala shughuli zao licha ya mtu aliyefika ofisini kwake kujitambulisha kwa jina la Melvin Kauffman kama Ofisa utawala wa kituo hicho kilicho chini ya Shirika la Harmony International (januari,30,2013).
"Leo amekuja mgeni mmoja akiwa na familia yake akajitambulisha kuwa ni Melvin Kauffman kuwa ni Ofisa utawala wa kituo cha Care and Share kilichopo Simike na kwamba alikuwa anaomba idhini ya kumchukuwa mtoto mmoja yupo Hospitali ya Rufaa Mbeya kitengo cha uzazi Meta kwa ajili ya kumlea na kwamba anawatunza watoto kama hao watatu ambao wanaonekana wakubwa lakini huyo mtoto anayedaiwa kuchukuliwa baada ya mkataba hayupo katika orodha ya watoto aliowaonesha katika picha na maandishi,"amesema Mwalwego.
Amesema kuwa amemjibu Melvin kuwa kabla ya kumchukuwa huyo mtoto aliyekuwa Hospitali atalazimikia kufika katika kituo chake ikiwemo na kufuatilia suala la mkataba wa Amina Nganile na baadaye kujiridhisha kama kituo hicho kimesajiliwa kisheria na taratibu za kuwachukuwa na kuwatunza watoto hao kama zimefuatwa.
Kamanda wa polisi Mkoa wa Mbeya Diwani Athumani ameahidi kulifuatilia suala hilo na kujuwa ukweli na undani wake ili kama kuna tatizo liweze kushughulikiwa na endapo kuna makosa ya kisheria, sheria iweze kuchukuwa mkondo wake.
Mwisho.

Mama adaiwa kumuuza mtoto ni baada ya kuwekeana mkataba wa kutunza mimba na 'wazungu',yadaiwa baada ya kujifunguwa Hospitali ya Ifisi Mbeya wazungu watoweka naye hakumuona hata sura,aliambiwa alimzaa mtoto wa kiume wa kilo 4,akienda kituo cha kulelea watoto Simike adaiwa kuoneshwa watoto yatima waliokotwa


Na Thompson Mpanji,Mbeya
MWANAMKE mmoja  Mkazi wa Mtaa wa  Ikuti,Kata ya Iyunga, jijini Mbeya  amedaiwa  kumuuza  mtoto aliyemzaa mwenyewe kwa wazungu  wanaomiliki kituo kimoja cha watoto yatima   cha jijini hapa ambao hadi sasa haieleweki walipo  pamoja na kichanga chake  kiume kinachodaiwa kuzaliwa  kikiwa na uzito wa kilogramu nne.
Tukio hilo ambalo limewasikitisha wananchi walio wengine  linadaiwa kutokea mwanzoni mwa Novemba,2012 ambapo makubaliano yanadaiwa kufanyika mwezi,oktoba,2012  katika maeneo  ya Ikuti  mbele ya mashahidi  likiwepo  kampuni  moja la  mwanasheria  wa kujitegemea  la jijini Mbeya.
Mwenyekiti wa mtaa wa Ikuti,Kata ya Iyunga,Immanuel Mwasote amekiri kuwepo kwa tukio hilo  na kumtaja mwanamke huyo kuwa ni Amina Nganile ambaye alikuwa akiishi katika mtaa huo na alikuwa mjazito  na  wenzake kuthibitisha alijifungua salama  lakini baada ya siku mbili alionekana bila mtoto jambo lililowashtusha wengi na kumfikisha ofisini kwake kwa kesi mbili.
Mwasote amesema  Amina alifikishwa ofisini kwake  na wanakikundi  wenzake wa kikundi cha Tumaini kwa madai ya kushindwa kurejesha deni la mkopo katika shirika la Eclof sanjari na kumhoji  alikompeleka mtoto  ambapo alijibu yupo ustawi wa jamii akiendelea kulelewa .
“Kutokana na majibu hayo tuliingiwa wasiwasi na ndipo tukampeleka katika kituo cha polisi Iyunga kwa mahojiano na baadaye walimwachilia,kwa hiyo  tuliwaachia polisi waendelee na uchunguzi na baadaye amehama mtaa wangu sijuwi alipokwenda,”amesema.
Akizungumza na Mwandishi wa  gazeti hili Msimamizi wa kikundi Tumaini ,Winfrida Nzunda  amesema  mwenzao huyo  alipokuwa mjamzito   walikuwa wakija wazungu na gari ambalo nambari zake hawakuzishika na kumchukuwa kumpeleka kuhudhuria  kliniki katika Hospitali ya Ifisi na kumrudisha hadi alipojifungua  na kulazwa  siku moja na kutoka bila mtoto.
Winfrida amesema  baada ya kumhoji  alielezea kuwa   baada ya kujifungua  hakuiona sura ya mtoto wake  baada ya kuchukuliwa na wazungu  hao ambao walikuwa wanawake wawili na wanaume watatu zaidi ya kumfahamisha kuwa  amejifungua mtoto wa kiume mwenye uzito wa kilo nne  na kwamba hadi leo haelewi  alipo mtoto wake  na wazungu hajawaona tena.
“Lakini baada ya kumbana sana alituambia kuwa Mama yake huyo aliyemtaja kwa jina la Mama Kasile  anayesimamia kituo cha kulelea watoto cha  For Care & Share-Children’s  Home kilichopo Simike jijini Mbeya  ndiye aliyemshawishi  kuwekeana mkataba na wazungu hao kumhudumia  hadi atakapojifunguwa  baada ya kutomjuwa mwanaume aliyempa mimba  na ndipo watamchukuwa mtoto kumlea hadi baada ya miaka 18  watamrejesha kwake,”amesema.
Msimamizi huyo wa kikundi amesema kuwa  baada ya kumbana zaidi aliwaeleza kuwa  mkataba wa kumhudumia ulimalizika  baada ya kujifungua na hivyo  wazungu hao  walimchukuwa mtoto huyo  na kwamba alipotoka Hospitali alikwenda kwa Mama Kasile ambako alihudumiwa kwa siku nne na baadaye kufukuzwa  kwa madai akajitegemee.
Amesema mwanamke huyo amethibitisha kuwa amedhurumiwa fedha na Mama  huyo kwani ana imani amepewa fedha nyingi  na kwamba katika hatua ya kushangaza  akifika kumwangalia mtoto anaoneshwa wale waliokotwa na kupewa muda wa dakika mbili  aondoke jambo ambalo linathibitisha kuwa mtoto wake ameshatoroshwa kwenda mashariki ya mbali.
Hata hivyo Winfrida amesema kuwa baada ya tukio hilo mwanamke huyo  amehama hapo mtaa wa Ikuti na haileweki anapoishi maeneo ya Nzovwe  na wanaendelea kumsaka  kutokana na kushindwa kurejesha deni la zaidi ya Sh.370,000 katika shirika la mikopo la Eclof  na hivyo wanahofia kufikishwa mahakamni kutokana na deni  la mwenzao huyo.
Meneja wa shirika la mikopo midogo  la Eclof tawi la Mbeya,Magdalena  Lekaaya amethibitisha kukopeshwa  Amina Nganile mkopo wa Sh.400,000 na kutakiwa kurejesha Sh.79,000 kila mwisho wa mwenzi pamoja na wanakikundi wenzake  lakini  baadaye hakuonekana hadi  wanakikundi walipomkamata.
Amesema baada ya kumhoji  na kumtania kwanini ameshindwa kurejesha mkopo ilhali ameshamuuza mtoto  alikiri na kudai hajapewa hata senti moja  na kwamba hana uwezo wa kulipa deni  wamfikishe kokote  na hivyo kumuona  kama amechanganyikiwa na kumwagiza aende kutafuta  hela hiyo chini ya udhamini wa wanakikundi wenzake lakini hajaonekana.
Baadhi ya ndugu,jamaa na marafiki wa Amina kutoka katika kijiji cha Isongole Umalila,wilaya ya Mbeya vijijini  wakizungumza  na gazeti hili wamesikitishwa na kulaani vikali tukio hilo na kjuiomba serikali  iweze kuchukuwa mkondo wake.
Gazeti hili linayo nakala ya mkataba wa makubaliano ya kumuuza mtoto huyo  baada ya ‘wazungu’ hao kutunza mimba  ya mwanamke huyo aliyetajwa kwa jina la Amina Paulo Nganile  na mtoto atayezaliwa  hadi afikie umri wa miaka 18.
Nakala ya mkataba huo una masharti sita yaliyoainishwa  katika kutimiza makubaliano  yaliyofanywa Oktoba,5,2012 kati ya kituo cha kulea watoto maarufu “Watunzaji’ Care & Share-Children’s home wa S.L.P. 573,Mbeya-Tanzania,East Afrika Phone No.0252502749 na Amina Paulo Nganile anayeishi karibu na Itende JKT,eneo la Nzovwe,Mbeya ambaye kwa upande mwingine anaitwa MAMA MZAZI.
Sehemu ya makubaliano hayo yameandikwa kama ifuatavyo:” kwamba watunzaji ni wenye kumiliki kituo cha kulelea watoto wadogo chini ya umri wa miaka 18,kwamba kwa hiari yao watunzaji  na kwa hiari ya MAMA MZAZI ambaye ni mjamzito wamekubaliana  kuwa MAMA MZAZI atatunzwa  na kituo hicho yeye mwenyewe na kusaidia gharama za kujifungua mtoto.
“Kwamba baada ya mtoto kuzaliwa ‘watunzaji’ wataendelea kumtunza  mtoto atakayezaliwa mpaka atakapofikia umri wa miaka 18,kwamba baada ya mtoto kufikisha umri wa miaka 18 ‘mama mzazi ‘ataruhusiwa kumchukuwa mtoto  wake,kwamba matunzo kwa mama mzazi yatakoma mara baada ya kujifungua.”
Sharti la sita limesema,” kwamba MAMA MZAZI hamjuwi aliyempa mimba na hivyo hana uwezo wa kutunza mimba na mtoto atayezaliwa  hivyo anakubali kuwa mtoto atayezaliwa atunzwe  na ‘watunzaji ‘hadi atakapofikia umri wa miaka 18.”
Aidha sehemu ya mkataba huo imesema makubaliano hayo yametiwa sahihi na wahusika wote  mbele ya mwanasheria ambaye ni  Melvin Kauffman wa For care & share-children’s home na ‘Mama Mzazi’ Amina Paulo Nganile na shahidi aliyeandikwa kwa jina la Anna Kasile mwenye nambari ya simu 0754 615021 mbele ya Wakili kutoka kampuni ya Mwakolo and Co.Advocates,P.O.BOX 2908,Mbeya-0754052231 ikiwa imewekwa na mhuri wa kampuni hiyo ya mwanasheria wa kujitegemea.
Jitihada za kumtafuta ‘mama mzazi’ ambaye ni mama wa  kichanga cha kiume   kilichozaliwa na uzito wa kilo nne  zinaendelea ili kupata ukweli  wa tukio hili ambapo anayedaiwa mama mkubwa aliyemshawishi  kumuuza mtoto huyo  alipopigiwa simu  na kuhojiwa kuhusiana na tukio hilo alijibu kwa jazba kuwa hasipotezewe muda
Anna Kasile ambaye anadaiwa kuwa ni mama mkubwa,msimamizi wa kituo aliyekuwa  muda wote na 'wazungu' hao alimwambia mwandishi wa habari hizi kuwa  amuulize vizuri Amina sababu ya yote hayo na ikiwezekana amtafute aende naye kituoni hapo.
Kasile amesema  amehojiwa na watu wengi  ikiwemo waandishi wa habari na polisi kwa hiyo amechoka kujieleza, hawezi kupoteza muda kwa ajili ya masuala ya kipuuzia na hatimaye alikata simu na alipopigiwa zaidi ya mara nne alikata simu licha ya kutumiwa ujumbe mfupi wa maandishi kufafanua tuhuma dhidi yake kuwa amekuwa na kawaida ya kuwauza watoto anaowaokota wametupwa na kuwalea hakujibu.
Jitihada  za  kuwasiliana na Kamanda wa Polisi mkoa wa Mbeya,Diwani Athumani,a Kampuni ya Wakili Mwakolo(Mwakolo and Co. Advocates)  na Ofisi ya ustawi wa jamii  Mkoa wa Mbeya kujuwa  utaratibu wa kuasili watoto na mkataba wa makubaliano  zinaendelea.
 Mwisho.

Taarifa ya Polisi Mbeya,mchungaji mbaroni kwa uchochezi



TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI
“PRESS RELEASE” TAREHE 31. 01.2013.

WILAYA YA MBEYA MJINI   – MUINJILISTI AHOJIWA POLISI KWA UCHOCHEZI.

MUINJILISTI NICHOLAUS S/O LUWONEKO @ KAMWAGILA,UMRI MIAKA 35,MHEHE,MKAZI WA MTONI MTONGANI – DAR ES SALAAM ALIKAMATWA NA MAKACHERO JANA JIONI TAREHE 30.01.2013 HUKO ENEO LA IYUNGA NJE YA KANISA LA MORAVIAN USHIRIKA WA IYUNGA JIJINI MBEYA KWA TUHUMA ZA KUHUBIRI KANISANI HAPO AKITUMIA MANENO YA KICHOCHEZI DHIDI YA DINI NYINGINE.UCHOCHEZI HUO HAUKUWAFURAHISHA BAADHI YA WAUMINI NDIPO WAKATOA TAARIFA. AMEKAMATWA AKIWA PIA NA CD’S NA VIPEPERUSHI AMBAVYO NI SEHEMU YA UCHUNGUZI UNAOENDELEA. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI ANATOA WITO KWA WANA MBEYA /WANANCHI WOTE KUWACHUKIA /KUTOWAKUMBATIA WACHOCHEZI WA MADHEHEBU /DINI YOYOTE ILI KUJIEPUSHA NA MADHARA AMBAYO YAMEKUWA YAKIONEKANA KATIKA BAADHI YA MAENEO NCHINI NA DUNIANI. AIDHA ANATOA PONGEZI KWA WOTE WANAOENDELEA KUTHAMINI AMANI,USALAMA NA UTULIVU HUSUSANI WAUMINI WALIOTOA TAARIFA HII NA KUFANIKISHA KUKAMATWA MUINJILISTI HUYU.JESHI LA POLISI MKOANI  WA MBEYA HALITAVUMILIA KAMWE UCHOCHEZI WA NAMNA YOYOTE MKOANI HAPA.

WILAYA YA MBEYA MJINI - KUPATIKANA NA BHANGI

MNAMO TAREHE 30.01.2013 MAJIRA YA SAA 21:30HRS HUKO UYOLE JIJI NA MKOA WA MBEYA. ASKARI POLISI WAKIWA DORIA WALIMKAMATA TITO S/O SAMSON,MIAKA 21,MKINGA,BIASHARA MKAZI WA UYOLE AKIWA NA BHANGI KETE 42 SAWA NA GRAM 220 KATIKA KIBANDA CHAKE CHA BIASHARA YA KUUZA JUICE NA MAJI .MTUHUMIWA NI  MVUTAJI NA MUUZAJI  WA BHANGI NA TARATIBU ZA KISHERIA ZINAFANYWA ILI MTUHUMIWA AFIKISHWE MAHAKAMANI. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI ANATOA WITO KWA JAMII KUACHA KUTUMIA DAWA ZA KULEVYA  KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NA NI HATARI KWA AFYA YA MTUMIAJI.

WILAYA YA RUNGWE- KUPATIKANA NA BHANGI

MNAMO TAREHE 30.01.2013 MAJIRA YA SAA 21:30HRS HUKO ENEO LA MWISHOLWA- TUKUYU WILAYA YA RUNGWE MKOA WA MBEYA. ASKARI POLISI WAKIWA DORIA WALIWAKAMATA 1.FRANK S/O BENARD, MIAKA 25, KYUSA, MKULIMA MKAZI WA BUJINGA 2.AMBONISYE S/O MLONGOTI, MIAKA 25, KYUSA, MKULIMA MKAZI WA BUJINGA NA 3. EDWARD S/O EDWINE ,MIAKA 30,KYUSA MKULIMA, MKAZI WA MTAA WA BAGAMOYO WAKIWA NA BHANGI MISOKOTO MITATU  SAWA NA GRAM 15 . WATUHUMIWA NI WAVUTAJI WA BHANGI. WATUHUMIWA NI WAVUTAJI WA BHANGI NA TARATIBU ZA KISHERIA ZINAFANYWA ILI WATUHUMIWA WAFIKISHWE MAHAKAMANI. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI ANATOA WITO KWA JAMII KUACHA KUTUMIA DAWA ZA KULEVYA  KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NA NI HATARI KWA AFYA YA MTUMIAJI.


Signed By,
[DIWANI ATHUMANI – ACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.

Monday, January 28, 2013

Maoni ya Wasomi kutoka Roma kuhusu Katiba Mpya ya Tanzania

Maskani > Haki na Amani >  2013-01-26 07:42:11
A+ A- Chapisha ukurasa huu Tuma kwa e-mail






Mchakato wa kukusanya maoni ya Katiba Mpya ya Tanzania unaendelea vyema, awamu ya kwanza ilikuwa ni kuhamasisha na kukusanya maoni kutoka kwa watanzania mmoja mmoja. Hatua ya pili imekuwa ni kukusanya maoni kwa makundi maalum. Yafuatayo ni baadhi ya maoni yaliyotolewa na wanafunzi wanaosoma mjini Roma, kama sehemu ya mchango wao katika kuandika Katiba Mpya ya Tanzania.
1. Kuhusu Mahakama ya Kadhi:
Mahakama hii ni ya kidini na inahusiana na utatuzi wa maswala ya kidini. Hivyo basi, kutokana na kwamba Tanzania yetu tangu kupata uhuru wake inajukana kama nchi isiyo fuata misingi ya dini yoyote, swala la Mahakama ya Kadhi isiingie kwenye katiba; mahakama iendelee kubaki kama mmojawapo wa mihimili mikuu ya nchi inayo ratibu maswala ya dini husika, bila kuihusisha Katiba ya nchi ambayo ni ya wananchi wote wafuasi wa dini fulani na wasio fuata dini yoyote. Mahakama za kidini zisiingie katika katiba kwani Tanzania haina dini.
2. Kuhusu Tanzania kujiunga na OIC
Jumuiya ya Nchi za Kiislam OIC ina malengo na itikadi zake zinazojikita hasa katika masuala ya kidini. Tanzania hadi sasa haina dini yoyote rasmi ila ni wananchi wake wanao abudu kwenye dini na madhehebu mbalimbali. Ikiwa kuna wananchi wanaotaka kujiunga na Jumuiya hii wapewe nafasi kama watu binafsi na si kama nchi. Tanzania isijiunge na OIC kwa kuwa hii ni Jumuiya ya Kidini. Suala la Tanzania kuwa na uhusiano wa kidiplomasia na Vatican halina uhusiano wowote na madai ya baadhi ya watu kutaka Tanzania kujiunga na OIC.
3. Kuhusu mfumo wa Elimu
Kwakuwa Serikali inalo jukumu la kuhakikishia wananchi wake Elimu, mfumo wa Elimu usiwe wa kidini badala yake uendelee kusimamiwa na serikali itakayokuwa madarakani.Mchango wa dini mbalimbali katika sekta hii uendelee kuheshimiwa na kuthaminiwa, ila serikali iliyoko madarakani ndiyo itoe taratibu na sheria (zisizoshikamana na dini yoyote) zinazopaswa kufuatwa katika swala zima la utoaji Elimu.
4. Kuhusu uteuzi wa viongozi wa serikali na wa mashirika ya kiserikali
Uteuzi wa viongozi hawa uzingatie sifa za anayeteuliwa na wala usifanyike kulingana na sera za kiundugu au kidini. Si kwa sababu mteuliwa ni rafiki au ndugu wa Kiongozi fulani au ni muumini wa dini fulani, basi anafaa kushika madaraka. Nyadhifa zitolewe kwa kuzingatia “Mastahili, sifa na vigezo vinavyohitajika.
5. Kuhusu uchaguzi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano.
Hadi sasa watanzania tunajua kuwa bara na visiwani ni Taifa moja na kwamba hatuna tofauti yoyote kama raia. Hivyo basi, kwakuwa Zanzibar na Tanzania bara ni nchi moja, Raisi wa Jamhuri ya Muungano atoke upande wowote ule wa Muungano na kusiwepo utaratibu wa kupata Rais kwa zamu kati ya Tanzania bara na Zanzibar. Utaratibu wa kupata Rais kwa zamu kati ya pande hizo mbili unaweza ukawa hatari na kutishia zaidi usalama na amani ya Taifa kwani inawezekana kutokea kwamba kusitokee aidha mgombea nafasi hiyo mahali ambapo Rais alitakiwa kutokwa kadiri ya mfuno uliopo hadi sasa.
Nafafanua: ikiwa kwa mfano kwenye uchaguzi ujao Rais anapaswa kutokea Zanzibar au bara, na ikatokea kwamba kwenye ukanda huo hakuna mgombea aliyejitokeza, au aliyejitokeza asipigiwe kura, nini kitafanyika? Kumbe kipengele kinachosititza kuwa Rais achaguliwe kwa kuzingatia bara na visiwani kingeweza kuangaliwa upya na kufanyiwa marekebisho ili Rais achaguliwe kutoka eneo lolote la Tanzania.
6. Kuhusu utoaji mimba
Utoaji mimba ni swala linalohusu haki msingi za binadamu zinazoongozwa na dhamiri nyofu. Hakuna serikali yoyote inayoweza kuingilia dhamira ya mwananchi. Kama vile ambavyo serikali haiwezi kumchagulia mwananchi yeyote mwenza wa maisha, au kuwaamuru wananchi kuvaa mavazi yaliyoshonwa kwa mtindo fulani au ya rangi fulani, hali kadhalika, serikali haipaswi kujiingiza kwenye maswala ya kuratibu na kuhalalisha kisheria maswala yanayohusu dhamira na hasa mauaji ya watu wasio kuwa na hatia!
Jukumu la serikali ni kulinda maisha na usalama wa raia wake wote na si kuratibu mauaji ya baadhi ya raia ambao bado hawajazaliwa. Licha ya hilo, mila na desturi za kiafrika si mila za mauaji bali ni mila zinazotetea uhai na kuulinda. Utoaji mimba ni utamaduni wa kifo usiopaswa kukumbatiwa na mwanadamu yeyote na hasa chombo kinacho ratibu maisha ya wananchi kama ilivyo Katiba ya nchi. Katiba ilinde haki za watoto ambao bado hawajazaliwa.
7. Kuhusu ndoa za watu wa jinsia moja
Serikali isitambue ndoa ya watu wa jinsia moja na kuiweka katika Katiba ya nchi, kwa kuwa ni jambo linalo kwenda kinyume na maadili ya kiutu na kijamii. Hivyo swala hili lisipate nafasi katika Katiba ya nchi. Kama ilivyo hoja iliyopita, hata hii inayofuata inahusu dhamira ya mtu binafsi. Kama baadhi ya wananchi wakiamua kuishi muunganiko (kwani haiwezi kuitwa ndoa) wa watu wa jinsia moja, liwe ni chaguo lao binafsi, ila lisitambulike kikatiba! Katiba ya nchi izingatie maadili na utu wema.
8. Uraia wa nchi mbili:
Kuna haja kwa Katiba ya Tanzania kusoma alama za nyakati kwa kuruhusu raia wake kuwa na fursa ya uraia wa nchi mbili pale inapowezekana ili kuweza kufaidi matunda ya jasho la watanzania wanaoishi ughaibuni.