Na Thompson Mpanji,Mbeya
MTANDAO wa
jinsia Tanzania(TGNP) kwa kushirikiana na wanaharakati na wadau
mbalimbali wanatarajia kushiriki Tamasha mapema septemba,3,2013 ambapo
litatoa nafasi na fursa kwa wanaharakati zaidi ya 5,000 kushiriki
kutoka ndani na nje ya Tanzania.
Tukio
hili la siku nne,linajumuisha uchambuzi,utafiti,uanaharakati,kujenga
uwezo,sanaa vyote vikiwa na matokeo dhahiri ili kutoa ama kuonesha
ushuhuda wa yale yanayojiri miongoni mwetu.
Malengo
ya tamasha la jinsia 2013 ni kusherehekea miaka ishirini ya harakati
za ukombozi wa wanawake kimapinduzi inayochangia upatikanaji wa haki za
wanawake,usawa wa kijinsia na haki za kijamii.
Kuongeza
uelewa wa muktadha uliopo kimataifa,wa mfumo dume na uliberali
mamboleo,madhara yake kwa wanawake walioko pembezoni na jamii
zao,mapambano yao dhidi ya mifumo chanya na mingine kandamizi,na
mikakati mbadala kwa ajili ya ukuaji na maendelo endelevu yenye usawa na
haki.
Aidha
kuendeleza uelewa wa nadharia na vitendo kwenye ukombozi wa wanawake
kimapinduzi,ikiwa ni pamoja na kutunza kumbukumbu za mapambano halisi
dhidi ya mfumo dume na uliberali mamboleo,na jinsi ya kuimarisha
ukombozi wa wanawake kimapinduzi katika ngazi zote.
Tunasema
hongera TGNP,wadau na wanaharakati wengine kuazimisha Tamasha hilo
ambalo ninaamini litawapatia mwelekeo wenu katika harakati hizi za
kumkomboa binadamu na hasa mwanamke.
Ninaweza
kusema kuwa Tamasha hilo litasaidia kufanya ufuatiliaji na tathmini
kuhusu mlikotoka,mlipo na mnapoelekea katika harakati hizi ngumu ambazo
kwa wakati mwingine zinahatarisha maisha na hivyo kuhitaji moyo wa
kujitolea na kujituma zaidi kutoka ndani ya sakafu ya moyo,ndani ya
mishipa na damu kwa ujumla.
Tunaamni
kuwa tamasha hilo pia litawaweka pamoja na kupanga mikakati na mipango
kazi itakayotekelezeka katika ngazi zote kwa ajili ya ujenzi wa
harakati za ukombozi wa wanawake kimapinduzi nchini Tanzania,Afrika na
dunia kwa ujumla.
Tamasha
hili litasaidia kuimarisha utambuzi,mitandao,ujenzi wa nguvu za pamoja
na miungano ya ukombozi wa wanawake kimapinduzi kama misingi ya
kuelekea tapo la ukombozi wa wanawake kimapinduzi wa Afrika.
Tunaambiwa
kuwa katika Tamasha hilo kutakuwa na Mada mbalimbali kama vile jinsia
Demokrasia na maendeleo,miaka 20 ya harakati za ukombozi wa wanawake
kimapinduzi,haki na usawa wa kijinsia,tuko wapi na tunakwenda
wapi,Mapambano ya haki ya ardhi na uchumi,rudisha rasilimali kwa
wananchi,mapambano ya ukombozi wa wanawake kimapinduzi kwa ajili ya
Demokrasia kwenye vyombo vya kiserikali na visivyo vya kiserikali.
Mada
nyingine ni pamoja na mabadiliko ya katiba au mapinduzi,Mapambano ya
ukombozi wa wanawake kimapinduzi na ujenzi wa tapo miaka ishirini ijayo
sanjari na ujenzi wa umoja wa Afrika kwa mtazamo wa ukombozi wa
wanawake kimapinduzi.
Kabla
ya kuendelea tuangalie hili Shirika la TGNP linatoka wapi na linafanya
nini katika jamii,ni miongoni mwa mashirika yasiyo ya kiserikali
yanayofanya jitihada mbalimbali katika kuhakikisha tatizo hili
linakomeshwa kabisa na kutoweka katika jamii ya kitanzania na dunia kwa
ujumla.
Ni
shirika la kiraia na kiuharakati,linalotetea mabadiliko ya kijamii kwa
mtazamo wa kifeministi ambayo yanalenga kwenye usawa wa
jinsia,ukombozi wa wanawake,haki za kijamii,kufikia na kumiliki
rasilimali kwa wanawake,vijana na makundi mengine yaliyoko pembezoni.
Dhana
ya TGNP ni kujenga tapo la mabadiliko katika jamii,ambalo litachangia
kuwepo kwa jamii yenye mabadiliko ambayo inatambua na kuthamini masuala
ya jinsia,demokrasia,haki za binadamu na haki za kijamii.
Kwa
mujibu wa Ofisa uhusiano wa TGNP Kenny Ngomuo anasema septemba,3,2013
ni Tamasha la jinsia ambalo huandaliwa na mtandao wa jinsia
Tanzania(TGNP) wakishirikiana na mtandao wa mashirika watetezi wa haki
za binadamu na usawa wa jinsia (FemAct),pamoja na washirika wao
wengine kama mitandao ya jinsia ngazi ya kati ( IGNs),zilizopo katika
ngazi za wilaya,makundi mbalimbali ya kijamii ambayo ni sehemu ya
semina za jinsia na maendeleo (GDSS) za TGNP, na vikundi vingine
ambavyo vimetambuliwa katika utafiti kuhusu harakati za ukombozi wa
wanawake kimapinduzi (TFMB).
Ngomuo
ansaema Tamasha la jinsia ni nafasi ya wazi kwa ajili ya watu
binafsi,mashirika na mitandao,walio katika mapambano
yanayofanana,kubadilishana uzoefu,taarifa,kujengeana uwezo,kusherehekea
mafanikio na kutathmini changamoto zilizo mbele yao,kujenga na
kuimarisha mitandao,na kupanga kwa pamoja mikakati kwa ajili ya kuleta
mabadiliki ya kijamii kwa mtazamo wa kifeministi,kujengeana uwezo ili
kuchangia katika mijadala ya wazi kuhusu maendeleo ya jamii na binafsi.
Ofisa
huyo anasema Lengo kuu la tamasha ni kuwaleta pamoja
wanawake/wanaharakati wa kifeministi na wengineo,ambao wanawamini kwenye
usawa wa jinsia na ukombozi wa wanawake ,kutoka Nyanja zote za maisha
,kutoka vijiji na wilaya za Tanzania,na sehemu mbalimbali duniani,kwa
lengo la uanaharakati na ushirikishanaji wa taarifa kwa masuala
mahsusi.
Anasema
taswira ya TGNP inafanya jitihada za kuwezesha ukuaji wa vuguvugu la
ukombozi wa mwanamke kimapinduzi lenye misingi yake katika jamii hivyo
kupelekea kufanyakazi moja kwa moja na wanaharakati katika makundi ya
kijamii,wanamtandao na makundi ya muungano katika ngazi mbalimbali.
Ngomuo
anasema mkazo mkubwa unawekwa katika kukuza uwezo wa hayo makundi na
mitandao ili yaweze kufanya uchambuzi wa kijinsia na ujenzi wa nguvu ya
pamoja katika kutekeleza mipango yenye kuleta mabadiliko ndani ya
jamii zao na kujenga mahusiano na wengine katika ngazi ya jamii ya
taifa,kikanda na kimataifa.
Anafafanua
zaidi kuwa dhima ya TGNP ni kuwa chachu katika ujenzi wa harakati za
vuguvugu la ukombozi wa mwanamke kimapinduzi unaolenga kubomoa mfumo
dume na mifumo mingine kandamizi ikiwepo ukoloni mamboleo,ubeberu na
ubepari ngazi zote,kutetea,kushawishi na kushinikiza uwepo wa usawa wa
jinsia,ukombozi wa mwanamke kimapinduzi,haki ya kijamii.
Aidha
Ngomuo anabainisha Dira yao ni kuwepo kwa jamii ya Tanzania
inayoheshimu usawa wa jinsia na haki ya kijamii,kusimamia haki za
jamii.
Hata
hivyo anahitimisha kwa kuelezea mafanikio kwa miaka 20 tangu TGNP
ianzishwe ni kuwa imefanikiwa kushawishi sera za umma kuingiza masuala
ya harakati za vuguvugu la ukombozi wa mwanamke kimapinduzi,ikiwepo
kuingiza masuala ya usawa wa kijinsia na haki za kijamii kwenye mifumo
na taasisi ikiwemo na kukuza hamasa na uelewa wa wanachama,washiriki na
serikali,kila lakheri TGNP na wadau wengine katika Tamasha hilo ambalo
litaongeza kasi,ari na nguvu ya kufanyakazi zaidi!!.
tmpanji@yahoo.comwww.mpanjimwanamai.blogspot.com
0765 813180